Nini story au kisa nyuma ya username yako na avatar yako hapa JF

Hayo majina ni ya muunganiko wa atom ili kupata molecule.

Vander Wo Forces ni very weak bond btn atom. Covalent & Ionic ni very strong bonds. Nasemea kunganisha uhusiano wenu kuanzia ktk kufafana kwenu
 
Hayo majina ni ya muunganiko wa atom ili kupata molecule.

Vander Wo Forces ni very weak bond btn atom. Covalent & Ionic ni very strong bonds. Nasemea kunganisha uhusiano wenu kuanzia ktk kufafana kwenu

Lakini hayo si majina tu au tumeshakuwa molecules sasa? Anyway acha tuone
 
Dah mkuu haya ni magonjwa yaangu sana napenda sana kusikiliza hizi sauti za kispaniola zikiimba...sasa next time ukiwa unacruise na ur Novia hebu tupia hii kitu ya Don Omar na Jlo iitwayo "Hold you down" Hakika utopenda ufike haraka muendako kiongozi..
 
Dah mimi jina langu na avator yangu vina stori ya kusikitisha sana......

Kuna siku rafki yangu mmoja alikufa. Akafa weeeeeeeeeeeeeeeeeeeee....Mi nkajua utani kumbe akafa bana.....Sasa mi nkasema inakuwaje anakufa tu hivi hivi......Serikali ikashusha bei ya umeme...

Ndo hivyo asee...Huwezi amini yani
 

Hahahaha..... Umenichekesha tena si kidogo
 
Rafiki ako katisha hahaha
[emoji4] [emoji4] [emoji4]
 
Nilipokuwa advanced level pale ihungo boys bukoba
Niliweka print za "chief" kwenye mashati yangu yote ya tomato ili yasiibiwe, niliandika chief kwa sababu nilikuwa na ndoto za kuja kuwa chief executive officer wa kampuni yangu kubwa ya agro processing(iko on process)
Basi wanafunzi wote walinifahamu kwa jina la chief
 
Jina hili la KATA KUCHA ninalotumia humu lilitokana na kufurahishwa na jamaa mmoja aliyekuwa akifanya biashara yake Ubungo Mataa.

Kuna siku tukiwa kwenye foleni tukisubiri kuruhusiwa huku nikiwa nimejiinamia kwenye siti kwa uchovu baada ya kukaa foleni muda mrefu, mara huyu jamaa mfanyabiashara akafika dirisha akinadi bidhaa yake "....kata kuchaaaaaa...nauza kikata kuchaaa....." kwa sauti ya mkwaruzo kidogo.

Wote tulokuwa kwenye gari tukageuka kutazama aina ya 'vikata kucha' anavyoviuza. Kuhamaki kumbe jamaa amebeba MAJAMBIA yanang'aa mno na makali haswa na ndio bishara yake. Sote ndani ya gari tulicheka sana kwa namna hivyo vikata kucha vilivyo.

Alikuwa akitumia lugha ya kuficha ukali wa maneno badala ya kunadi " nauza jambia" yeye aliita vikata kucha. Na ndio ID yangu. Maana alinisogezea "vikata kucha" vyake karibu zero distance na nilipokaa kuhamaki kumbe ni Jambia.
 

Bertha, Beatrice, Bernadeta, Belinda etc
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…