Kunguru wa Manzese
JF-Expert Member
- Apr 20, 2016
- 12,729
- 18,119
Wana njaa hao sio poa bora hata maofisa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mishahara bongo ni modogo sana ndiyo inayochochea rushwa,wizi n.k unajua police pesa anayochukua(taking home)baada ya makato,na ana familia ujue,ana watoto wanasoma ujue na ana watu wanaomtegemea.Serikali yetu kwa sasa imewapa uhuru sana kitengo cha usalama mpaka imefikia wakati wanavuka mipaka na kushirikiana na wezi au na watu wengine watenda maovu. Polisi kama tunavyoelewa ni kulinda raia na mali zao lkn leo imegeuka imekuwa kuonea raia na kunyang'anya mali zao.
Imagine Polisi anakula mchongo na mwizi kaibe sehemu fulani ukiitiwa mwanoo sie tupo karibu tutafika on time. Achana na hilo, kuna kitu ambacho mimi nashindwa kuelewa kwanini watoto wa viongozi wa usalama nao wanakuwa na vyeo wakati sio waajiriwa wa Serikali?
Majuzi nimeshuhudia jamaa kashikwa na simu siwezi jua ni ya awizi kweli au laah ila sasa Polisi wamemshika kitu cha kwanza walichomwambia tupe laki mbili na nusu ili tufute kesi, jamaa akagoma akadai aliyeniuzia simu namjua na ni Polisi fulani twendeni kwake akalipe yeye
Wakamchukua ila saa hii naongea yupo ndani anaugulia maumivu anadai kapigwa rungu kwa kosa la kumsingizia afisa. Sasa najiuliza kwani Polisi kwenye mafunzo yao huwa wanafundishwa kupiga tu hamna mbinu nyingine za kisheria wanazopewa labda uchunguzi kwanza kwa jambo walilosikia au wanafundishwa kubebana?
Yote kwa yote nchi hii kwa sasa kama huna pesa huna haki Serikali inabidi iangalie wanyonge mikoani watu wanateswa sana, Polisi wameshika mikoa kama ndio wenye nchi.
Hata ungeajiri nani kwa mishahara hii sioni suruhisho.Brother acha kuteteza uovu...Tanzania hakuna wizi...nenda tunduma pale ujionee wafanya biashara wanavyoibiwa usiku, na kituo cha polisi kipo pale pale jirani hawaangaiki na lolote?! Hata wanainchi wakienda kureport zaidi sana wanahitaji hela tena....ki ufupi jeshi hili lifumiliwe lote...hakuna imani na taasisi yooote...PERIOD!!!