Jamani usiku wa kuamkia leo nimeota kuwa pinda amefika ofisini kwangu,tukaanza kuongelea habari za katiba. Tukabishana sana kuhusu mjadala wa katiba ulivyohodhiwa na ccm. Mwisho akaniambia hawezi kuendelea kubishana na mtumishi wa umma mwenye mlengo wa upinzani. Nakumbuka nilimwambia kuwa watumishi wengi wa umma upinzani upo myoyoni na si majukwaani, akamwamuru RAS aniwajibishe Mara moja. Mara nikasikia hodiii, Mzee mmoja amefika Asubuhi sana akiwashitaki Polisi kwa kumwomba pesa bila kosa wakati yeye ni mlalamikaji. Ila jamani hii si mara ya kwanza,wakati uchaguzi wa 2005 unakaribia niliota,nikmwona mkapa akigombana na Kikwete kwenye corridor ya muhindi mmoja anaitw a Iqbar,yupo upanga jirani na salander bridge. Hoja kubwa kwao ilikuwa nani atakuwa waziri mkuu Kikwete akiwa rais.