Nini tija ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kwa Walimu?

Ngoja nimtag mwamba aje a achangie huu uzi
mpwayungu village

Ova
CWT sio Chama cha serikali bali ni taasisi inayomilikiwa na walimu,hiki Chama nichakiharakati chenye lengo la kumtetea mwalimu pale anapopata matatizo pamoja nakutetea maslahi ya walimu

UHALISIA : kwasababu cwt viongozi wao wengi nipandikizi, Wala rushwa, Majizi ndio maana hakijali tena walimu wanajijali wenyewe. Mwalimu unaweza kusitishiwa mshahara wako Kwa sababu mbalimbali ukaamua kwenda Kwa viongozi wa CWT wakutetee lakini hawafatilii na Wala hawajali matatizo yako
 
Kwa uchache malengo ya vyama vya wafanyakazi ni kutetea maslahi na haki za wanachama wao, ama vile mazingira Bora ya kufanyia kazi, mishahara inayoweza kukizi mahitaji n.k
Wanahitaji kumkata mwalimu pesa kwa ajili ya kumtetea maslahi yake?
HIzo gharama zinatumikaje!?
 
Adui wa mtu ni wale wa nyumbani kwake.


Walimu wanasalitiana kama ambavyo wabunge wanavyowasaliti wananchi
 
Je mazingira ya kazi yanahusika kwenye wajibu wa chama kwa wanachama wake?
 
Mimi siioni labda waje wenyewe waalimu watwambie
 
Ukijua kazi ya hawa hapa utajua kazi hicho chama
  1. ACT Waz
  2. Chapa ya Jogoo Magomeni Uslama
  3. Chama cha wenye Mandevu kule Buguruni
 
Hata Magufuli alikuwa Mwalimu, Kassimu Majaliwa ni Mwalimu pia.
Huyo mwl wamchongo. Walimu maafisa vipenyo hata kazi hawafanyi ndio maana wakipata huo Urais wala hawajui shida za walimu
 
Ukijua kazi ya hawa hapa utajua kazi hicho chama
  1. ACT Waz
  2. Chapa ya Jogoo Magomeni Uslama
  3. Chama cha wenye Mandevu kule Buguruni
Mapandikizi siyo?
Kwa hivyo walimu wanahusika kwenye kura?
 
kile chama hamna kitu zaidi ya kuwanyonya walimu,hela ya CWT wanayomkata mwalimu inaelekeana na hela ya NHIF ambapo anakuwa na wategemezi sita
mi nilipendekeza angalau wakate 0.2% ili inayobaki waielekeze kwenye mfuko wa bima
hayo yote hayawezekani maana chama ni cha maticha ila nyuma yake kina watu wazito
 
Mimi ulivyotumia neno takeaway kwenye maelezo yako inanimate ukakasi sana ;kwenye kiswahili hakuna umoja ama uwingi wa matakwa iwe umoja au uwingi neno ni moja tu yaani matakwa tu,yapo maneno mengi hayana uwingi au umoja
 
Lengo la vyama vingi vya wafanyakazi ikiwa ni pamoja na CWT ni kuwagawa wafanyakazi dtu wale wahenga tukumbuke enzi za JUWATA chama kilikuwa na nguvu maana kilikuwa kinaunganisha wafanyakazi wote
 
Huyu Mama sitta aliunda kampuni tanzu ndani ya cwt ya kusimamia biashara za cwt na ndiyo inayomiliki mwalimu house pale ilala na mapato yake hayaeleweki yanakoingia na wakurugenzi wake siyo walimu. Nina wasiwasi kuwa hata hiyo benki siyo ya walimu na huenda ipo chini ya Mama sitta! Walimu wameibiwa mno na cwt ndio maana mh. Magufuli alikionya na kutaka kuifuta Ile benki.
 
Hakina msaada, viongozi wapo kwa ajili ya maslahi yao na si ya walimu,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…