Wanandoa wa siku hawana uvumilivu na wana tamaa ya fedha na mali, wana ubinafsi, unakuta mmoja ana mshahara mwingine hana anadharaulika na kunyanyaswa. Mwingine akiona jamaa yake kafulia anaachana naye na kwenda kwa msela mwingine asiyetaka watoto wa baba mwingine. Wale watoto inabidi waende kwa babu/bibi kulelewa huko, na hao vikongwe uwezo ukiwaishia watoto wanakimbilia mitaani. Kingine ni usaliti kunapelekea ndoa kuvunjika na watoto kukosa matunzo ya wazazi wote wawili. Kwa ujumla maadili ya ndoa yameporomoka kwa kiwango cha kutisha