Nini sababu ya Polisi kujihusisha na vitendo vya wizi?

Wax wings

Member
Joined
Sep 26, 2019
Posts
15
Reaction score
10
Serikali yetu kwa sasa imewapa uhuru sana kitengo cha usalama mpaka imefikia wakati wanavuka mipaka na kushirikiana na wezi au na watu wengine watenda maovu. Polisi kama tunavyoelewa ni kulinda raia na mali zao lkn leo imegeuka imekuwa kuonea raia na kunyang'anya mali zao.

Imagine Polisi anakula mchongo na mwizi kaibe sehemu fulani ukiitiwa mwanoo sie tupo karibu tutafika on time. Achana na hilo, kuna kitu ambacho mimi nashindwa kuelewa kwanini watoto wa viongozi wa usalama nao wanakuwa na vyeo wakati sio waajiriwa wa Serikali?

Majuzi nimeshuhudia jamaa kashikwa na simu siwezi jua ni ya awizi kweli au laah ila sasa Polisi wamemshika kitu cha kwanza walichomwambia tupe laki mbili na nusu ili tufute kesi, jamaa akagoma akadai aliyeniuzia simu namjua na ni Polisi fulani twendeni kwake akalipe yeye

Wakamchukua ila saa hii naongea yupo ndani anaugulia maumivu anadai kapigwa rungu kwa kosa la kumsingizia afisa. Sasa najiuliza kwani Polisi kwenye mafunzo yao huwa wanafundishwa kupiga tu hamna mbinu nyingine za kisheria wanazopewa labda uchunguzi kwanza kwa jambo walilosikia au wanafundishwa kubebana?

Yote kwa yote nchi hii kwa sasa kama huna pesa huna haki Serikali inabidi iangalie wanyonge mikoani watu wanateswa sana, Polisi wameshika mikoa kama ndio wenye nchi.
 
Tangu zamani, polis wa bongo wanashirikiana na majambazi. Labda ni mfumo tulio ukubali. Hali ilikua mbaya sana wakati wa WBM Mungu amrehemu.

Nakumbuka, 1995 hadi 2000, tunduma border, Mambazi walikua wakifunga mtaa saa nne Usk na kituo kikubwa cha polis kiko hapo.
 
Serikali yetu kwa sasa imewapa uhuru sana kitengo cha usalama mpaka imefikia wakati wanavuka mipaka na kushirikiana na wezi au na watu wengine watenda maovu. Polisi kama tunavyoelewa ni kulinda raia na mali zao lkn leo imegeuka imekuwa kuonea raia na kunyang'anya mali zao.
Maslahi madogo.
 
Ugumu wa maisha. Mshahara wa muuza mtunda
Wala sio ugumu wa maisha!!SIO KILA MTU ANA FAA KUWA ASKARI., Nenda tra, takukuru, bandari ambako wanalipwa vizuri mambo ni yale yale tu, ukiingia kwenye anga zao!

Mbona wazee wa zamani waliweza kuishi kwa kufuata miiko ya kazi?
 
Tabia binafsi za mtu usifanye ndo tabia ya Taasisi nzima polisi

Kuna vijana malimbukeni kwenye izi taasisi hao ndo ttzo JWTZ na Polisi

Izi taasisi zinaajiri vijana ila haziwapi elimu na pia aziwafundishi kueshimu wananchi ambao ndo waajiri wao
 
Nyumba na gari.

Hivi ndio vitu vikubwa viwatesao watanzania walio weng na si polisi tu.na kidogo kwenye elimu na afya
Sasa Chakufanya hapa serikali inatakiwa

1)Ijikite barabara kwenye mfumo wa National housing.miradi mikubwa ya kujenga mamilioni ya nyumba za serikali nchi nzima na wananchi wapange humo kwa kodi ndogo mno watu wasiwe na ulazima wa kujenga nyumba binafsi.

2)Kodi za magari ziwe halisia gari isichukuliwe kama kitu cha anasa..mtu alipie ushuru wa 3% wa bei ya kununulia.wengi wata afford kuagiza na kumiliki magari kwa unafuu

3)serikali iboreshe elimu iwe kiwango na standard iwe sawa na shule za private hususan shule za mission..na ipunguze gharama za kusomesha kwa hadi 70%...mfano badala ya ada ya mwaka kulipia 2m...mwananchi alipe 250,000

3)hospital matibabu free.

Haya yote yanawezekana kabisa sababu Tanzania ya 70s maisha haya yalikuwepo na nchi nyingi zilizoendelea wanaishi kwenye mifumo ya namba hii.yakifanyika haya wizi na ufisadi nchini vitapungua sana .
 
Askari ni wapumbavu,wanadai mishahara wakati wanamiliki bunduki; “by mobutu seseseko “
 
Hawa Polis wetu aiseee ni mtihani sana
Serikali yetu kwa sasa imewapa uhuru sana kitengo cha usalama mpaka imefikia wakati wanavuka mipaka na kushirikiana na wezi au na watu wengine watenda maovu. Polisi kama tunavyoelewa ni kulinda raia na mali zao lkn leo imegeuka imekuwa kuonea raia na kunyang'anya mali zao.

Imagine Polisi anakula mchongo na mwizi kaibe sehemu fulani ukiitiwa mwanoo sie tupo karibu tutafika on time. Achana na hilo, kuna kitu ambacho mimi nashindwa kuelewa kwanini watoto wa viongozi wa usalama nao wanakuwa na vyeo wakati sio waajiriwa wa Serikali?

Majuzi nimeshuhudia jamaa kashikwa na simu siwezi jua ni ya awizi kweli au laah ila sasa Polisi wamemshika kitu cha kwanza walichomwambia tupe laki mbili na nusu ili tufute kesi, jamaa akagoma akadai aliyeniuzia simu namjua na ni Polisi fulani twendeni kwake akalipe yeye

Wakamchukua ila saa hii naongea yupo ndani anaugulia maumivu anadai kapigwa rungu kwa kosa la kumsingizia afisa. Sasa najiuliza kwani Polisi kwenye mafunzo yao huwa wanafundishwa kupiga tu hamna mbinu nyingine za kisheria wanazopewa labda uchunguzi kwanza kwa jambo walilosikia au wanafundishwa kubebana?

Yote kwa yote nchi hii kwa sasa kama huna pesa huna haki Serikali inabidi iangalie wanyonge mikoani watu wanateswa sana, Polisi wameshika mikoa kama ndio wenye nchi.
 
Hali yao ya maisha ni duni. Nchi za wenzetu , waajiriwa wa serikali wana mishahara mikubwa zaidi ya sekta zingine
 
Tamaa ya kujipatia utajiri wa harakaharaka imewatawala lakini pia ushirikiano wa baadhi yao na majambazi ni sababu nyingine.
 
Tabia binafsi za mtu usifanye ndo tabia ya Taasisi nzima polisi

Kuna vijana malimbukeni kwenye izi taasisi hao ndo ttzo JWTZ na Polisi

Izi taasisi zinaajiri vijana ila haziwapi elimu na pia aziwafundishi kueshimu wananchi ambao ndo waajiri wao
Brother acha kuteteza uovu...Tanzania hakuna wizi...nenda tunduma pale ujionee wafanya biashara wanavyoibiwa usiku, na kituo cha polisi kipo pale pale jirani hawaangaiki na lolote?! Hata wanainchi wakienda kureport zaidi sana wanahitaji hela tena....ki ufupi jeshi hili lifumiliwe lote...hakuna imani na taasisi yooote...PERIOD!!!
 
Back
Top Bottom