Nini Tofauti ya Leaded na Unleaded Petrol?

Ina maana huwa hawakaguliwi au wanachakachua wakifikisha kituo cha mafuta
Me naona huko mafuta yanapochukuliwa yanakuwa yana hali moja..(ubora)

Nahisi wakishafika vituoni ndiyo kila mtu anaongeza mambo anayoyajua yeye...

Yaani bongo taabu sana
 

Hilo gari labda uliweka mafuta ya taa badala petrol ndo likakataa kuondoka.. Kuna watu wanaweka mafuta ya zaidi ya sh million moja kwa trip na wanaweka sheli yoyote tu wanacho angalia ni bei na huwezi kusikia semi trailer imekataa kuondoka kisa wameweka mafuta shel flani. Kwa bongo mafuta ni yale yale tu. Total, oilcom, puma na hizi shel ndogo za mtaani zote wananunua mafuta sehem moja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna sheli zinafungiwa kwa kuchakachua mafuta hujawa lisikia hili pia... usifananishe total puma na vitu vya ajabu ajabu...
 

Sasa weka mafuta shell yoyote ukiwa na engine za bmw au D4 petrol kama hatujasikia manalalamikia hizo gari mbovu
 
Nilishawahi nunua diesel Kigoma.

Kufika kaliua engine ikafa.

Mafundi wakatoka Mwanza. Wakaja kukagua wakakuta Fuel Pump imekufa. Diesel imechakachuliwa.
 
Shel zinafungiwa kwa kubana pump sio kuchakachua mafuta. Hivi unafkiri kuchakachua petrol ni easy kama maziwa unaweza kutia maji tu???

Sent using Jamii Forums mobile app
wanachakachua mzee bongo vyote vinawezekana na ndio maana PUMA TOTAL zinaheshimika kwa ubora wao na nidhamu miaka nenda rudi ingekua mafuta yote ni sawa nao wangekua wakawaida tu kama hizo Kayumba oilcom. Kila kitu kina grade mkuu pia usifananishe injini ya scania na hizi gari ndogo.
 

Ok puma au total kuwa bora ni mtazamo wako tu mimi naongelea uhalisia. Mafuta ya total na kayumba oilcom ni yale yale hakuna kinachoongezwa wala kupunguzwa yote wanatoka sehem moja. Usifkiri kisa total ni kampuni ya wazungu ukadhani mafuta yao wanatoa ulaya. Total unazoona bongo zinaendeshwa na waarabu na waswahili hao hao wanaomiliki shel za kayumba wanatumia tu brand ya total.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kama ni yaleyale mbona bei tofaut? Provided kwa vituo vya hapa dar nikimaanisha sio mbali na depot hivyo transportation fee haipo
 
I'm sorry to say this,wewe ni bogus sana tena kiazi
 
Sasa kama ni yaleyale mbona bei tofaut? Provided kwa vituo vya hapa dar nikimaanisha sio mbali na depot hivyo transportation fee haipo
Bei tofauti iko wapi wakati bei za kuuza wanapangiwa na ewura? Kama total mafuta yao ni tofauti na sheli zingine wajaribu kuuza bei juu zaidi ya iliopangwa na ewura.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwann total africana bei ni tofaut na camel oil ambayo ipo hapohapo upande wa pili wa barabara? Nijib swal we k
Tofauti ya bei ni ushindani wa biashara sio ubora wa mafuta. Mafuta yote yanaagizwa kwa pamoja na yanauzwa bei moja kwasababu mafuta yote ni yale yale hakuna tofauti . Baadhi ya sheli zinashusha bei ili kuvutia wateja. Jibu ndo hilo

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Unachoongea hukijui wewe....juzi tu hapa gari iliniwakia taa ya check engine kuipeleka kuifanyia diagnosis tatizo likaonekan ni mafuta niliyoweka asbhi maan hilo tatizo lilikuja kutokea mchana acha kudangany watu
 

Chief wewe una akili na uelewa ila sio applicable kwenye context. Uwe unaelewa achaga kulipuka tu! Issue ni specs za gari versus aina ya mafuta! Sio habari ya mafuta ya bei gani! Mimi namiliki gari amabalo specs zake ni ulipe unleaded tu!

Ukijiwekea mambo mengine unaharibu.Unaongea nini? Nyie ndio mnaofanya watoto waone elimu haina faida wacha ubishi! Kama la kwako linatumia kila aina ya mafuta well and good ila usibishe ..inawezekana hata user manual ya gari husomagi. hapa tunasaidia kila mtu apate uelewa wewe unaleta hearsay zako!

Issue sio kuweka kila sheli, wanatumia gari ya aina gani? Utafananisha gari za europe ambazo ni sophiscated say na Kirikuu au Carina TI ? Ingawa hata hizo za japan zinahitaji adabu ya mafuta.

Unaposema petrol station zote zinapokea mafuta ya aina moja maana yako ni ipi? Unajua kua mafuta yanapofika kila kampuni inafanya uchambuzi na kupata product mbalimbali bila kuathiri ubora au kuvunja sheria? Dhana ya unleaded vs super unaielewa au unadhani yote ni kuweka tu? Ukijibu hizo facts tutakua tumesaidia wengi badala ya generalization as if hujui kinachoendelea!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…