mashakaDaima
Member
- May 3, 2013
- 38
- 5
Onyesha ni ku Onya yaan kutoa Angaliz😵nesha linatokana na Mzizi ona kwa hiyo Onesha ni kusaidia kutazama, mfano ni sahihi kusema Ameonesha kilipo kikwazo sio ameonyesha kilipo kikwazo. Mfano.Ni maonesho ya Biashara sio maonyesho.
'Onyesha' yatoka kwenye mzizi 'onya' na 'Onesha' yatoka kwenye mzizi 'ona'. 'Kuonya' ni tofauti na 'kuona'.Si sahihi kusema:'Juma ametuonyesha mpira'.Sahihi ni 'Juma ametuonesha mpira'. Si sahihi kusema 'Kutakuwa na maonyesho'.Sahihi ni kusema 'Kutakuwa na maonesho'. Kuonya ni kukaripia au kutisha.Kuona ni kutazama kwa ajili ya kutambua. Kwahiyo,chochote kihusucho kutazama,kuangalia na kuchungulia,neno sahihi ni ona(kuona/kuonesha).
Sasa kwa nini kamusi zina neno "onyesha" likimaanisha kutazama?
Ina maana wale wataalam wote walioshiriki kuzitunga hizo kamusi wamekosea?
Kwa hiyo nikisema Vuta-Nkuvute "ananionea" nitakuwa namaanisha yeye anaona kwa niaba yangu au nitakuwa namaanisha hanitendei haki?
Nakushauri ufungue kamusi ua TUKI uangalie maana ya "onyesha" kabla hujaja na simulizi zisizo na mamlaka.
usihadaike na hilo jiamini, zinakosolewa Pinalcode za kisheria itakuwa hizo kamusi , Mzizi wa Neno ni Ona sio Onya, ona inazaa Onesha na Onya inazaa Onyesha!
Mkuu, lugha kama yalivyo mavumbuzi mengine, hufanyiwa review mara kadhaa kupata utengamavu. Hapo mwanzo neno ONYESHA lilitumika kweli na sishangai ukiniambia kuwa lipo kwenye kamusi ya TUKI lakini si neno sahihi.
Kama TUKI watatoa toleo jipya la kamusi, hilo neno ONYESHA halitatumika kwa maana ya zamani. Kwa kifupi neno sahihi ni ONESHA na hiyo ni kwa mujibu wa BAKITA, review ya mwaka 1998. Neno 'onyesha' lina maana isiyo rasmi ya MAONYO kutokana na shina ONYO
TUKI toleo la 2010
(chapa ya tano) lina "onyesha".
Oxford toleo la 2012 lina "onyesha"
Na hao BAKITA katika ukurusa wa tovuti yao wanatumia "maonyesho". Kama
huniamini bofya
hapa.
Onyesha ni ku Onya yaan kutoa Angaliz😵nesha linatokana na Mzizi ona kwa hiyo Onesha ni kusaidia kutazama, mfano ni sahihi kusema Ameonesha kilipo kikwazo sio ameonyesha kilipo kikwazo. Mfano.Ni maonesho ya Biashara sio maonyesho.
Niwekee mamlaka inayoeleza hivyo.
Onyesha ni ku Onya yaan kutoa Angaliz😵nesha linatokana na Mzizi ona kwa hiyo Onesha ni kusaidia kutazama, mfano ni sahihi kusema Ameonesha kilipo kikwazo sio ameonyesha kilipo kikwazo. Mfano.Ni maonesho ya Biashara sio maonyesho.
mamlaka gani unayozungumzia hapa ya MBINGUNI AU YA BODI YA PAMBA.???
Mkuu ingawa tunatofautiana kiitikadi,ila hapa uko sahihi!
.Je na hapa lipi neno sahihi "yupo sahihi" au "yuko sahihi".....!???
.
Hapa, "yuko" itakuwa ina maanisha sehemu au mahali,ila "yupo" inahusika na mtu mwenyewe moja kwa moja.Kwa hiyo yupo sahihi ni sahihi zaidi. Naweza kusahihishwa!