Sahiba,
I am starting by telling you this,We can only move forward if we agree on what went wrong.Tumekwama tulipokwama kwa sababu hatujui tulikosea wapi hivyo tunaendeleza old failed politics.
Mkuu tulifahamu wapi tulikwama na hili sote tunafahamu kwamba ni mfumo wa siasa -UJAMAA..Hapa tupo sote iweje leo tushindwa baada ya kufahamu tuliharibu wapi bado sababu zijengwe around huo huo ujamaa..
Hoja yako haina tofauti kabisa na hoja ya wanasiasa ambao bado leo wanazungumzia Ukoloni au Utumwa wakati sio sisi tuliwekwa utumwani..
Nyerere kwa kuelewa athari za Ukoloni alijenga misingi inayopingana na Ukoloni ktk UTAWALA na ndio maana leo hii wewe upo HURU..lakini inashangaza watu kama nyie mnashindwa hata kunyoosha mikono yenu kumshukuru Mungu kuwa huru...
Awamu ya pili, ilianza kwa sura mpya kuondokana na Ujamaa na mkajenga mikakati inayolenga kuvunja misingi ya Ujamaa, hakuna mtu kati yetu aliyepinga.. Sasa tunapokosea utekelezaji wake tunarudi nyuma kutafuta mchawi.. basi tusiseme ni Nyerere nadhani tulikotoka ni kutawalkiwa na sijui lawama hasa zimfuate nani, Muingereza, Mjarumani Mreno au Mwarabu maanake hawa wote walitutawala wa nyakati tofauti..
Hivi visingizio ni vya mtu aliyechoka na maisha.. ni hulka ya Wadanganyika maanake hata ndugu zetu kutofanikiwa kwao huwalaumu wazazi kwa kutowapa elimu na wakiwa na elimu lakini mambo bado sii mazuri basi itakuwa kwa nini walizaliwa Tanzania..
Upuuzi mtupu.... Tumekosea wapi! tulikosea kuingia Ubepari kichwa kichwa kutupa miiko na maadili ya viongozi tukifikiria kwamba adui wetu mkubwa ni umaskini hivyo tuanze kujitajirisha sisi wenyewe...ndiyo hayo maazimio klama ya Zanzibar.. mbopna mwalimu maazimio yalipokuwa hayafanyi kazi tuliyavunja! iweje leo tunashindwa kuvunja Azimio ambalo linaturudisha utumwani!
Achana Mkapa, huyo Mwinyi kachukua nyumba za msajili wa majumba hapo Dar hazipungui kumi kawapa hadi wajukuu wake majumba ambayo hakuyatolea hata ndululu! bado utasingizia Ujamaa!
Zakumi,
Katika mashirka yote yaliyobinafsishwa sijui elfu 3, asilimia kubwa imejengwa na mwalimu..Ukinunua gari mwaka 1960 lazima uelewe siku moja litakuja kufa hivyo ni muhimu ujiandae kwa miaka ijayo..Yes, mwaka 2009 hilo gari la mwaka 1960 litaonekana kuwa ni la kupikia mabumunda na togwa but still lina thamani kwa wanaojua..sidhani kama ulitegemea Nyerere afikirie sayansi ya utengenezaji magari mwaka 2009 hivyo asubiri hadi teknologia hii itakapo kuwepo!
Tukishindwa kuelewa hivyo basi hapo ndipo tulipo haribu!