Nionavyo mimi: Miaka kumi ya Rais Magufuli umasikini utaongezeka sana

Mkulima gani wewe aliomba Serikali imsaidie kununu Korosho?

Kwa kukusaidia tu, wakati haya yanatokea Prof. Magigi ndiye alikuwa Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho na Byakanwa mkuu wa Mkoa. Mkurugenzi aliwaomba wakulima wauze kutokana na bei ya soko la Dunia lakini RC-Byakanwa alikuwa anapita usiku na polisi kuwaambia wakulima wasiuze na ndio maana kwenye minada kadhaa kuna baadhi walikataa na tena sio wakulima perse.

Ndipo mkuu wa nchi akipoambiwa kuwa Korosho ni deal. Lakini kabla kumbuka JPM alimuagiza Majaliwa aongee na wafanyabiasha na siku ile saa kumi walikuwa na mkutano Ikulu ila JPM alikataa kabisa kuchukua ushauri na taarifa ya Waziri wake Mkuu na badala yake yeye akaamua Serikali itanunua korosho zote.

Kwa taarifa yako zile korosho walitegemea watauza zaidi ya 4,000/= lakink badala yake Serikali imekuja kuuza chini ya 2500 na ndio maana mpaka leo haitaki kuwalipa wakulima wa korosho na kumbuka hapo wametumia Wanajeshi na wadau mbalimbali kama vile watunza maghala.

Mambo ni mengi aisee, wewe ingekuwa mkulima ungejua angalau baadhi. Ila unatumia 'speech' za viongozi wa kisiasa kusema watu wamelipwa na wew ni mkulima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
waliompa urais nadhani wanajuta. anaweza kwa kiasi kidogo uwaziri. nchi hii ni kubwa mno huwezi kuiendesha kibabe kama familia yako. amenunua ndege kibabe, anajenga mega projects kibabe. anahangaika na chadema kibabe. kila kitu ubabe huwezi kufanikiwa kwa sababu mwisho wa siku lazima ujue kuwa unaowafanyia ubabe siyo ng’ombe, ni binadamu. nadhani miaka mitano inamtosha.
 
Meko,Dotto na Bashite ni Mabilionea.

If you can't stand the heat,get out of the kitchen.
 
Wanajitokeza wengine kushangaa au kusikia Ni Mimi ataongea lakini sidhani kama ndio kumkubali na wengi hawana jeuri ya kumuuliza . . Nakumbuka yule mmoja tu kule Tabora sijui Igunga ile, alimwambia aachie fedha hali Ni mbaya.
I think people in rural areas don’t even know what poverty means! They live with it and get used to it.
We fill sorry for them but they don’t know anything, they think that’s a normal life
 
Sawa wewe ndie mkulima. Lakini haujajibu swali ulitaka serikali ifanye nini wakati wakulima wakakataa wenyewe kuuza wakisema bei ni ndogo?
 
Sawa wewe ndie mkulima. Lakini haujajibu swali ulitaka serikali ifanye nini wakati wakulima wakakataa wenyewe kuuza wakisema bei ni ndogo?
Umemuelewa lakini mchangiaji? Wale hawakuwa wakulima.

Haya hata kama walikuwa ni wakulima wajibu wa serikali unadhani ulitakiwa uwaje.?

Kilichowakumba kusini kwenye korosho ni Mungu wa mbinguni ndiye atakayesamehe.

Ni moja ya maamuzi mabovu kabisa kuwahi kufanywa na serikali.

Sent using iphone pro max
 
Africa kuendelea ni ndoto haina strategic planning kila ajae uja na yake ili avute 20% anaiba kwa ajili ya familia yake.Halafu akishindwa kujiletea maendeleo japo ana kila kitu lawama anatupiwa mzungu
 
Noma sana! Mirija imekata na akili zimerudi.
Kuna kipindi fulani miaka ya nyuma niliwahi kuongea na polepole kipindi hicho alikua mkuu wa wilaya nadhani.
Huwezi amini ndio huyu wa sasa hivi kwa jinsi alivyokua anamponda Jiwe kuhusu maswala ya uchumi
Ni hulka ya mswahili anaposhiba akili huwa likizo
 
Raisi wa Russia, Vladimir Putin amesema..
"AFRIKA NI KABURI KWA WAAFRIKA"

"Muafrika anapokuwa tajiri anaweka fedha zake kwenye mabenki ya Switzerland. Anaenda ufaransa kwa ajili ya matibabu.

Anawekeza kwenye nchi za Ulaya. Anafanya shopping Dubai.Ananunua bidhaa kutoka China. Anasali Roma au Macca. Watoto wanasomeshwa nchi za Ulaya. Anasafiri nchi za Canada, Ulaya na Marekani kufanya Utalii.

Siku Akifa Anaenda Kuzikwa Kwenye Makaburi ya Kijijini kwao.

Kwahiyo AFRIKA ni makaburi tu kwa Waafrika. Kwani umeshaona wapi Makaburi yakiendelezwa?

~Putin Asks
 
Sawa wewe ndie mkulima. Lakini haujajibu swali ulitaka serikali ifanye nini wakati wakulima wakakataa wenyewe kuuza wakisema bei ni ndogo?
Waziri mkuu akishakuwa na kikao na wafanyabiashara na Ni wazi kilikuwa na. Muendelezo mzuri mpaka pale Bwana mkurupukaji alipovamia kikao na kuleta ubabe was jeshi. Kila kitu jeshi kana kwamba ndio suluhisho la kila kitu. Hebu muulizeni kile kiwanda alichosema jeshi wajenge cha korosho kimepotelea wapi?
 
Ni Rais mzuri sana, Mthubutu na Mtu anayejiamini mno ila kama kuna Kitu ambacho amefeli ni kupata Washauri ( Wasaidizi ) walio Wanafiki sana.
 
 
Hakuna jambo gumu duniani kama kuwaridhisha Watanganyika sababu hawaeleweki ni kipi wanachokihitaji.
Maana kama raisi isingeliiangilia kati kutatua hilo tatizo ungeliwasikia wanalalamika kwamba serikali haitatui shida za wakulima.
Hongera JPM naipenda Tanzania.
 
Hebu tuambie maisha bora kwa kila mwananchi ni yapi. Unajua kuna vitu mnavisema na hamjui maana yake nini

God save us

Wewe kama mpaka leo hujui nini maana ya Maisha Bora kwa Kila Mtanzania ni vyema ukaendelea tu kulamba miguu ya Humphrey Polepole hapo Lumumba! Sitakuambia hiyo maana yake. Sawa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…