Nini unachokikumbuka kwa mtu ambaye hayupo leo duniani

Nini unachokikumbuka kwa mtu ambaye hayupo leo duniani

Nayakumbuka yote aliyonifanyia Baba yangu..alikuwa mwalimu wangu..faraja yangu..rafiki pia..miaka mitatu Sasa Naona Kama Jana..[emoji22]

Rest well Daddy..kabinti kako kadogo kanakukumbuka kila iitwapo leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee! Naamini nawe utakuwa Mama mwema kwa wanao. Wape upendo kma uliopewa na Dady
 
Naikumbuka sauti yake kwa Mara ya mwisho.."kabinti kangu alhamisi narudi nyumbani tule pasaka pamoja"

Alhamisi ikafika namsubiri Baba sebuleni mdogo wangu ametoka kanisani kwenye ilikuwa alhamisi kuu..akaingia ndani ananiambia dada ..Baba kapata ajali..nilipatwa na bumbuwazi ninachokumbuka baada ya pale nikakimbilia chumbani nikapiga magoti nakusali.

Mama na dada na mdogo wangu wakaelekea hospital..baada ya muda wanarudi mama ananiambia kavae Dela maana nilikuwa na kitenge..nikajua tunaenda wote hospitali..naelekea sebuleni Naona Kaka zangu na vijana majirani wanatoa vitu nje...ile siku sitakaa niisahau.

Sent using Jamii Forums mobile app
kuna tukio katika maisha ni zaidi ya kovu kwenye moyo!.
Kesho yako itakuwa vizr zaidi ya jana!
 
Tulio wai kupoteza watu waliochangia leo kuwa kama tulivyo.

Wana Jf.
Katika kuishi tunakutana na watu wengi sana lakini wapo watu ambao kamwe hatuwezi kuwasahau pindi wanapo tangulia mbele ya haki (kifo).

Hii ni kutokana na sababu nyingi zikiwemo ukaribu, urafiki, undugu pengine Mahusiano yetu na matendo yao.

Nakumbuka Anko alifariki wiki 1 tu baada ya kuanza matibabu ya mkono wangu uliokuwa umevujika! Aliniacha bado sijapona ukweli niliumia na kulia sana japo haikubadili uhalisia.
nakukumbuka Anko X!

Japo nilipona badae ashukuliwe Mungu!

Karibuni wanajamvi kwa kile ulichowai kutendewa au kutenda kwa mtu ambaye hayupo duniani! Kupitia hilo ndio linakufanya umukumbuke!

Mapendo na busara za wazazi wangu.
 
Naikumbuka sauti yake kwa Mara ya mwisho.."binti yangu mdogo alhamisi narudi nyumbani tule pasaka pamoja"

Alhamisi ikafika namsubiri Baba sebuleni mdogo wangu ametoka kanisani kwenye ilikuwa alhamisi kuu..akaingia ndani ananiambia dada ..Baba kapata ajali..nilipatwa na bumbuwazi ninachokumbuka baada ya pale nikakimbilia chumbani nikapiga magoti nakusali.

Mama na dada na mdogo wangu wakaelekea hospital..baada ya muda wanarudi mama ananiambia kavae Dela maana nilikuwa na kitenge..nikajua tunaenda wote hospitali..naelekea sebuleni Naona Kaka zangu na vijana majirani wanatoa vitu nje...ile siku sitakaa niisahau.

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole babe... Mwanga wa milele umuangazie
 
Cause she's the girl that I never had She's the heart that I wanted bad
The song I heard on the radio That made me stop and think of her
And I can't, I can't, I can't concentrate anymore
And I need, I need, need to show her what her heart is for It's been mistreated badly
Now her world has started falling apart Falling apart

Jamie scott- unbreakable

I miss you
R.I.P

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Namkumbuka rafiki angu Josephine alikuwa akinipitia tuende kanisani. Ndiye alikuwa best friend kimtaani.....

Usiku mmoja nikapata taarifa ya msiba wake. I was shocked kwa kweli sbb aliumwa malaria tu 😢😢 aisee that night was very bad.
May your soul continue resting in Paradise J wangu.

Mwanga wa milele uwaangazie marehemu wote wapumzike kwa amani 🙏
 
Back
Top Bottom