Elections 2010 Nini Tofauti ya Mramba, Chenge NA Mwakalebela?

Elections 2010 Nini Tofauti ya Mramba, Chenge NA Mwakalebela?

Wadau napata shida sana kuelewa ni nani anayestahili kuachwa ktk kikao cha CCM kilichotoa maamuzi ya mwisho juu ya nani apitishwe na nani aachwe, report ya SFO toka kule uingereza juu ya sakata la Radar inamtaja wazi Mgombea ubunge wa jimbo la Bariadi magharibi Endrew John Chenge ni yupi si mwadilifu kati yake na Mwakalebella? nisaidieni wadau wa Sheria
 
nimeshangazwa na hatua ya nec ya ccm kumtosa bwna mwakalebelea kuteuliwa kugombea ubunge iringa mjini kwa tiketi ya ccm ingawa alishinda kura za maoni, kama ishu ni kesi, mbona kibao wana kesi mahakamani lakini wamepitishwa, kwa mfano mramba, chenge nk
ina maana kama nagombea mtu akikurupuka tu na kunifungulia kesi basi ndio iwe sababu ya kumuacha mtu? kuna lack of consistence ktk hili cjui hapa imekaaje!
 
Kimsingi NEC imemsomea dua tu ili kuhitimisha kile ambacho kamati ya siasa ya mkoa imeelekeza kifanywe dhidi yake, inaelekea bwana Mwakalebela alijiingiza kichwakichwa kwenye viwanja hivyo,hata hivyo asikate tamaa hizo ndiyo siasa za Africa zina udhiiiii!!:frusty:
 
mi pia nilishangaa sana wakati chiligati anatangaza hayo. nilijiuliza swali hilihilo. whats wrong with ccm?
 
swali je endapo Mramba atachaguliwa alafu akapatikana na hatia kabla hajamaliza kipindi chake cha ubunge je hawaoni kurudia uchaguzi itatugharimu pesa nyingi na huku tunararamika hatuna hela kwanini wasisubiri maamuzi ya mahakama wameliaangalia hili
 
Nini tofauti ya hawa watu wawili katika medani sa siasa za CCM?
Kwanini jina la Pesambili lirudi ili hali yuko mahakami tayari kwa tuhuma vile vile?
Hivi tunaongozwa na CCM ya Vichaaaaa??

33nhx69.jpg

Fredrick Lameck Mwakalebela

2hoh8ra.jpg

Basil Pesambili Mramba

Mwakalebela sio mwenzetu.
 
mweee mwakalebela, mafweza uliyoiba TFF ungewekeza sehemu za maana sasa ona mdogo wangu umegawa mahela karibu yote na kuambulia aibu. wewe ni mwizi na unajijua CCM wana taarifa zako zote siyo za rushwa tuu.
 
swali je endapo Mramba atachaguliwa alafu akapatikana na hatia kabla hajamaliza kipindi chake cha ubunge je hawaoni kurudia uchaguzi itatugharimu pesa nyingi na huku tunararamika hatuna hela kwanini wasisubiri maamuzi ya mahakama wameliaangalia hili

Maana yake ni kuwa tayari hukumu na mchakato wote wa kesi umeapangwa.
 
Mbona wengi tu wana tuhuma lakini wamepitishwa; Kikwete anausongo na majina ya watu wa Mbeya nini?

Si uliona hata Riz moja alivyomfurusha Kifu asishike sukani pale jangwani!! Tofauti ipo kubwa sana tu pesa 2 mtandao wake mkubwa,ukimbania tifu lake ni kubwa,Mwaka bado kifaranga na hana madhara na alipambana na kigogo ambacho hata Super BULA alikimbia!
 
Mbona wengi tu wana tuhuma lakini wamepitishwa; Blandes anakesi ya rushwa mahakamani lakini nae kapitishwa!! Kikwete anausongo na majina ya watu wa Mbeya nini?

Kiboko kabisa ni ie ya LOWASA aliyepigiwa kura 40,000 wakati wamasai wote wenye umri wa kupiga kura ukijumlisha monduli awafiki 40,000 imekuwa kama ile ya znz na cuf enzi zile!
 
Sawa wote hawa siwanashitakiwa na kesi zao ziko mahakamani inakuwaje mmoja anatolewa
alafu mwingine anaachwa au monica mtandao?

Kile kibwagizo "BINADAMU WOTE NI SAWA NA AFRIKA NI MOJA" inaelekea kilikudanganya. Ukweli upo kwenye physical processes za kibadamu lakini ki-utashi na influence tuko tofauti. Kumlinganisha Mwakalebela na Chenge sio sahihi. Kumbuka Chenge yupo kwenye kamati ya Maadili, na ndio mwanasheria aliyebobea katika kamati hiyo. Mengineyo kuhusu Chenge yalishasemwa.

Sometimes ago nilishangaa kuona mambo ya kawaida ambayo msemaji wa TFF Ndg. Kaijage alipaswa kuyaongea, utakuta Mwakalebela ndio anayazungumzia. Kumbe ilikuwa janja ya nyani!


Mwanasiasa akiangukia pua ni stahiki yake..........!
 
Huyo mmoja tuhuma zake zipo kwenye kupata hicho cheo ila huyo mwingine anatuhuma kwenye kitu kisicho na uhusiano na anachogombea.

Mbona Ndolanga na Rage walishawahi kushinda kura za maoni na kutoswa (kama sikosei mwaka 2000) japo kesi yao mahakamani haikuwa inahusiana na uchaguzi?
 
mwakalebela na mramba kuwalinganisha ni sawa na kulinganisha tembo na sungura...katika mafisadi wa nchi hii mwakalebela hayupo kabisaaa ni masikini mwenzetu tu huyu labda ana hela ya kubadilishia mboga tu hata kama aliiba TFF wizi wake hauna adhali kwa watanzania lakini wizi wa mramba ndo unaosababisha aki mama wajawazito wanakufa na vichanga vyao hospitalini....wananchi wa iringa hawamtaki monica mbega sema monica na kikwete ni damu damu walikuwa wote wizara ya fedha so wanafahamiana hawa toka zamani....lakini kweli takukuru toka waanze uchunguzi so far ni mwakalebela na mungai tu ndo wamefikishwa mahakamani...which is not true
 
Hawa wote dugu moja. Hawa wote hawastahili kuwepo madarakani period. Chenge na Mramba mimi nashangaa ni
watu gani wasio na haya including Lowassa sijui Karamagi, Rostam hivi sio vyema kwenu mkajiengua na kuliongoza
au kulitawala taifa hili mkakumbukwa kwa mema machache mliyofanya mpaka watu wafike mahali waseme sasa basi
halafu mpate aibu ambayo haitafutika kizazi hata kizazi. Achieni madaraka achane tamaa mmeshajineemesha vya kutosha
Haya machozi ya watanzania mkae mkijua hayataenda bure kuna malipo mbele ya safari kwa namna moja au nyingine.
Isife siku mkasema hamkushauriwa. Yetu macho TIME WILL TELL!!
 
Back
Top Bottom