Nini utofauti kati ya Landcruiser VX na Landcruiser

Huyu mnyama unakatiza naye barabara yoyote
View attachment 1629571
Kuna series nyingi za Toyota land cruiser kuanzia f20, f30, f60, f70, f80, f90, f100 na F200. Katika matoleo yote f70 ndio toleo la Land cruiser limedumu kwenye uzalishaji mpaka leo na lina maisha bado. Kikubwa pamoja na kubadilika kwa technology ya transmission wao huwa hawana Automatic ni manual transmission tu.
 
Mkuu kuna Land Cruiser series 70 LX na ZX zinakuja na mfumo wa Automatic Transmission ila injini ni ile ile 1HZ.
 
Wewe utakuwa unazungumzia gx ya miaka ya nyuma sana!
Hapana inawezekana kabisa, nimeendesha ford ranger za 2016 / 2017 version mbili tofauti kuna nyingine handle ya kupandisha window ni kuzungusha mpaka side mirror ni manual ila field shughuli yake ni nyingine. Na kuna version nyingine kila kitu ni umeme kuanzia seat adjustment, side mirror, na power window za kibabe tu.
 
P

Lx sio body type ......refer here

Prado zote nne so far kila kizazi neno TX linapatikana.. huwezi sema ni body type wakat zote nne ni body tofauti

Hizo herufi ni trim
 
Matairi ni makubwa, rimu yake pia imekaa kishamba ila ni ya kazi sio rimu ya kuuzia
 
Kweli, hizo initial GX, GXL, VX, ni classes ndani ya kila series za land cruiser. Kwa toleo LC200 GX huwa ni full manual. Hata rims zake huwa ni steel na sio alloys na rangi yake mara nyingi ni white na ina mkonga (snorkel). Kuanzia GXL na matoleo mengine ya juu yanakuwa graded kulingana na vitu vya ziada vilivyokuwa installed ili kutoa luxury experience. V8 nyingi za MaDC huwa ni GX, kidogo MaRC ndio wanakuwa na GXL na VX. Na Mkuu anatumia limited Edition SAHARA Horizon. Namna ya kutofautisha GX, GXL, VX na SAHARA https://www.toyota.com.au/landcruiser-200
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…