Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikiota ndoto niking'atwa na mbwa na ndoto hii imekuwa ikijirudia mara kwa mara. Nimejaribu kuwauliza wachungaji, manabii na watu mbalimbali wanipe tafsiri ya ndoto hii 'iliyoniganda' kwa miaka mingi sasa lakini sijafanikiwa kupata jawabu. Najua humu kuna manabii, wachungaji na watu wenye pako tofauti wanaoweza kunisaidia kuotolola (kutafsiri) ndoto hii. Inawezekana hili likawa aina fulani ya pepo chafu linalotaka kuniangamiza. Nikijua aina ya pepo hili itakuwa rahisi kupanga mkakati wa kulikemelea mbali kabla halijanidhulu.
Nawasilisha.
:israel:
Few tips kuhusu ndoto (Biblical Perspective)
1. Kwanza ndoto ni bayana au halisi (kuna watu zaidi ya 10 kwenye biblia waliota ndoto na ikawa kweli, Mfano Yakobo, Yusufu, Mwokaji na Mnyweshaji wa mfalme Farao, Mfalme Suleiman, Daniel, Mfalme Nebukadreza, Yusuph mumewe Mariamu, Mke wa Pilato, Mamajusi wa mashariki.
Wote hawa waliota ndoto na zikawa kweli, hata mfalme Suleiman alipata ufalme na utajiri kupitia ndoto.
2. Ndoto ikijirudia maana yake jambo hilo ni hakika na ni lazima litokee (Mfalme Farao aliota ndoto ikajirudia mara mbili, Yusuph akamwambia kuwa kwa kuwa imejirudia maana yake ni ya muhimu sana. Pia kurudia kwa ndoto maana yake unapuuzia.
3. Ndoto ni lugha ya mawasiliano ya rohoni, Mungu au shetani anaweza kuja kwa njia ya ndoto
4. Vitu unavyoviona kwenye ndoto vyaweza kuwa sio exactly what they look like, mfano unapoona mbwa haina maana kuwa ni mbwa kweli... kawaida kuna sheria ya rohoni ya kubadilisha maumbo inayotumiwa na ufalme wa Mungu na hata shetani pia, ni kanuni. Mfano Yesu baada ya kufufuka aliwahi kuwatokea wanafunzi wake akiwa na sura nyingine (Mark 16:12). Therefore, mtu mbaya kama mchawi anapokuja kukudhuru anavaa sura nyingine ili usimtambue, hii ni kanuni ya rohoni. Mchawi huyo anaweza kuwa ndugu yako anajua utamwona na kumtambua hivyo ananuizia umbo lolote, mbwa, paka, nyoka, n.k
5. Kwa ufahamu wangu ndoto hiyo sio nzuri hata kidogo, tafadhali tafuta msaada wa haraka sana kwa mchungaji mwenye maarifa ya ndoto, nakushauri uende kwa any pastor anayesali Ufufuo na Uzima, Kawe; they are experts in that area.
Alternatively, ningekuwa mie nikishtuka tu kwenye hiyo ndoto naanza kuivunja hapo hapo kisitokee kitu chochote kibaya kinachopangwa katika ulimwengu wa roho, in the name of Jesus. Kwa taarifa yako matatizo ya watu yanaanzia rohoni na huwa wanayaona katika ndoto ila hawajui what they mean and their impacts. Ndoto ni monitoring system ya maisha ya mtu na ndio moja ya sababu Mungu kuweka usingizi.
I have a lot to say about dreams lakini hayo ni machache sana.