Nionavyo mimi: Miaka kumi ya Rais Magufuli umasikini utaongezeka sana

Nionavyo mimi: Miaka kumi ya Rais Magufuli umasikini utaongezeka sana

Sikia nikweli uyasemayo ila angalia kwa mapana hathari ya kiuchumi kwa wale sio mafisadi pili lipo kundiktk utawala wake wanakula nchi nani asie juwa? Sasa kama mafisad wapo wapelekwe mahakama ya mafisadi ambayo kwa miaka mitano Sina uhakika imefanya kazi.
Nenda segerea ndio utajua kama zinafanya kazi ana lah

God save us
 
Hii miundombinu anayoijenga wakati huu ingeendana na maisha bora kwa kila Mtanzania, basi Magufuli angekuwa ni bonge la Rais kuwahi kutokea Tanzania!

Kwa bahati mbaya asipochukua hatua mapema, atakuja kushangaa sana hapo baadae nchi yetu ikigeuka kuwa Ethiopia ya pili! Ina mpaka treni ya umeme pale Addis Ababa, ina mradi mkubwa wa kuzalisha umeme kuliko yote Afrika!

lakini wananchi wake kila siku wanakamatwa kwenye makontena ya malori na wengine hata kufia njiani kwa lengo tu la kwenda kutafuta maisha bora nje ya Ethiopia. Kisa ni kuwekeza nguvu kubwa kwenye maendeleo ya vitu na kusahau maendeleo ya watu.

Yaani mpaka mwaka huu 2015 bado napokea mshahara ule ule alioniachia Kikwete!! Halafu badala ya kuniletea unafuu wa maisha, ndiyo kwanza ananiongezea makato ya Bodi ya Mikopo! Ni mfanyakazi mwenye uwendawazimu tu atakaye muelewa Magufuli.
Hebu tuambie maisha bora kwa kila mwananchi ni yapi. Unajua kuna vitu mnavisema na hamjui maana yake nini

God save us
 
WAnatengeneza umasikini kimakusudi sababu wao wanasaza Kodi zetu ni wanufaika ili watutawale.Mwafrika huwa athamini heshima anayopewa na wenzake wampao leseni ya udereva uwalipa mabaya na kuwaona ni wajinga tu tofauti na wenzetu.
 
Wakati ule alikuwa mgombea Uraisi kwa tikiti ya chama chenu alikuwa msafi?

God save us
Niwaulize nyie CCM wenye Tiss/Takukuru/other security apparatus mliwezaje kuruhusu fisadi mpk kufikia nyadhifa ya kua waziri mkuu na mkamuacha agombee urais wa nchi na mpk leo mmeshindwa kumchukulia hatua yoyote ile.
 
Sasa unachopinga ni kipi? Basi tuambie wewe unaejua serikali imenunua korosho kwa bei gani? Na kuhusu watu ambao hawajalipwa shida sio serikali ni viongozi wa vyama vya msingi ndio ambao wanaleta ubabaishaji hasa makatibu wa vyama vya msingi ndio maana wiki kadhaa zilizopita akatangaza kuvivunja na kuvifutia usajili baadhi ya vyama.
Mimi ni miongoni mwa watu ambao nilipima tani kadhaa lakini nikazungushwa kwenye malipo lakini nikaamua kufuatilia mwenyewe kuanzia wilayani matokeo yake wiki tatu zilizopita pesa zangu zikaingizwa kwenye Akaunti tena kwa bei ileile ya 3300.
Tunawaomba nyie chadema kwenye msimu wa Korosho ujao korosho muje muzinunue nyie japo kwa TSH 3000 ili muwanufaishe wakulima
Acheni kuuongopea Umma.
Hongera JPM naipenda Tanzania
Ina maana makatibu wa vyama vya ushirika wakichelewesha malipo ya wakulima wa korosho suluhu ni kuvifuta vyama vya ushirika ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ninachojali pesa yangu nimelipwa haijalishi ni lini.
Wakulima inapaswa wajilaumu wenyewe sababu wanunuzi kutoka India na Vietnam walitaka kununua korosho kwa TSH 2500 wao wakakataa kuuza wakisema bei ni ndogo wakaiomba serikali iwasaidie sasa wewe ulitaka Magufuli afanye nini?
Hapa umedanganya au hujui

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niwaulize nyie CCM wenye Tiss/Takukuru/other security apparatus mliwezaje kuruhusu fisadi mpk kufikia nyadhifa ya kua waziri mkuu na mkamuacha agombee urais wa nchi na mpk leo mmeshindwa kumchukulia hatua yoyote ile.
kojoa ukalale maana huna hoja.
 
Mbona akifanya ziara hasa huko vijijini watu wanajitokeZa kwa wingi na kumshangilia?!
wamezoea hali ya umasikini na kufanya kuwa ni sehemu ya maisha ama hawajui kwamba wako kwenye lindi la umasikini.
Wanajitokeza wengine kushangaa au kusikia Ni Mimi ataongea lakini sidhani kama ndio kumkubali na wengi hawana jeuri ya kumuuliza . . Nakumbuka yule mmoja tu kule Tabora sijui Igunga ile, alimwambia aachie fedha hali Ni mbaya.
 
Tatzo hamueleweki, watu wakipelekwa mahakaman kama wakina rugemalila, kitilya na wengine mnaanza tena kulalamika wanaonewa
Wakipelekwa mahakamani basi wahukumiwe sio kesi zinahairishwa kwa kipindi cha miaka sita kwa kisingizio cha upelelezi bado haujakamilika.
Kama umepeleleza miaka hiyo yote bila mafanikio basi watuhumiwa waachiwe.
Justice delayed justice denied.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wenyewe wakija hapa watakujibu mambo ya SGR,Stigler's gorge,kujenga zahanati kila kata,elimu bure etc

Ndio majibu yao hayo,waulize sasa haya mliyoyasema yanamsaidiaje mtumishi wa umma?Utasikia nyie ni wapiga dili tu.
Wamesahau CAG kabainisha 1.5trilioni haionekani.
 
Umeongelea mambo mengi Ila umesahau stahiki za watumishi wa umma. Hakuna increment wala kupanda madaraja kwa kipindi cha miaka mitano. Pamoja na hayo yote bodi ya mikopo imeongeza makato kutoka % 8 mpaka% 15 nje ya mkataba ambao watu walisaini kipindi wanaomba mikopo. Pamoja na kuongezeka Kwa makato ya HESLB pia zimeongezwa faini mbalimbali kwenye ambazo zinapeleka watumishi kwenye dimbwi la umasikini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii ya bodi ya mikopo ni msiba mzito Sana watu wanakatwa hela almost yote. Serikali ifikirie upya watumishi umaskini umeongezeka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyie ndio wale mnaowaambia wengine wajiajiri wakati nyie mmeajiriwa na ikitokea ajira imeota mbawa mnakufa kwa stress haraka sana
Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza.
JFY nimeacha ajira nimeeudi kujiari kipindi hiki hiki cha. JPM
 
Back
Top Bottom