Nini Tofauti ya Leaded na Unleaded Petrol?

Unaanzaje kuzingatia namba ya petrol kama za oil?? maana petrol inakuishia popote safarini unaangalia kituo kilichokaribbu nawe
 
Tatizo ni uaminifu tu
 
Kuna chimbo lita 1750 mzinga pale wapo vizuri hayazingui kabisa bei mtere
Jamani nataka niseme jambo moja, juzi nmeweka mafuta mbagala pale waliandika SUPER nikasema hii super si ndo wanasem mazur (nikajisemea komoyo moyo), baada ya kuweka nikaenda nilipoenda nikapaki ilikuwa sio mabli ni kama nusu KM tu...
 
Kwa Tanzania tofauti kati ya unleaded, petrol au super ni majina tu ila mafuta ni yale yale, ukiona wameandika super sio kwamba ndo mazuri ila wameandika ili kuvutia wateja tu. Petrol station zote wananunua mafuta sehemu moja na bei ya kuuza wanapangiwa ila wengine wanaamua kuyaita unleaded wengine super au petrol ila hakuna tofauti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna baadhi ya kampuni ni waaminifu
Kuhusu mafuta kuja kwa bulky ni kweli, lakini baada ya hapo kila kampuni inatia vichanganyishi vyake tofauti, ndio maana unaona rangi za mafuta zinatofautiana kwa makampuni,
 
Kuna baadhi ya kampuni ni waaminifu
Kuhusu mafuta kuja kwa bulky ni kweli, lakini baada ya hapo kila kampuni inatia vichanganyishi vyake tofauti, ndio maana unaona rangi za mafuta zinatofautiana kwa makampuni,
Ile rangi inayowekwa kwenye petrol haina kichanganyishi chochote ni rangi tu wanaweka ili kutofautisha petrol na diesel au mafuta ya taa. Tena rangi yenyewe wanaweka kidogo sana vijiko viwili vya chai unaweza kuweka kwenye tank la lita 31,000 na rangi ikabadilika.. kusema kuna kampuni flani ndo wana mafuta mazuri kuliko wengine hilo sio kweli labda useme kuna baadhi ya sheli wana matank machafu ndo maana mafuta yao yanaonekana hayana ubora

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi hii excelium inasafisha / kuimarisha kweli engine kilometer baada ya kilometer kama wanavyodai wenyewe hawa Total?
 
Kibongobongo tunataka wese la Bei rahisi hayo mengineyo mnajua nyie wasomi
 

Una ushahidi wa hili? Umeshatumia mafuta ya sheli za Puma mara ngapi?
 
Vipi kuhusu takwimu zinazotolewa na serikali zikionesha kampuni fulani ina mafuta bora kuliko nyingine.
 
Vipi kuhusu takwimu zinazotolewa na serikali zikionesha kampuni fulani ina mafuta bora kuliko nyingine.

Msamehe bure, mara tank chafu mara hivi, ye ajue tu sio kila petrol station ni ya kununua mafuta.Kwa wamiliki wa magari mazuri na wanaopenda magari yao wanajua ila kama mtu anaendesha guta anaweka mafuta tu popote! Kuna gari ambazo ukiweka mafuta ya hovyo hata kuwaka haiondoki!
 
Watu wengi wanasema Puma,Total na Engen ndiyo wana mafuta yenye ubora...
Hili limekaaje...?

Nilinunua mafuta Puma kwwnye dumu ni mekundu,
Kuna siku nikanunua Engen kwwnye dumu ni meupe yanakaribua maji..

Ila kwa upande wangu binafsi, kuna kituo kimoja cha mafuta knaitwa Njake, kipo maenwo ya mianzini Arusha, nikuweka mafuta yao huwa nasikia gari yepesi sana...linachanganya vizuri sana.
 

Kweli mkuu....hili jambo la mafuta ni la kuzingatia mno,Leo asbhi nimeweka mafuta kwenye hizi petro station uchwara baada ya KM kadhaa tu gari inawasha taa ya check engine then kwenda kwa fundi kuifanyia diagnosis tatizo likaonekan ni mafuta niliyoweka
 
Ina maana huwa hawakaguliwi au wanachakachua wakifikisha kituo cha mafuta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…