Wakuu naombeni ushauri. Nipo njia panda mm kama kijana wa miaka 27 napata ukakasi juu ya mstakabari wa maisha yangu. Saa nyingine navutiwa na kutafuta mwanamke ila saa nyingine nikifikiri mambo Yao kutoka Kwa watu wanao nizinguka Nakata tamaa. Pia nikiangalia Dunia ilichonipa Wala hakina nguvu Kwa Sasa kuniwezesha mimi kuwa na familia. Sasa utata unakuja kama nisipo oa maana yake hata mtoto sitegemei kuwa nae Kwa Sababu sitaki kuwa na mtoto bila ya ndoa kutokana na niliyoyaona kwangu na ninayo yashuhudia kutoka Kwa watoto Wa aina hii. Kwa hiyo wakuu naombeni ushauri nitaishije kama mwanaume bila ya mke wala mtoto