Ninunue ipi kati ya Bajaj na Gari kwa biashara ya Bolt

Ninunue ipi kati ya Bajaj na Gari kwa biashara ya Bolt

Umeongea bonge la point, kweli mkoani bajaji used zipo nyingi ukibahatika ya 3M ni kama mpya
Bora ununue mpya moja kuliko ununue bajaj chakavu mbili za 3M utalia na unaweza ukaisusa gereji au ukazipaki nyumbani maana utakua umefunga nazo ndoa ya kikristo hautapata mteja wa kumuuzia
 
Kamanda mkataba wa Bajaji ni miezi 18 sio miaka miwili hili ninauzoefu nalo

Hiyo miaka miwili ni gari.

Kwanini miezi 18 isiwe 24? Maana wewe ndiye unayetoa mtaji na wewe ndiye unayempa maisha.

Mf; Life expectancy ya engine ya Bajaj TVS ambazo ndio zinapendwa ikimpata mtu anayejielewa ina uhai wa zaidi ya miaka 5 bila kutiwa vidole na fundi, service kubwa ya Bajaj ni rubber za kwenye miguu tu na oils hamna kingine so tuseme baada ya miaka yako miwili ya mkataba bado atabaki na chombo salama miaka mitatu ndo kianze kumsumbua.
 
Nenda mikoani kanunue bajaji chakavu hata laki 7 aifiki,ilete mjini peleka gereji mburahati huko gharama kuirudisha barabarani haizidi milion 2.

Kwa hiyo ela unapata bajaji 2 na kuziweka barabarani.

Just imagine yourself
Usije fuata huu ushauri kwani mafundi watakufanya wewe ndo DECI/Q NET yao ya kuvuna pesa maana hio spana popote
 
Usije fuata huu ushauri kwani mafundi watakufanya wewe ndo DECI/Q NET yao ya kuvuna pesa maana hio spana popote
Hahaaaaa eti DECI.... ila ni kweli kbs kuna mwamba anapenda sana kununua vyuma chakavu yaani. Tena vile chronic fikiria mtu ananunua Nissan Murrano imepiga shimo huko babati zaidi ya Km 300k.......daily utamkuta garage na overlorry kama yy ndo fundi.... ununuzi wa vyuma chakavu umemfanya afanane na mafundi garage kwa mavazi na tabia. Akinyoosha tu mkono zile kucha unajua huyu fundi.
 
Anyway, hapa Dar nimeambiwa ni 2 years mkuu kwa bajaji mpya na daily ni hy 20k
Mkataba ni miaka miwili usishushe hata kidogo, mkataba utakaoingia na dereva uwe na kipengele kwamba kama dereva hajawasilisha hesabu kwa wakati uwe na uwezo wa kumwajibisha mdhamini wake (hii ni muhimu sana maana driver anaweza asilete hesabu kwa wakati ukamfata mdhamini akakwambia “mimi nahusika dereva akikimbia na Bajaj” so utakapotaka kuvunja mkataba baada ya dereva kusumbua sana utaacha hela zako nyingi nyuma).

Chuma funga GPRS kwa usalama zaidi,bima kata compressive mwaka wa kwanza wa pili kata ya kawaida or com'ssve ila ishushe thamani ili ulipe kidogo maana hapo dereva anakuwa ndiye mlinzi wa chombo zaidi.usimpe dereva Bajaj ikiwa uchi mpe favor mkopeshe pesa mwambie atazilipa mwisho wa mkataba ili aweke roof na milango ya pembeni pamoja na ngao ili kwanza iwe rahisi kwake kufanya kazi pia body iwe salama.

NB; Zingatia sana kumpa chuma mtu anayejitambua hasa mwenye mke ili mkewe awe ndo mdhamini wake na wawe wanahimizana ukiwapa hawa yoo yoo watakusumbua kazi utaiona chungu.

Hope nimesaidia kiasi kama kuna nilichosahau wataongeza wengine,kila la heri mkuu.

Sent from my Redmi Note 5 using JamiiForums mobile app
 
Kamanda mkataba wa Bajaji ni miezi 18 sio miaka miwili hili ninauzoefu nalo

Hiyo miaka miwili ni gari.
Mimi nipo Dar na kwa huku nimeambiwa ni miezi 24. Inawezekana inatofautiana kati ya mkoa na mkoa mkuu
Mkataba ni miaka miwili usishushe hata kidogo,mkataba utakaoingia na dereva uwe na kipengele kwamba kama dereva hajawasilisha hesabu kwa wakati uwe na uwezo wa kumwajibisha mdhamini wake (hii ni muhimu sana maana driver anaweza asilete hesabu kwa wakati ukamfata mdhamini akakwambia “mimi nahusika dereva akikimbia na Bajaj” so utakapotaka kuvunja mkataba baada ya dereva kusumbua sana utaacha hela zako nyingi nyuma)...
Umesaidia sana mkuu. Asante. Vip unaeza kuwa na sample ya mkataba plz kama unaona turudi Pm nikupe email address untumie mkuu.
 
Biashara ya bajaji inalipa Sana kama unafanya mwenyewe na inalipa kidogo Sana Kama ukimkabidhi mtu muaminifu ila ukikutana na mtu mwenye tamaa mwsho inakutia umaskin mtu siku nyingine anapiga bingo had 50 kwa siku alaf anakupa...
Mikataba ukipata watu wanaojitambua hela unapata,chuma unazi-monitor kwa GPS ukiziona mtaani muda ambao siyo elekezi kwenye paper unamuonya dereva akupe sababu ninini kimesababisha sababu hazina point unaizima unaifata ilipo that's why inasisitizwa tafuta watu smart wanaojua ninini maana ya maisha hawa waluwalu watakutia stress.

Sent from my Redmi Note 5 using JamiiForums mobile app
 
Mimi nipo Dar na kwa huku nimeambiwa ni miezi 24. Inawezekana inatofautiana kati ya mkoa na mkoa mkuu

Umesaidia sana mkuu. Asante. Vip unaeza kuwa na sample ya mkataba plz kama unaona turudi Pm nikupe email address untumie mkuu.

Ninao mmoja ambao hiki kipengele cha kuweza kumkamata mdhamini sikukiweka mwanzo ila nilipopata changamoto ndiyo nikaujua umuhimu wake,nakutumia pic pm utautazama mfano wake
 
Mkuu nimechukulia siku za mkataba yaani miaka miwili; mwaka mmoja siku 365, miaka miwili siku 730. Hope umeelewa. Na nimefanya hivyo kwa kuwa makipo ni kwa siku ambayo ni 20k.
Sawa, na tumeelewa hivyo. Ila katika original statement yako ulisema hivi ..... "...hivyo kufanya kwa mwaka kuwa 20,000× siku 730=14,600,000..." Nanukuu. Hapo ulibidi useme kwa miaka miwili. Lakini tumekuelewa mkuu.
 
Mikataba ukipata watu wanaojitambua hela unapata,chuma unazi-monitor kwa GPS ukiziona mtaani muda ambao siyo elekezi kwenye paper unamuonya dereva akupe sababu ninini kimesababisha sababu hazina point unaizima unaifata ilipo that's why inasisitizwa tafuta watu smart wanaojua ninini maana ya maisha hawa waluwalu watakutia stress.

Sent from my Redmi Note 5 using JamiiForums mobile app
Mkuu ni GPS ya aina gani hiyo inayo weza kuzima bajaji?

Au ni kifaa gani wanakitumia... Naomba kujua.
 
Mkuu ni GPS ya aina gani hiyo inayo weza kuzima bajaji?

Au ni kifaa gani wanakitumia... Naomba kujua.
Nitakupa namba za jamaa yupo Ilala ndiye anayenifungia zangu,natumia app za iTrack na Tracker Home chuma unazima kwa sms tu muda wowote iwe inatembea iwe ime-park.

Nakutumia PM mkuu.
 
Back
Top Bottom