Unasubiri yakukute ya 20%? Anza upya.. si Ujinga.. we wa kiumeni.. acha kulialia..aliyekengeuka ni mwanamke na si wewe...!!:crazy:Ndugu zangu naombeni msaada kwenye kisa hiki cha kweli . nina mke tuliyefunga ndoa yapata miaka 11 iliyopita, mke wangu tulikutana kazini kwenye kiwanda cha kutengeneza biscuits ambapo yeye alikuwa teller mimi ni mwendesha mashine.
Baada ya kuoana nilimwendeleza kimasomo kwakuwa yeye alikuwa wa form IV nami ni darasa la saba, kwakuwa alifanya vizuri katika kozi zake alifanikiwa kupata kazi kwenye shirika moja la kimataifa kama administrative secretary.
Sisi huku kiwanda kilifungwa kutokana na biscuits kukosa masoko kutokana na ushindani uliopo hivyo nikalazimika kukaa nyumbani huku nikijitahidi kutafuta vibarua vya hapa na pale.
Issue ni kwamba mke wangu sasa amekuwa mbogo hataki kusaidia kitu chochote hapa nyumbani na ikitokea akatoa hela basi masimango yanatisha, tutaitwa majina ya kila aina mara poyoyo, mara Mario nk.
Wakati tunaoana kila mmoja alikuwa na mtoto na wote tulikuwa tunawalea kwa mapenzi bila ubaguzi, cha kushangaza yeye mtoto wake kampeleka international school wa kwangu amemwacha aendelee na hizi za kayumba!
Kinachonipa taabu sana ni kurudi usiku wa manane wakati mwingine akiwa amelewa nikimuuliza anasema walikuwa na kazi nyingi na mikutano inayoambatana na vinywaji, pia ana safari nyingi za kikazi na akifika huko huwa hataki nimpigie simu eti namsumbua!
Sasa je huyu bado anastahili kuwa mke wangu? Si kawa wa mataifa sasa niachane naye nikaoe mwingine?
Vikao vya wazee vimeshindwa kutoa ufumbuzi wanamuogopa au sijui ni kwamba anawakatia mkwanja mrefu?!
Nawasilisha
Kuna mada ulikuja nayo hapa ukisema kama nakumbuka vizuri uamini ndoa. Kuna siku nikakushauri umtokee yule mheshimiwa wa kawe kwani yeye ataka mtoto tu si kuolewa. Kuna nyingine ulisema nyie medical doctors mna ethics. Sasa hii unasema wewe ni std seven. Anyway michango ni muhimu kwa wale wenye situation kama hiyo.
Pole sana ila sikushauri kuoa mke mwingine maana utamuongezea midomo ya kulisha naye atazidi kuwanyanyasa. Fight na maisha kwanza yakae level kwa faida ya mtoto wako.
Nyumba kubwa
Toa ushauri tafadhali kumsaidia Bwana Mulama - JF watu wanavyeo/fani na majina bandia
Nakushukuru kwa umakini wako mkuu ila sasa nakushauri upitie upya "the art of the representations" utapata majibu yote. unajua nyie wasomi mnajua mengi kunizidi nisiyesoma inawezekana ukashindwa ku premise hoja zangu kwa sababu zina miss comprehensiveness component!
Mulama,
Umeshaanza maadalizi ya QT? Maana naona kwa STD VII hapo kwenye RED yawezekana ulisoma ENZI ZA MWALIMU!
Eti MwanajamiiOne, hiyo hapo nyekundu ​huwa kweli inawezekana kwa binadamu?Mulama.... Pole sana, kama una uhakika wa hili basi oa mke mwingine... Lakini zungumza nae kwanza na kama kweli anakupenda basi atajirekebisha
Mulama,
Umeshaanza maadalizi ya QT? Maana naona kwa STD VII hapo kwenye RED yawezekana ulisoma ENZI ZA MWALIMU!
Mulama,
Kama ndoa yako ya miaka 11 ni halali na kama hii hoja umeileta ikiwa ni wewe mwenyewe muathirika basi nakushauri usikurupuke kuoa mwanamke mwingine...
Kuoa TENA hakujawahi kuwa ni suluhisho la matatizo ya ndoa duniani kote - Mke wa pili huwa ni MBAYA zaidi kuliko Mke wa kwanza, na watatu ni mbaya zaidi kuliko wa pili, e.t.c.
Kutokana na post yako inaonekana mkeo wa kwanza mlishaachana (kwa uzuri au kwa ubaya), equally na mkeo wako huyu "msumbufu" alikwisha achika (kwa uzuri au kwa ubaya) and that tells me that nyote ni "broken-heart" kwa kuwa mahusiano yenu ya kwanza YALISHINDWA KUSIMAMA.. Kwa mantiki hiyo basi, inawezekana sana hata hiyo miaka 11 imekuwa ni ya "kubahatisha" zaidi na ndiyo maana wewe binafsi umeshindwa kuongeza hata elimu kiasi cha kutosha na mkeo pia haujamsomesha kiasi cha kutosha..
Administrative Secretary (post form IV) siyo "investment" ki-elimu bado angaweza kuwa kwenye nafasi kubwa zaidi kama kumsomesha kwako na mahusiano yenu ya ndoa yangekuwa IMARA toka mwanzo.. Na wewe pia kama ungekuwa hauna "element" ya "Utegezemezi aka Mario" kwa miaka kumi na moja ungekuwa una japo Diploma na au umejiajiri mwenyewe e.t.c
Kwahiyo I would boldly say, Ndoa yenu haijajengwa kwenye msingi imara, na, kwa maana hiyo basi inabidi NYOTE wawili mrudi kwenye "drawing board" na muanze upya kutengeneza ndoa yenu, of which naamini kwa msaada wa Wazazi, Ndugu, na Viongozi wa Imani za kiroho mnaweza kuanza upya maisha mema ya ndoa yenye heri na baraka... Ikishindikana, basi, ni vyema, kila mmoja akachukua mkondo wake mpya wa maisha na ku-MOVE ON kwa maana kuwa you two were not meant for each other...
Jioni Njema - Nawahi Bia za Baridi pale Baracuda kabla Tanesco hawajakata umeme!