NIONAVYO: Michezo ya ligi NBC baadhi kuchezewa Amani stadium, Bodi ya ligi sio wa kulaumiwa:

NIONAVYO: Michezo ya ligi NBC baadhi kuchezewa Amani stadium, Bodi ya ligi sio wa kulaumiwa:

Tsyamatsy

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2023
Posts
265
Reaction score
421
Kumekuwa na songombingo kuhusu baadhi ya Michezo ya ligi ya NBC Bara kwenda kuchezewa katika uwanja wa Amani Zanzibar.
Mjadala umekuwa ni mpana. Suala hili lilianza pale Simba walipokuwa wanatafuta uwanja wa kuchezea baada ya Lupaso kufungwa na Simba kutotaka kutumia uwanja wa Azam Chamazi, ndipo kulipozuka tetesi kuwa SSC walitaka kuutumia uwanja wa Amani lakini Kwa wakati huo kanuni za Bodi ya ligi hazikuwa zinaruhusu.
Baada ya muda Bodi waliangalia kanuni zao na hatimae wakazirekebisha na kuruhusu Kwa timu inayopenda kwenda huko iende.
NIONAVYO: Kwa suala hili la ligi Michezo kupelekwa Zanzibar wakulaumiwa sio Bodi bali Kama ni lawama basi wakulaumiwa ni TIMU yenyewe inayochagua kupeleka mchezo wake huko. Sababu Bodi "HAILAZIMISHI" timu yoyote kuchezea huko Bali ni matakwa ya Club husika.
Club husika ndio wanajua wanachokifuata huko na wanafaidika na nini. Pia ni Club ndio inayopaswa kuangalia na kuelewa kuwa wanachama na wapenzi wake wanafaika vipi Kwa wao viongozi kupeleka mchezo huko. Kwa maana hakuna kanuni inayo' WALAZIMISHA' Wao kwenda huko NI kiherehere Chao Tu.
 
Basi kama serikali kasi yake ya ujenzi wa viwanja ni ndogo,Itumike PPP viwanja vijengwe viwe vitega uchumi vya manispaa wa vitakapo jengwa.
 
Bei ya kiingilio anapanga nani?
Utajua
Labda unieleweshe, kwani kuna tofauti anayepanga kiingilio mechi za NBC ligi zikifanyika Bara na hizo zinazopelekwa Zanzibar?? Na je, upangaji wa bei unahusika vipi
Hivi umeelewa ulichoandika, umesema msimu uliopita kulikuwa na tetesi za Simba kuomba kucheza amani lakini Bodi ya ligi ilikataa sababu kanuni haziruhusu. Msimu huu Bodi ya ligi imerekebisha kanuni lakini hutaki Bodi ya ligi ilaumiwe. Kama msimu uliopita walizuiwa kwanini msimu huu wameruhusu.
Inawezekana umekurupuka Tu kuandika na huelewi, inabidi nikueleweshe, misimu iliyopita hakukuwa na kanuni za kuruhusu Michezo ya ligi kuu ya Tanganyika kwenda kuchezewa Zanzibar. Na ili kukidhi hayo mahitaji ndio iliwabidi warekebishe kanuni zao na kuweka kingele cha kuruhusu kwenda huko.
Sasa hizo club zinazochagua kwenda huko ni viherehere vyao Tu.
 
Ni sababu za kishirikina tu ndio zimewafanya Azam wapeleke game huko kwa hisani ya utopolo
 
Labda unieleweshe, kwani kuna tofauti anayepanga kiingilio mechi za NBC ligi zikifanyika Bara na hizo zinazopelekwa Zanzibar?? Na je, upangaji wa bei unahusika vipi

Inawezekana umekurupuka Tu kuandika na huelewi, inabidi nikueleweshe, misimu iliyopita hakukuwa na kanuni za kuruhusu Michezo ya ligi kuu ya Tanganyika kwenda kuchezewa Zanzibar. Na ili kukidhi hayo mahitaji ndio iliwabidi warekebishe kanuni zao na kuweka kingele cha kuruhusu kwenda huko.
Sasa hizo club zinazochagua kwenda huko ni viherehere vyao Tu.
Anayetengeneza kanuni ni nani?
Bodi ya ligi mipaka yake inaishia wapi?
Ligi ya Zanzibar inasimamiwa na nani?
Zanzibar Wana ligi yao na bara tuna ligi yetu kwanini ligi ya bara ipelekwe Zanzibar.
Je huku bara Kuna vita Kama ilivyotikea Sudan aukuna majanga yanayozuia ligi isichezwe.
 
Basi kama serikali kasi yake ya ujenzi wa viwanja ni ndogo,Itumike PPP viwanja vijengwe viwe vitega uchumi vya manispaa wa vitakapo jengwa.
Uwanja Kama wa Kaitaba Bukoba ni wamanispaa lkn hauna ata flame moja ya biashara .
 
Hivi umeelewa ulichoandika, umesema msimu uliopita kulikuwa na tetesi za Simba kuomba kucheza amani lakini Bodi ya ligi ilikataa sababu kanuni haziruhusu. Msimu huu Bodi ya ligi imerekebisha kanuni lakini hutaki Bodi ya ligi ilaumiwe. Kama msimu uliopita walizuiwa kwanini msimu huu wameruhusu.
Wameboresha. Kanuni si sheria wala msahafu.
 
Back
Top Bottom