Nimeshangaa mara kadhaa lugha hiyo inatokea wapi "Chanjo inayobadilisha mfumo wa DNA" (Gwajima na Shekhe farid Mussa wanasambaza habari hiyo).
NAdhani pamoja na kiwango cha duni cha elimu sababu yake ni hii: madawa ya chanjo za COVID zinapatikana kwa njia tofauti.
1) chanjo za kawaida; hapa wanatumia virusi zilizodhoofishwa, au kuuawa; ikiingizwa katika mwili, mfumo wa kinga mwilini unaitambua na kutengeza askari dhidi yake zinazoweza kushambulia virusi hai na kuziua. Namna hiyo ya chanjo ni namna iliyokuwa kawaida hadi juzi, ni namna ya chanjo zote za magonjwa mbalimbali tulizopokea kama watoto, dhidi COVID mifano yake ni Sinopharm na Sinovac kutoka China na Bharat Biotech kutoka Uhindi.
2) chanjo zilizopatikana kwa njia ya kuchezea DNA / RNA ya virusi yenyewe ambayo ni tekinolojia mpya sana (mifano Biontech, Johnson, Astra). Hapa vipande vya DNA au RNA vya virusi vinabadilishwa katika maabara na kuingizwa katika mwili, ambavyo haviwezi kusababisha ugonjwa lakini vinasababisha jibu la mfumo wa kinga mwilini unaotengeneza askari husika.
Naona lugha ya "genetically modified vaccine" imesababisha imani kwamba chanjo hizo zinabadilisha muundo wa DNA mwilini. Ambayo si vile, inayochezewa ni mfumo wa DNA / RNA ya virusi kabla ya kuingiza chanjo mwilini.
Bila shaka anayependa kuamini na kuwafuata akina Gwajima na Farid Mussa hataniamini. Anayependa kujielimisha anaweza kusoma kwa mfano hapo
https://en.wikipedia.org/wiki/COVID-19_vaccine, na usipopenda kutegemea Wikipedia ni sawa, unapata vyanzo vingi sana kwenye tanbihi ya makala uanpoweza kujenga hoja mwenyewe.
(Sijui kama ni faida kwamba siku hizi kuna chaguo baina ya ujinga uleule kwa ladha ya Kiislamu na ladha ya Kikristo. )