'Operation' ni Msako. Unaweza kuwa ni kutafuta,kujua,kukamata na kutokomeza au kuangamiza jambo lililokusudiwa na hao wanaolitekeleza.
'Mission' ni jukumu maalumu la kimkakati ambalo linatakiwa kufanyika ndani ya muda maalumu na kuisha kwa muda maalumu kwa weledi na ukamilifu usiotia shaka.Kwamba jambo hilo ni lazima lifanyike na kufanikiwa kwa muda uliopangwa.
Mfano.Nipo Arusha.Ninatakiwa kwenda Tanga kutafuta mtu aliyeniibia pesa zangu. Hapa ninaanza kupanga mkakati (mission).
Halafu, ninatakiwa kujua atakuwa wapi, na nani,na ni mtu wa namna gani,atakuwa na nini, je ana silaha? (Bado ni mission).
Sasa nikishajiridhisha na taarifa hizi na kisha nikaamua kumfuata huko huko aliko na kumtia nguvuni. Hapo ninakuwa nimefanya msako wa kumpata mwizi wangu(Operation).
Halafu nikisharudi mtu aniulize, vipi ulikuwa wapi siku hizi mbili tatu,hujaonekana mtaani!?
Namjibu, ahaa! Nilikuwa na kazi moja hivi muhimu sana,ndio maana nilikuwa sionekani, basi namalizia hivyo.(mission). Mara nyingi 'mission' huwa ni mpango mkakati wa siri,halafu matokeo yake hutokea baada ya kukamilisha kazi,nayo inaweza isiwekwe wazi sana. Halafu watu wanasema, tumefanikiwa. Kama hukuwa nao unaweza usijue, labda waamue kukwambia.
Ndivyo nijuavyo!