NINI TOFAUTI KATI YA MZIMU NA
PEPO
Watu wengi hawajui tofauti iliyopo
kati ya mzimu ( Ghost ) na pepo (
Demon ). Tofauti ni hii hapa.
MZIMU NI NINI?
Zipo nadharia nyingi zinazo elezea
mzimu ni kitu gani, nadharia iliyo
zoeleka ni ile inayosema mzimu ni
roho ya mtu aliye kwisha kufa. Mtu
huyo anaweza kuwa amekufa zamani
sana, ama muda mfupi ulio pita. Sitaizungumzia sana nadharia hii leo, isipokuwa nitazungumzia kwa ufupi
nadharia nyingine inayo jibu mzimu
ni kitu gani.
Mzimu ni nishati ( energy), roho au
haiba ( personality) ya mtu ambaye
amefariki dunia lakini imekwama
katika sehemu iliyo kati ya duniani ( ulimwengu wa nyama/ulimwengu
unao onekana ) na mahali ambapo
roho hiyo inatakiwa kwenda kuishi
baada ya maisha ya hapa duniani
kukamilika ( ulimwengu usio onekana/ afterlife/ land of the souls )
. Watafiti wengi wana amini kuwa roho hizi zinakuwa hazijui kama
zimekufa katika ulimwengu wa nyama ama hazitaki kuamini kama zimekufa
katika ulimwengu wa nyama ama
hazikubaliani na kifo chao katika
ulimwengu wa nyama. Mara nyingi
roho hizi huwa ni roho za watu
ambao walikufa katika mazingira
yanayo tatanisha kama vile kufa kwa
kuuliwa bila sababu ( cold blood), kutolewa kafara, ama kufa baada ya
maisha ya msukuleni. Kwa ufupi hizi
huwa ni roho za watu ambao
walidhulumiwa haki yao ya kuishi
hapa duniani. Mizimu inaweza
kujidhirisha na kuonwa na wanadamu
ama wanyama katika namna tofauti
tofauti kama vile muonekano ( hapa
mizimu ,huwatokea ndugu, jamaa na
marafiki zao wakiwa katika maumbo
ya sura zao wakati wanaishi duniani
na mara nyingi huwatokea wakiwa
na nguo walizo penda kuzivaa wakati
wa uhai wao ), sauti, harufu( hapa
kwenye harufu mzimu unapo mtokea
muhusika,hujidhihirisha kwa harufu
yake ya mwili ( kila mtu ana harufu yake ya mwili, watu huweza
kuwatambua watu wao wa karibu kwa harufu zao za mwili ), ama pafyumu ( katika pafyumu, mzimu utamtokea
mtu kwa harufu ya marashi ambayo
alikuwa anapenda kuyatumia wakati
yupo duniani katika ulimwengu wa
nyama. Wakati mwingine, mzimu
huweza kuwatokea ndugu jamaa na
marafiki zake kwa kuwashika.
Kwa ufupi mzimu huwa ni roho
ambayo imewahi kuishi katika
ulimwengu wa nyama kama
mwanadamu ama mnyama.
PEPO ( DEMON ) Hawa ni roho
waovu ambao hawajawahi kuwa
wanadamu .Mara nyingi mapepo
huwa na mitego mingi na huwa na
tabia za kitoto kitoto sana (
Nitalizungumzia hili hapo baadaye ).
Haiwezekani kuwazungumzia mapepo
kwa parandesi moja pekee, hii ni kwa
sababu kuna mambo mengi sana
ambayo yanatakiwa kuzungumzwa
kuhusu mapepo, maelezo ninayo
yatoa hapa yanawazungumzia mapepo katika namna ambayo wanatofautiana
na mizimu.
N.B: Mapepo ni wajanja sana, wakati mwingine huweza kuwatokea ndugu, jamaa, na marafiki wa mtu ambaye
amekufa wakijifanya wao ndio roho
wa mtu huyo na hivyo kuanza kutoa
maelekezo ya kufanya kwa ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu
ambapo mwisho wa siku, wahusika
wanajikuta wakiwa wamefungwa na
nguvu za giza zitendazo kazi zake
kutoka kuzimu. Ni muhimu sana kujua
namna unavyo weza kutofautisha kati
ya roho ya mtu aliyekuwa anaishi
na roho za mapepo hawa ambazo
huwatokea wahusika kwa ajili ya
kuwadanganya..
TOFAUTI kubwa kati ya mizimu na
mapepo ni kwamba, mizimu ni roho
za watu ambao waliwahi kuishi hapa
duniani kama binadamu ilihali
mapepo ni roho ovu ambazo
hazijawahi kuishi duniani kama
wanadamu.