Nini Tofauti ya Leaded na Unleaded Petrol?

Asante kwa hio kwa wenye magari ya kisasa una uamuzi wa kuweka yoyote tu kati ya leaded na unleaded sio?

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu gari za kisasa nyingi kwenye manual yake zinasema utumie unleaded...baadhi ndio unaweza tumia leaded ukitaka ila at your own risk. Ni vema kuithamini gari kutokana na specs ulizopewa.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa maelezo yaliyoshiba,vipi sasa kuhusu Yale magari ambayo mdau kaeleza hapo juu (yenye valve mbili) kwamba bila Lead yanaweza kunock? Hawa wanafanyaje kama lead imepigwa marufuku?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa maelezo yaliyoshiba,vipi sasa kuhusu Yale magari ambayo mdau kaeleza hapo juu (yenye valve mbili) kwamba bila Lead yanaweza kunock? Hawa wanafanyaje kama lead imepigwa marufuku?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ngoja nipitie comment ya mdau afu nitarejea. Ila kwaufupi ni kwamba. Yawezekana magari hayo ni yale ya teknolojia ya zamani sana. Ila kwasasa hakuna kampuni ambayo inazalisha mafuta yenye kiambato cha risasi (Lead).
 
Asante kwa hio kwa wenye magari ya kisasa una uamuzi wa kuweka yoyote tu kati ya leaded na unleaded sio?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sina uhakika sana Kama Kuna petrol yenye lead kwa sasa , Mana kampuni nyingi zilikuja na additives ambazo ni salama zaidi, kwa mfano Total wana kitu kinaitwa excelium .

Neno super lilikuwa linamaanisaha leaded petrol, na ilikuwa ina rangi nyekundu, unleaded ilikuwa in rangi ya kijani, sijajua Kama neno super bado linamaanisha leaded petrol kwa sasa ama labda linamaanisha kitu kingine.

Sent
 
Asante kwa maelezo yaliyoshiba,vipi sasa kuhusu Yale magari ambayo mdau kaeleza hapo juu (yenye valve mbili) kwamba bila Lead yanaweza kunock? Hawa wanafanyaje kama lead imepigwa marufuku?

Sent using Jamii Forums mobile app
Magari ya valve mbili ni zamani sana asee , unazungumzia Landrover 109 huko, Ni Kama standard kwa sasa gari za petrol kutumia valve nne.

Niliweka hapa Kama reference tu Ila kiuhalisia magari hayo hayapo mengi barabarani
Sent
 
Nashukuru mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngoja nipitie comment ya mdau afu nitarejea. Ila kwa ufupi ni kwamba. Yawezekana magari hayo ni yale ya teknolojia ya zamani sana. Ila kwa sasa hakuna kampuni ambayo inazalisha mafuta yenye kiambato cha risasi (Lead).
Ok,nashukuru nimeelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu gari za kisasa nyingi kwenye manual yake zinasema utumie unleaded...baadhi ndio unaweza tumia leaded ukitaka ila at your own risk. Ni vema kuithamini gari kutokana na specs ulizopewa.


Sent using Jamii Forums mobile app
Mafuta yaliyochanganywa na lead kwasasa hayapo kabisa sokoni, baada ya lead kupigwa marufuku hapo kitambo. Ni vile tu jina la "unleaded" lilikua limezoeleka ndio maana kampuni nyingi hazikuliondoa na linaendelea kutumika, hivyo basi usiwe na mashaka kabisa petrol zote ni unleaded

Kuhusu namba za mafuta hizo zinaelezea mchanganyiko mpya ulioreplace lead, ntaelezea baadaye. Ila tu ni kwamba kila engine ina specific number ya mafuta hayo, nadhani ipo juu kwenye mfuniko wa tenki. Ukizingatia hiyo namba utaenjoy sana perfomance na efficiency ya injini yako, ila unapoignore haiharibu injini bali inashusha hivyo vitu na life span yake
 
Maelezo mazuri,hizo namna za mafuta zinapatikana kituo chochote cha mafuta?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tofauti ya petrol inatokana na tofauti ya octane rating, mchanganyiko uliotiwa ndani yake kuzuia knocking ya injini. Kuna octane rating maarufu mbili
1. 95 hii ndo huitwa pia "unleaded
2. 98 hii ndo huitwa pia "super" au "premium"
Ndo maana ukifika sheli utakuta pampu hii imeandikwa "unleaded" na ile imeandikwa "super" au "premium"

NANI ATUMIE SUPER NA NANI UNLEADED
Ni muhimu kujua pia kuwa bei ya petrol super ni juu kidogo kuliko unleaded. Kwahiyo kuna makundi yanatofautiana katika kutumia mafuta haya
1. SUPER/PREMIUM (OCTANE RATING 98)
Engine zote za petrol zinaweza kutumia petrol hii bila shida. Hata hivyo kutokana na bei yake kuwa juu kidogo (sio sana) hakuna sababu ya kupoteza pesa yako kama engine yako haiko reccomended kwa mafuta haya
Injini nyingi za D4 ( direct injection) zinashauriwa kitumia mafuta haya kuepusha matatizo ya uchafu unaotokana na mafuta yaliyo chini ya kiwango. Haya ndio mafuta ya kiwango cha juu
2.UNLEADED (OCTANE RATING 95)
Engine nyingine zisizokuwa reccomended kwa premium zitumie haya. Ni cheap kidogo

NB: kama unaishi maeneo yasiyo na premium wakati injini yako ni reccomended , tumia unleaded huku ukiongezea additive za kusafishia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maelezo yako yamejitosheleza,asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maelezo yako yamejitosheleza,asante

Sent using Jamii Forums mobile app
Jamani nataka niseme jambo moja, juzi nmeweka mafuta mbagala pale waliandika SUPER nikasema hii super si ndo wanasem mazur (nikajisemea komoyo moyo), baada ya kuweka nikaenda nilipoenda nikapaki ilikuwa sio mabli ni kama nusu KM tu, nikapaki, nikaja kuiwasha kesho yake nikaanza safari, ila niliona gari ikiwa tofaut sana, cha kwanza ikawa nzito kuliko nilivyozoea, unakuta gari ipo speed 60 au 70 ila rpm haishuki kwenye 3 (3000) baada ya muda kidogo ikawaka taa ya check injini, nikatmbea hivyo hvyo mpaka nika fika safar yangu huku nikiwa najiuliza ni nini kilichorokea, baadae nikawa naenda sehem tena nikaenda puma kuongeza wese, kiukwel baada ya hapo gari ikarud kwenye hali yake kabisa ikawa nyepesi hta iwa speed 100 rpm inashuka mpka 1800 au 2000, ndo nikapata jibu kuwa ishu ilikuwa yale mafuta niliyoweka mbagala. Na taa ya injini chek haikuwaka tena

Hvyo nataka kusema kuwa sio kila wanaoandika SUPER wanamaanisha wengine wanajiandikia tu, tuweke mafuta kwenye kampuni zinazojulikana kwa kweli, maana ile shel walioniwekea mafuta machafu haina hata miezi 6 tangu ifunguliwe na mafuta yao wanauza bei rahic kuliko wengine 1780 kwa lita, kumbe siri wanaijua wenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole,huenda yalichakachuliwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…