Nini tofauti ya OPERATION na MISSION katika Intelijensia?

Nini tofauti ya OPERATION na MISSION katika Intelijensia?

hata mimi

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2017
Posts
1,356
Reaction score
1,442
Haya maneno yana maana mbali mbali kutegemea na muktadha wa matumizi. Sasa tuache maana zingine zote hebu naomba ufafanuzi wa haya maneno kwenye shughuli za kiusalama (jeshi la polisi, jeshi la magereza, jwtz, tiss, nk)

Mfano utasikia
1.Wamekamatwa vibaka na wazururaji kwenye operation maalumu

2.Amekamilisha mission maalumu ya kuwafuatilia wenye vyeti feki... wametumbuliwa wote!
 
Kwenye operation ni mchakato wakuchunguza na kukomesha japo haina utokemezaji wa mojakwamoja kama ni msako watakaojilengesha ndio watakamatwa au kudhibitiwa ila wengine watasalia
Mission ni lengo na hatua ya moja kwa moja mlengwa huwa anafahamika na kazi ni moja tuu kukomesha na kudhibiti moja kwa moja japo yote yawezakutumika katika mbinu za kijeshi kwa kikosi kimoja au zaidi
 
Haya maneno yana maana mbali mbali kutegemea na muktadha wa matumizi. Sasa tuache maana zingine zote hebu naomba ufafanuzi wa haya maneno kwenye shughuli za kiusalama (jeshi la polisi, jeshi la magereza, jwtz, tiss, nk)

Mfano utasikia
1.Wamekamatwa vibaka na wazururaji kwenye operation maalumu

2.Amekamilisha mission maalumu ya kuwafuatilia wenye vyeti feki... wametumbuliwa wote!
Mission ni neno pana zaidi ambapo operation inaweza kuwa ndani ya mission. Mfano Our Mission is to eliminate drugs hence we have to run a critical operation for it.
 
Mfano utasikia
1.Wamekamatwa vibaka na wazururaji kwenye operation maalumu

2.Amekamilisha mission maalumu ya kuwafuatilia wenye vyeti feki... wametumbuliwa wote!
chunguza TENSES zilizotumika hapo: Operation huhusisah watu/makundi/ majeshi mengi, mfano: operation barras.
Mission ni singular- huhusisha watu/ mtu ama timu moja: mfano-geranimo ekia
 
Haya maneno yana maana mbali mbali kutegemea na muktadha wa matumizi. Sasa tuache maana zingine zote hebu naomba ufafanuzi wa haya maneno kwenye shughuli za kiusalama (jeshi la polisi, jeshi la magereza, jwtz, tiss, nk)

Mfano utasikia
1.Wamekamatwa vibaka na wazururaji kwenye operation maalumu

2.Amekamilisha mission maalumu ya kuwafuatilia wenye vyeti feki... wametumbuliwa wote!
Operation ni "zoezi" na mission ni "lengo".
1. Kwenye operation dhidi ya wawindaji haramu: yaani zoezi la kutafuta wawindaji haramau
2. Kukamilisha mission ya kuwakamata wawindaji haramau: Kukamilisha lengo la kuwakamata waindaji haramu.
 
Operation kikawaida tu ni general terms ya kazi maalumu kufanikisha Jambo fulani la ...mfano operation tokomeza malaria mashuleni,, mission kutoa elimu juu kujikinga na Malaria sijui kugawa chandarua inaweza kuwa kupilizia sawa nk
 
Mm niavyojua operation nikutekeliza/kufanya jambo kwa mda mfupi linaweza kufanyika kwa siri ama kwa uwazi mission ni kutekeleza/ kufanya jambo kwa mda mrefu linaweza likatekelezwa kwa siri ama wazi

Lakini yote kukamikisha/kufikia malengo flani
 
'Operation' ni Msako. Unaweza kuwa ni kutafuta,kujua,kukamata na kutokomeza au kuangamiza jambo lililokusudiwa na hao wanaolitekeleza.

'Mission' ni jukumu maalumu la kimkakati ambalo linatakiwa kufanyika ndani ya muda maalumu na kuisha kwa muda maalumu kwa weledi na ukamilifu usiotia shaka.Kwamba jambo hilo ni lazima lifanyike na kufanikiwa kwa muda uliopangwa.

Mfano.Nipo Arusha.Ninatakiwa kwenda Tanga kutafuta mtu aliyeniibia pesa zangu. Hapa ninaanza kupanga mkakati (mission).

Halafu, ninatakiwa kujua atakuwa wapi, na nani,na ni mtu wa namna gani,atakuwa na nini, je ana silaha? (Bado ni mission).

Sasa nikishajiridhisha na taarifa hizi na kisha nikaamua kumfuata huko huko aliko na kumtia nguvuni. Hapo ninakuwa nimefanya msako wa kumpata mwizi wangu(Operation).

Halafu nikisharudi mtu aniulize, vipi ulikuwa wapi siku hizi mbili tatu,hujaonekana mtaani!?

Namjibu, ahaa! Nilikuwa na kazi moja hivi muhimu sana,ndio maana nilikuwa sionekani, basi namalizia hivyo.(mission). Mara nyingi 'mission' huwa ni mpango mkakati wa siri,halafu matokeo yake hutokea baada ya kukamilisha kazi,nayo inaweza isiwekwe wazi sana. Halafu watu wanasema, tumefanikiwa. Kama hukuwa nao unaweza usijue, labda waamue kukwambia.

Ndivyo nijuavyo!
 
Haya maneno yana maana mbali mbali kutegemea na muktadha wa matumizi. Sasa tuache maana zingine zote hebu naomba ufafanuzi wa haya maneno kwenye shughuli za kiusalama (jeshi la polisi, jeshi la magereza, jwtz, tiss, nk)

Mfano utasikia
1.Wamekamatwa vibaka na wazururaji kwenye operation maalumu

2.Amekamilisha mission maalumu ya kuwafuatilia wenye vyeti feki... wametumbuliwa wote!
Opeartion huwa ni mpango mkakati wa dharura na ambao ni siri; ya wale wanaohusika na kuifanya operation hiyo wakati mission ni mpango mkakati ulio wazi no usio wa siri na unaweza ukawa ni wa dharura au si wa dharura
 
Operation Ni ukusanyaji wa taarifa, Uchambuzi wa nguvu za adui, kuzisanbaza na mwisho kuweka wazi possible threats mnazoweza kumbana nazo.

Baada ya kukusanya, kuzipima na kuzisambaza taarifa sasa ndio Makamanda wanakuja na mipango, Mikakati dhidi ya adui.

Operation ndio ina mzaa Mission.
Operation picha kubwa Mission vipande vinavyounda picha ( eer day tasks ) baada ya upembuzi wa kina.
 
Operesheni ni ile kwa mfano mtu ana jipu mguuni unampasua kuliondoa jipu.

Mission ni maeneo ya taasisi za kidini na hasa hasa Roman huwa wana mission zao.

Asante.
 
Back
Top Bottom