Nini tofauti baina ya Arts in Education na Arts with Education?

Konzogwe

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2008
Posts
434
Reaction score
156
Wadau heshima yenu! Naomba mnisaidie haya yafuatayo, kwanza naomba tofauti ya hizi university programes kati ya:
BA. Arts in Education na BA. Arts with Education.
Pili, hivi mtu aliyesoma digree ya Fine Art kama iliyoanzishwa Udom, ataifanyia kazi gani mfano hapa Tanzania? Kweli kuna soko la ajira zake?
Natanguliza shukrani.
 
Kuhusu tofauti bado natilia shaka ingawa kwa kuangalia unaweza kung'amua tofauti ya hizo kozi. BA. with education ni purely ualimu. na hiyo nyingine natilia shaka kama inafanana na niliyofafanua.
Ila kwa hapa Tanzania wanazuoni wanaofaulu kusoma bidhaa ya arts wanashindwa kuiaply kwenye daily do kwa kuwa hawana background zenye msingi huo.
Ni ubabaishaji wa kuchukua watu wa fani nyengine na kuwabembeleza kujiunga na masomo kwa fani hii hasa waje kuwa maafisa utamaduni na kazi zifananazo na hizo. bila kusahau ualimu.

Soko la ajira ya sanaa kwa tanzania ni kubwa sana ila tatizo hakuna kiwanda cha kuwaandaa washika soko.

Ninasomea sheria niweze kuitumia katika sanaa zangu na wenzangu nchini.
 
Mnisaidie majibu jamani! Nini tofauti yake?
 
Arts in Education & Arts with education
 
Nafikiri una maana ya tofauti ya Bachelor of Education in Arts na Bachelor of Arts with Education

Bachelor of Education in Arts ni degree ya ualimu kwenye masomo ya arts. Ni kama tu unavyoenda chuo cha ualimua kusomea ualimu. Kwa mfano unaweza kusomea ualimu kwenye masomo ya English na Kiswahaili. Kama unataka kufundisha basi hii ndio yenyewe.

Bachelor of Arts with Education ni degree ya BA kama zingine ila una specialize kwenye ualimu. Mwanzoni unasoma kama wanafunzi wengine wa BA lakini major yako inakuwa kwenye education. Hii course unaweza kuwa mwalimu lakini pia unaweza kuwa mwajiriwa wa aina nyingine kwenye sekta ya elimu na hata nje ya ualimu.

Inategemea lengo lako ni lipi lakini kama unataka kuwa mwalimu muda wote basi bora hiyo ya juu. Lakini kama unaona unaweza kufanya kazi tofauti na kufundisha darasani basi ya pili inafaa zaidi.
 
Nilishamueleza awali lakini nikaona hana imani hata kidogo ndo maana nikamtumia passage asome mwenyewe.
 

Tofauti kubwa ni kuwa Arts in education wanaandaliwa kuwa walimu wa vyuo vya ualimu kwenye masomo ya arts au ma administrator kwenye elimu. Hivyo masomo mengi wanayosoma ni ya ualimu na somo moja la kufundisha let say English. Lakini BA with education wanaandaliwa kwa ajili ya kufundisha shule za sekondari hivyo wao wanasoma masomo ya ualimu kwa kiwango kidogo sana na kujikita zaidi kwenye masomo ya mawili yanayofundishwa kwenye shule za sekondari za A-level mfano atasoma zaidi English na Historia na kidogo sana ualimu.
 

Asante sana mkuu. Hii naona imekaa vema. To recap: 'in education' inaandaa 'wakufunzi' (kufundisha namna ya 'kufundisha'!) wakati 'with education' inaandaa walimu katika fani/masomo fulani.
 
Mwabeja sana/asanteni sana/msengwile/songela zigizigi/thanks a lot/mkorire bhuya/mwakondya/ashee
 
hongera sana mimi nasoma in education na ndivyo ilvyo safi kwa ufafanuzi mzuri sina la kuongeza hapo
 
Mimi nimechaguliwa BA OF EDUCATION,sasa wanandugu hii yenyewe inakuwaje au inahusika na nini?Naomba mnisaidie pia
 
Wadau vipi kuhusu barchelor of science in physics unakuwa nani baada ya kusoma na vp kuhusu ajira naomba msaada wen wa maelezo ya kina karibuni
 
Mimi nimechaguliwa BA OF EDUCATION,sasa wanandugu hii yenyewe inakuwaje au inahusika na nini?Naomba mnisaidie pia

Unakuwa mtaalamu wa mambo ya elimu lakini katika mwelekeo wa arts. Utasoma masomo ya ualimu na somo moja la kufundisha mfano: history na education subjects. kawaida walimu hawa huandaliwa kuwa walimu wa vyuo lakini kutokana na uhaba wa vyuo husika huwa wanapelekwa hata secondary kufundisha.
 
Wadau vipi kuhusu barchelor of science in physics unakuwa nani baada ya kusoma na vp kuhusu ajira naomba msaada wen wa maelezo ya kina karibuni

baada ya kumaliza unakuwa mtaalamu wa fizikia hivyo chansi ya kuajiriwa ni kuwa utapambana kwenye soko la ajira na watu waliosoma fani zingine lakini zenye mwelekeo wa fizikia. Kikawaida masomo kama hayo huwa yanawaandaa academicians na si professionals (nina maana kuwa academicians wanakuwa wamebobea kwenye somo husika hivyo huitajika zaidi katika taasisi zinazohusika na mambo ya utafiti kuhusu somo husika). Hawa mara nyingi hawatakiwi kuwa wengi na kawaida wanatakiwa kuwa vichwa kwelikweli ili wabaki kwenye vyuo vikuu au taasisi za kitafiti lakni si kwenye kuajiriwa ambako kunahitaji watendaji kazi professionals..
 
Okey ndo hivo,sory bt chuon wameeandi hvo pekee,bt i think in arts mkubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…