.....unategemea nini Jiji bado wanatumia sewage system aliyojenga mkoloni 1950s kwa population ya watu laki mbili?
Sawa kabisa mkuu Koba, tuna Mstahiki Meya,Mkurugenzi wa Jiji(watatu?),Mkuu wa Mkoa, Mwaziri wote wako Dar, Wahandisi watendaji wazito wote wako Dar.
Lakini hao wote ni kama wametoka Kijijini jana na hamna mwenye imagination ya namna ya kutatua matatizo ya a sustainable city.
Kutwa watendaji hawa ni kwenye kongamano,warsha,semina na mikutano holela.
Kuna jamaa Mkenya kacomment (katika JF)kuwa Jiji la DSM ni chafu sana duniani, la 40 kutoka chini.
Mameya wanashindana kujilimbikia mali kwa uuzaji wa viwanja hata kwenye njia za maji.
Pale bonde la Mpunga Msasani, kuna Meya wa halmashauri ya Kinonondoni ameuza eneo la mapito ya maji.Ikinyesha mvua kidogo tu ni mafuriko maana maji hayana pa kwenda(pale kati ya Shoppers na Mayfair).Kila mtu anogopa kumfunga paka kengele.Huyu jamaa vile vile,kwa kadri ya magazeti, ametuhimiwa kuwauzia Halmashauri kompyuta kwa bei ya kuruka.
Kwa mtindo huu Jiji la DSM daima litaendeshwa kiswahili mpaka apatikane Albert Mnali wa kuwanyoosha hawa watu wanaohusika.