1. SSD ni nini, faida yake ni nini na kazi yake ni nini?
SSD ni storage device (kifaa cha kuhifazi data au taarifa kwa maana ya processed data), SSD in long term ni Solid State Disk.
SSD imekuja miaka ya hivi karibuni na kuwa mbadala wa HDD ambayo yenyewe in long term huitwa Hard Drive Disk, kwanini haya majina ya solid state na hard drive ni kwasababu SSD haina any moveable part ndani yake while HDD has, kitu kama disk plate with spindle for writing and reading of data.
Faida ya SSD
-Kwa kuwa SSD haina any moveable part ndani yake hivyo imekuwa smooth katika ku write and ku read data hence makes it very smooth in running ndio maana PC yenyewe SSD huwa ni very smooth.
2. Cloud storage ni nini, faida yake ni nini na kazi yake ni nini?
Cloud storage ni mfumo wa kidigitali/kisasa wa uhifadhi wa data na taarifa katika mtandao ambapo hatuhitaji kifaa hifadhi tuwenacho physically (physically means tangible, touchable ). Kwa maana hiyo third party ndio ana miliki server yenye storage device ya kuhifadhi data na yeye anakupa access ya kuaccess hizo data zako.
Let say Kampuni A ana miliki cloud storage server yenye storage device and then anatoa service ya uhifadhi data then wewe atakupa access through network that is internet kuhifadhi data zako huko kwenye server yake aidha bure au kwa kukulipisha chochote kitu.
Faida ya cloud storage
-unaweza kuaccess data zako on the go, popote uendapo ilimradi tu una parameters na credentials za kuweza kufikia server ya third party wako kulingana na makubaliano yenu, mostly you will need an internet, credentials to access the servers, and maybe a fee that can be paid monthly or annually depends na makubaliano yenu.
3.Virtual storage ni nini, faida yake ni nini na kazi yake ni nini?
Virtual storage, as a term virtual means not tangible, but in IT virtual storage maanake ni mkusanyiko wa physical storage devices (storage device nyingi kama SSD, HHD n.k) na kuanganishwa au kufanywa zionekane na kusoma katika mahali pamoja ambapo kitaalam tunaita SAN(Storage area network) nikama vile unafanya networking ambayo can be WAN, LAN, MAN. hizi storage ili ziwe SAN inabidi sasa ziwe na aidha RJ45 port, wireless, USB port (through shared) then inafanyika sharing mostly tunatumia server enabled - powered operating system.
Faida ya virtual storage
-Unaweza kuaccess data nyingi na zilizo sehemu tofauti tofauti kwa mara moja na within a minute.
Kwa kuongezea, cloud storage inaweza kuunganishwa katika virtual storage.
NB.
Zote kazi yake ni moja tu ambayo ni kuhifadhi data kwa kuwa zote ni storage tofauti ni mahali zilipo na utendaji wa kazi.
Asante.