Nini tija ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kwa Walimu?

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,252
Reaction score
36,513
Amani iwe kwenu,

Katika tafakuri yangu weekend hii nimejiuliza maswali kadhaa kuhusu faida wanayoipata waalimu kupitia chama chao cha waalimu kitaifa.
Kuna mambo kadhaa yanayotafakarisha nikaona vyema nije kwenu wanaJF tusaidiane kupata majibu.
  1. Tukianza na usajili wa chama cha waalimu, je ni cha kiserikali au NGO?
  2. Chama hiki kilianzishwa kwa takwa la waalimu au setikali iliwaundia chama chao kama inavyounda bodi za kudhibiti taaluma mbalimbali Tanzania?
  3. Chama hiki kinapokea makato na michango ya waalimu kutoka kwenye mishahara yao. Je michango au tozo hizo zinamfaidisbaje mwalimu kiuchumi kwa sababu siyo kodi ya serikali.
  4. Je chama kina mamlaka ya kusimamia taaluma za walimu? Chama kinaweza kumfutia mwalimu cheti chake cha ualimu?
  5. Umiliki wa mali unaofanywa na chama, kunawafaidishaje waalimu kwenye faida zitokanazo na mali hizo?
  6. CWT kimekuwa kikitambulishwa kwenye sherehe za Mei Mosi na serikali imekuwa ikitoa majibu ya matatizo ya waalimu kwa kuaddress chama chao.
  7. Chama hiki kama kinasimamia waalimu. Je vipi uhusika wa usimamizi wake kwenye utoaji wa taaluma yaani ustawi wa mitaala na qualitative education?
  8. Kwa nini serikali inapenyeza watu wake kushika nafasi za juu za uongozi wa chama hiki? Najua ninalolisema
Lengo la uzi huu ni kutambua malengo, wajibu na kazi za chama cha walimu (CWT).

Pia walimu mliopo humu mnakionaje chama hiki kama kinakidhi takwa la umoja wa waalimu au ni eneo lingine la siasa za Tanzania?

Zaidi ya stress na kukandamizwa na kunyonywa kwenye michango ya kila mwezi hakuna lingine la maana! Chama kiliundwa kimkakati kuwafubaza walimu kwenye harakati zao za kudai haki zao na ikafikiriwa wanaweza kujiunga na upinzani kuangusha mbuyu
 
Walimu kuwa na chama kuna faida kubwa sana kuliko hasara, ni kama simba walivyo na chama a.k.a mwamba wa lusaka anawasaidia sana kwenye magoli.
Hivyo chama ni muhimu sana kwa walimu.
 
Mimi naamini kuwa CWT pamoja na mapungufu yake bado kina umuhimu wake. Kumbuka kuwa mwajiri mkuu kwa nchi zinazoendelea ni serikali Kwa hiyo Kwa lolote like lazima ukubaliane na serikali.
 
Zaidi ya stress na kukandamizwa na kunyonywa kwenye michango ya kila mwezi hakuna lingine la maana! Chama kiliundwa kimkakati kuwafubaza walimu kwenye harakati zao za kudai haki zao na ikafikiriwa wanaweza kujiunga na upinzani kuangusha mbuyu
Serikali inatumia mfumo wa kikoloni wa divide and rule
 
Walimu kuwa na chama kuna faida kubwa sana kuliko hasara, ni kama simba walivyo na chama a.k.a mwamba wa lusaka anawasaidia sana kwenye magoli.
Hivyo chama ni muhimu sana kwa walimu.
Chama
Jumuiya
Umoja

Nadhani hata jina linasawiri shughuli za chama
 
Ni jambo jema kuzungumzia umuhimu wake
Umoja ni nguvu,Shirda ninayo Iona mimi ni aina ya viongozi wanaochaguliwa au kuteuliwa katika vyama hivyo wengi wao hujali maslahi yao zaidi Kwa hiyo nirahisi kutumiwa
 
Umoja ni nguvu,Shirda ninayo Iona mimi ni aina ya viongozi wanaochaguliwa au kuteuliwa katika vyama hivyo wengi wao hujali maslahi yao zaidi Kwa hiyo nirahisi kutumiwa
Naomba kufahamu malengo mahususi na malengo ya kimkakati ya CWT
 
Makato yake yamezidi kuwa mzigo kwa wanachama ifikie hatua hiki chama kikate flat rate kwa walimu maana kina vitega uchumi vingi sana na havimnufaishi mwalimu moja kwa moja hivyo ifikie hatua stahiki zichukuliwe ili kumpunguzia mwalimu mzigo wa makato au mbona nyama vingine vinakata moja tu kwa mwaka pale wanapikuwa na mazungumzo na serikali basi kukata mwalimu kila mwisho wa mwezi tena kwa asilimia huu ni unyonyaji mkubwa sana.Ili nalo mkalitizame tafadhali
 
Kwenye kipengere cha mchango wa Kila mwezi kingeangaliwa upya, yafanyike mabadiliko
 
Nilipoona Magreth Sitta alikuwa Rais wa CWT akagombea ubunge na alivyoshinda JK akampa uwaziri wa elimu kisha akawasaliti walimu wenzake basi niliishiwa hamu.

walimu wangekuwa wanajitambuwa wao ndio makarani wa uchaguzi wangetumia fursa hiyo kuiadhibu Ccm, lakini wenyewe ndio wamegeuka makuwadi wa kuratibu wizi wa kura.
 
Ni kweli adui wa mwalimu ni mwalimu mwenyewe,wakipata teuzi Huwa wanasahau kuwa na wao walikuwa walimu
 
Zaidi ya stress na kukandamizwa na kunyonywa kwenye michango ya kila mwezi hakuna lingine la maana! Chama kiliundwa kimkakati kuwafubaza walimu kwenye harakati zao za kudai haki zao na ikafikiriwa wanaweza kujiunga na upinzani kuangusha mbuyu
Kiongozi stress za walimu hazisababishwi na CWT, Hilo ni swala la mwalimu na mwajiri wake. Kabla hujakubali kufanya kazi yeyote lazima kwanza kufahamu mazingira, maslahi na changamoto za kazi husika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…