Tofauti ya petrol inatokana na tofauti ya octane rating, mchanganyiko uliotiwa ndani yake kuzuia knocking ya injini. Kuna octane rating maarufu mbili
1. 95 hii ndo huitwa pia "unleaded
2. 98 hii ndo huitwa pia "super" au "premium"
Ndo maana ukifika sheli utakuta pampu hii imeandikwa "unleaded" na ile imeandikwa "super" au "premium"
NANI ATUMIE SUPER NA NANI UNLEADED
Ni muhimu kujua pia kuwa bei ya petrol super ni juu kidogo kuliko unleaded. Kwahiyo kuna makundi yanatofautiana katika kutumia mafuta haya
1. SUPER/PREMIUM (OCTANE RATING 98)
Engine zote za petrol zinaweza kutumia petrol hii bila shida. Hata hivyo kutokana na bei yake kuwa juu kidogo (sio sana) hakuna sababu ya kupoteza pesa yako kama engine yako haiko reccomended kwa mafuta haya
Injini nyingi za D4 ( direct injection) zinashauriwa kitumia mafuta haya kuepusha matatizo ya uchafu unaotokana na mafuta yaliyo chini ya kiwango. Haya ndio mafuta ya kiwango cha juu
2.UNLEADED (OCTANE RATING 95)
Engine nyingine zisizokuwa reccomended kwa premium zitumie haya. Ni cheap kidogo
NB: kama unaishi maeneo yasiyo na premium wakati injini yako ni reccomended , tumia unleaded huku ukiongezea additive za kusafishia
Sent using
Jamii Forums mobile app