Nini Tofauti ya Sentensi hizi Mbili?

Nini Tofauti ya Sentensi hizi Mbili?

8691jakigili

Senior Member
Joined
Mar 30, 2012
Posts
179
Reaction score
67
(1) Mimi nimepita chuoni, au (2) Chuo kimenipitia mimi!

Tafakari na ujibu ukilinganisha na wasomi wetu (kwa idadi kubwa) hapa Tanzania. Kuelimika ni kubadilisha tabia na mwenendo huku ukidhihirisha tabia na mwenendo huo katika jamii unayoishi. Hivi msomi hapa bongo ni kuwa na vyeti vya daraja "A" la ufaulu au ni msomi mwenyewe kuwa ni cheti cha elimu katika jamii husika? Kama idadi ya wasomi imeongezeka tangu tupate uhuru wa nchi, lakini maadui wa Taifa letu hatujaweza kuwatokomeza; na kibaya zaidi adui mwingine ameongezeka, yaani ufisadi (akijumuishwa katika watatu ujinga, umaskini na maradhi). Wasomi na elimu ya Tanzania inatatua nini?
 
Kwa hiyo unataka utofauti gani kama unaanzisha post unaijadili wewe mwenyewe na kujipa majibu mwenyewe?
 
Maswali tashtiti (rhetorical questions) yanahitaji pia mjadala mkuu!!
 
(1) Mimi nimepita chuoni, au (2) Chuo kimenipitia mimi!

Tafakari na ujibu ukilinganisha na wasomi wetu (kwa idadi kubwa) hapa Tanzania. Kuelimika ni kubadilisha tabia na mwenendo huku ukidhihirisha tabia na mwenendo huo katika jamii unayoishi. Hivi msomi hapa bongo ni kuwa na vyeti vya daraja "A" la ufaulu au ni msomi mwenyewe kuwa ni cheti cha elimu katika jamii husika? Kama idadi ya wasomi imeongezeka tangu tupate uhuru wa nchi, lakini maadui wa Taifa letu hatujaweza kuwatokomeza; na kibaya zaidi adui mwingine ameongezeka, yaani ufisadi (akijumuishwa katika watatu ujinga, umaskini na maradhi). Wasomi na elimu ya Tanzania inatatua nini?

Mkuu ulishawahi kupata "A" kwenye masomo yako?
 
Halafu badilisha hii sentesi kwa kingereza kama kweli wewe chuo hakijakupitia..! "Baba mimi ni mtoto wako wa ngapi?"
 
Sidhani kama wewe 8691jakigili ni msomi ulieye elimika vya kutosha. Uwezo wa mtu haupimwi na viji swali kama vyako. Kama unataka kujua wasomi wa Tanzania elimu zao zimewasaidiaje na pia wamesaidia vipi nchi yao na si vyeti tu, andaa Proposal nzuri na ujiandae kufanya research.

Usikurupuke ku-post thread za kijinga kama hizi kwa ku-challenge wasomi wa Tanzania wakati wewe mwenyewe unaweza ukawa kilaza.

Rudi ukajipange upya, andaa Title yako nzuri ya research, andaa hypothesis iliyotulia, jenga hoja vizuir, na pia njoo na research questions, piga kazi na utapata majibu, kama hizo 'A' wanazopata watu zinalisaidia Taifa au vipi. Japo naona unajifanya kuwa na reasoning, lakini bado sana wewe ni mchanga kwa jinsi ambavyo andiko lako lilivyo.

Usiwe na wasiwasi kuhusu ufadhili, wapo kibao, wewe njoo na proposal na tutakusaidia, (nitafute: manyiri.manyi@gmail.com).

Nakusihi, kama wewe ni msomi kweli, na unataka kuwa-challenge wasomi wa Taifa hili, approach yako unayotumia ni ya kitoto sana!

Be blessed!
 
umepost sentesi hizo mbili na unataka tofauti ambazo tayar wew unazo kulingana na maono yako, lasivyo post hoja yako kama mjadala ili uweze pata maoni ya wanajamvi juu ya uhalali wa wasomi wa sasa.
 
Mfano nitakaoutoa hapa chini unaonekana ni wa kijinga na kukosa mantiki:

Ninamtafuta dereva wa kuendesha gari langu, wawili wamejitokeza. Wa kwanza, anajua kuendesha gari vizuri sana, lakini alifeli mtihani darasani kozi ya udereva (cheti chake kina maksi za chini kabisa). Wa pili, alifaulu mtihani "A" darasani, lakini hajui kuendesha gari.

Kama mfumo wa elimu tulionao hautatui matatizo tuliyo nayo kama taifa, nini faida na hatima yake? Sipingi dhana ya kufaulu darasani na kuwa na maksi nzuri A's. Hoja yangu ya msingi ni kwamba tuweze kufaulu vizuri darasani, vile vile tuoneshe elimu hiyo kwa vitendo!! Mfano: Wasomi wa kilimo wasaidie kutokomeza njaa nchini!
 
(1) Mimi nimepita chuoni, au (2) Chuo kimenipitia mimi.

Kwa faida ya wasomaji wa JF nitafafanua kidogo tofauti ya sentensi hizo mbili:
1. Mimi nimepita chuoni.
W + T + E (kiwakilishi, kitenzi na kielezi)

2. Chuo kimenipitia mimi
N + T + W (nomino, kitenzi na kiwakilishi)

Ukizichambua, hizo ni sentensi mbili tofauti zenye maana mbili tofauti ambazo hazina ulinganifu kabisa. Hata kiwakilishi, mimi, kinabeba maana tofauti ya kimuktadha. Katika sentensi ya kwanza, mimi ipo kwenye kiima ilhali katika ile ya pili, mimi ipo katika kiarifu.

Maelezo mengune aliyoweka mtoa mada ni ----- na vumbi la macho ( hayana maana).
 
Back
Top Bottom