Nini tofauti kati ya mzimu na pepo

Nini tofauti kati ya mzimu na pepo

Mapepo ni nini? Ni mali ya shetani anbaye ni mtawala wao, yesu anasema ibilisi na malaika zake, ni malaika walioanguka au kuasi.
'na malaika wasio ilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu. Yuda 1;6"
mapepo wawapo katika mwili wa mtu wanaweza kumfanyia vituko mbalimbali kama vile
1. Kuku vunjia ndoa
2. Kukufungia kipato chako
3.wanaweza kukufungia ufahamu ukiwa darasani,nyumbani nk.
Muzimu ni aina ya mapepo yatumiayo sura au kivuli cha mtu fulani mashuhuri aliyekufa ndani ya ukoo husika ndio maana baada ya yeye kufa huanza kujitafutia mtu mwingine ndani ya ukoo huo atakaye umiliki. Nao waweza kuja kwa mtu kwa njia ya uvamizi wa ndoto au sura ya mtu furani aliyekufa ndani ya ukoo.
Kwa maana nyingine niseme kwamba ndani ya ukoo wako yuko mtu aliyefunga mkataba na mizimu akafungamanishwa na roho hiyo kwa agano la kutambika au kupeana zawadi fulani au kwa kufanyiana sherehe fulani kwa bahati mbaya mtu yule amefariki nndani ya ukoo huo lakini kumbuka ameacha amefunga mikataba na mizimu ndani ya ukoo huo hivyo ule mzimu unaanza kutembea ndani ya ukoo ukijitafutia mtu wa kulinyuu upya mkataba.
"kutoka 20;5..........nawapatiliza wana maovu ya baba zao hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao;
kumbe kwa kuwa babu yako aliingia katika maagano na mizimu, roho hiyo imefungamanishwa na ukoo huo....................
MUNGU AKUBARIKI KWA SWALI LAKO ZURI...........
Jiongeze unaweza ukaelewa badaye vifungu vya bible ulivyotoa ni kwa uelewa wako
 
acha nitoe elimu,mzimu ni mashetani yaliyoishi katika vichwa vya mababu na mababa yanayodumisha mila za ukoo huo au kabila hilo,yanatoa maelekezo kupitia ndoto,yanauwezo wa kujigeuza sura ya mababu zako na mababa zako waliopita na kutoa maelekezo ndotoni,Pepo ni mashetani waasi wanaomshawishi mwanadamu kwenda kinyume na maamrisho ya mungu muumba,si pepo wala si mzimu ambao wana asili ya binadam

Dhana ya.mizimu ni pana...pamoja na hyo pia
Ni 'miungu ya familia' kwa jina lingine.....
Mungu atusaidie tuendelee kufunguka
 
Kama mzimu ni nafsi ambayo haikuamini kama imekufa,je hiyo nafsi nayo hufa badae? Na je ni wapi makao yake?
 
3984cb92fbf60c8cc9d9517a65f048fe.jpg

NINI TOFAUTI KATI YA MZIMU NA
PEPO
Watu wengi hawajui tofauti iliyopo
kati ya mzimu ( Ghost ) na pepo (
Demon ). Tofauti ni hii hapa.
MZIMU NI NINI?
Zipo nadharia nyingi zinazo elezea
mzimu ni kitu gani, nadharia iliyo
zoeleka ni ile inayosema mzimu ni
roho ya mtu aliye kwisha kufa. Mtu
huyo anaweza kuwa amekufa zamani
sana, ama muda mfupi ulio pita. Sitaizungumzia sana nadharia hii leo, isipokuwa nitazungumzia kwa ufupi
nadharia nyingine inayo jibu mzimu
ni kitu gani.
Mzimu ni nishati ( energy), roho au
haiba ( personality) ya mtu ambaye
amefariki dunia lakini imekwama
katika sehemu iliyo kati ya duniani ( ulimwengu wa nyama/ulimwengu
unao onekana ) na mahali ambapo
roho hiyo inatakiwa kwenda kuishi
baada ya maisha ya hapa duniani
kukamilika ( ulimwengu usio onekana/ afterlife/ land of the souls )
. Watafiti wengi wana amini kuwa roho hizi zinakuwa hazijui kama
zimekufa katika ulimwengu wa nyama ama hazitaki kuamini kama zimekufa
katika ulimwengu wa nyama ama
hazikubaliani na kifo chao katika
ulimwengu wa nyama. Mara nyingi
roho hizi huwa ni roho za watu
ambao walikufa katika mazingira
yanayo tatanisha kama vile kufa kwa
kuuliwa bila sababu ( cold blood), kutolewa kafara, ama kufa baada ya
maisha ya msukuleni. Kwa ufupi hizi
huwa ni roho za watu ambao
walidhulumiwa haki yao ya kuishi
hapa duniani. Mizimu inaweza
kujidhirisha na kuonwa na wanadamu
ama wanyama katika namna tofauti
tofauti kama vile muonekano ( hapa
mizimu ,huwatokea ndugu, jamaa na
marafiki zao wakiwa katika maumbo
ya sura zao wakati wanaishi duniani
na mara nyingi huwatokea wakiwa
na nguo walizo penda kuzivaa wakati
wa uhai wao ), sauti, harufu( hapa
kwenye harufu mzimu unapo mtokea
muhusika,hujidhihirisha kwa harufu
yake ya mwili ( kila mtu ana harufu yake ya mwili, watu huweza
kuwatambua watu wao wa karibu kwa harufu zao za mwili ), ama pafyumu ( katika pafyumu, mzimu utamtokea
mtu kwa harufu ya marashi ambayo
alikuwa anapenda kuyatumia wakati
yupo duniani katika ulimwengu wa
nyama. Wakati mwingine, mzimu
huweza kuwatokea ndugu jamaa na
marafiki zake kwa kuwashika.
Kwa ufupi mzimu huwa ni roho
ambayo imewahi kuishi katika
ulimwengu wa nyama kama
mwanadamu ama mnyama.
PEPO ( DEMON ) Hawa ni roho
waovu ambao hawajawahi kuwa
wanadamu .Mara nyingi mapepo
huwa na mitego mingi na huwa na
tabia za kitoto kitoto sana (
Nitalizungumzia hili hapo baadaye ).
Haiwezekani kuwazungumzia mapepo
kwa parandesi moja pekee, hii ni kwa
sababu kuna mambo mengi sana
ambayo yanatakiwa kuzungumzwa
kuhusu mapepo, maelezo ninayo
yatoa hapa yanawazungumzia mapepo katika namna ambayo wanatofautiana
na mizimu.
N.B: Mapepo ni wajanja sana, wakati mwingine huweza kuwatokea ndugu, jamaa, na marafiki wa mtu ambaye
amekufa wakijifanya wao ndio roho
wa mtu huyo na hivyo kuanza kutoa
maelekezo ya kufanya kwa ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu
ambapo mwisho wa siku, wahusika
wanajikuta wakiwa wamefungwa na
nguvu za giza zitendazo kazi zake
kutoka kuzimu. Ni muhimu sana kujua
namna unavyo weza kutofautisha kati
ya roho ya mtu aliyekuwa anaishi
na roho za mapepo hawa ambazo
huwatokea wahusika kwa ajili ya
kuwadanganya..
TOFAUTI kubwa kati ya mizimu na
mapepo ni kwamba, mizimu ni roho
za watu ambao waliwahi kuishi hapa
duniani kama binadamu ilihali
mapepo ni roho ovu ambazo
hazijawahi kuishi duniani kama
wanadamu.

a6e7483d414d02b895e802747c67c4d1.jpg
 
Nitakujibu kwa kifupi sana ijapokuwa hii ni mada ndefu mno.

Mizimu ni MAJINI, na mapepo ndo hayohayo MAJINI, PERIOD!

-Utofauti unakuja pale namna wanavyofanya kaz ktk vitengo vyao tofautitofauti.

-Mizimu imekaa ktk ngazi za kifamilia, ukoo, kikanda, kitaifa n.k na haya huwa yanakuwa yana nguvu saaana.

-Mapepo nayo ndo hayo hayo majini, sema mapepo mengi yanakuwa yanatengenezwa na wachawi/waganga. Huwa hayana nguvu saaana tofauti na yale majini hasa ambayo hayajatengenezwa na wanadamu.
 
Kazi kwelikweli
Nilijifunza enzi nasoma mafundisho ya komonio ya kwanza na kipaimara kwamba

Mungu ni nani??
Jibu mungu ni roho halisi kamili kabisa hakuanza wala hatakwisha

Now naona pepo na.mizimu nao ni roho

Wana amken kumekucha huyo mungu,pepo na mizimu hivyo vitu havipp..

Kuna mahala nilisikia kuna pepo mchafu ina maana kuna pia kuna pepo msafi but mchungaji anapo omba anasema pepo toka kwa jina la yesu..je likitoka pepo safi badala ya chafu??

Akili za iman mnazijua wenyewe aisee
 
SAFI SANA WANATUIBIA
 
acha nitoe elimu,mzimu ni mashetani yaliyoishi katika vichwa vya mababu na mababa yanayodumisha mila za ukoo huo au kabila hilo,yanatoa maelekezo kupitia ndoto,yanauwezo wa kujigeuza sura ya mababu zako na mababa zako waliopita na kutoa maelekezo ndotoni,Pepo ni mashetani waasi wanaomshawishi mwanadamu kwenda kinyume na maamrisho ya mungu muumba,si pepo wala si mzimu ambao wana asili ya binadam
Ni kweli mkuu, umesema sahihi, Mizimu inapenda kuabudiwa ndio maana inajifanya watu waliokufa ili itambikiwe matambiko ya kuyaabudu,
Na huwa inadumu kwenye jamii au ikoo unayoyaabudu kwa muda wote kama yataendelea kuabudiwa na ukoo husika.
Mapepo au Majini, ni jamii ya mashetani walioasi na kulaaniwa, huwa yanapenda kukaa ndani ya mtu ili kumhalibu na kumpotosha asitii amri za Mungu.
Mizimu, Mapepo zote ni Roho Chafu au Dirty Spirit.
 
Likud upo vizur kwenye nyanja hizi big up likud
 
Suala la mizimu kuwa ni watu waliyokufa ni mchezo tu anaoucheza shetani,ingekuwa mtu akifa anaweza kuja tena Ulimwenguni basi angeweza kutuambia yanayoendelea huko na kama alikuwa mtu muovu basi hiyo ingekuwa ni nafasi ya kutubia.
 
Ukisema holy ghost sio mzimu wala pepo umekosea, ukijua ghost ni nini basi kuongeze holy ni unafuu wa ghost yaani ghost mtakatifu lakini ni walewale
 
Mapepo ni nini? Ni mali ya shetani anbaye ni mtawala wao, yesu anasema ibilisi na malaika zake, ni malaika walioanguka au kuasi.
'na malaika wasio ilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu. Yuda 1;6"
mapepo wawapo katika mwili wa mtu wanaweza kumfanyia vituko mbalimbali kama vile
1. Kuku vunjia ndoa
2. Kukufungia kipato chako
3.wanaweza kukufungia ufahamu ukiwa darasani,nyumbani nk.
Muzimu ni aina ya mapepo yatumiayo sura au kivuli cha mtu fulani mashuhuri aliyekufa ndani ya ukoo husika ndio maana baada ya yeye kufa huanza kujitafutia mtu mwingine ndani ya ukoo huo atakaye umiliki. Nao waweza kuja kwa mtu kwa njia ya uvamizi wa ndoto au sura ya mtu furani aliyekufa ndani ya ukoo.
Kwa maana nyingine niseme kwamba ndani ya ukoo wako yuko mtu aliyefunga mkataba na mizimu akafungamanishwa na roho hiyo kwa agano la kutambika au kupeana zawadi fulani au kwa kufanyiana sherehe fulani kwa bahati mbaya mtu yule amefariki nndani ya ukoo huo lakini kumbuka ameacha amefunga mikataba na mizimu ndani ya ukoo huo hivyo ule mzimu unaanza kutembea ndani ya ukoo ukijitafutia mtu wa kulinyuu upya mkataba.
"kutoka 20;5..........nawapatiliza wana maovu ya baba zao hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao;
kumbe kwa kuwa babu yako aliingia katika maagano na mizimu, roho hiyo imefungamanishwa na ukoo huo....................
MUNGU AKUBARIKI KWA SWALI LAKO ZURI...........
 
hivi huu ulimwengu usionekanaa upo hapa hapa duniani? na je shetani anishi maeneo gani? ulaya south africa au ujerumani
 
Back
Top Bottom