Nionavyo mimi: Miaka kumi ya Rais Magufuli umasikini utaongezeka sana

Nionavyo mimi: Miaka kumi ya Rais Magufuli umasikini utaongezeka sana

Mtu akitaja korosho machozi huwa yananilenga[emoji30][emoji30][emoji30][emoji24][emoji24]
Mleta mada umeweka mada ya msingi sana
Approach za Magufuli ni kuweka MAVITU na si kunyanyua hali za WATU
Ndiyo maana yuko tayari kuumiza watu ili mavituvitu yake yaonekane

mfano kubomoa nyumba za watu wakati kuna stop order ya mahakama ili ajenge barabara njia nane

Kuacha Korona isambae ilimradi tu akusanye kodi akajenge mamiradi yake

Kuingilia biashara ya Korosho ili serikali yake ipate mihela mingi kupitia mgongo wa wakulima ili akajenge mavituvitu yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu ni mkuu TumainiEl, mbona lugha ni kama imegota?

Mbali na utofauti wa uandishi, mada pia imejikita kwenye mambo yale yale ya 'mavitu, mamiradi' kana kwamba ndiyo kila kitu kinachoifanya Tanzania.

Uharibifu mkubwa anaoufanya Rais Magufuli hauko kwenye kusambaratisha uchumi pekee, kitu ambacho kinarekebishika haraka.

Taifa lililosambaratika, lisilokuwa na umoja wa kitaifa haliwezi kuwa na uchumi endelevu na kuwa na maendeleo.

Kuendelea kuwepo kwenye madaraka kwa Magufuli kutatupeleka huko.

Kwa hiyo sio jambo la uchumi pekee, bali ni uharibifu wa misingi yetu kitaifa ndio utakaoturudisha nyuma zaidi.
 
Onesha msaada ambao serikali ya Magu iliwahi kuukataa ...kuna msaada umetolewa juzi hapa na USAID kupambana na corona. Je USAID ni wajomba zetu?
 
We have moved from easy money.... To hard earned money by working..... There is no longo longo as it used to be..... So suck it!!
Very interesting and valid observation...; how about the following fellows?
- Wastaafu hawalipwi mafao yao.

- Wafanyakazi hawaongezwi mishahara/kupandishwa madaraja.

- Uwepo wa miradi mingi mikubwa inayotafuna pesa za walipakodi mfano. SGR, Stiglers, Bombardier.

- Wengi kufunga biashara zao kwasababu wateja hawana pesa mifukoni.

- Wengi kupoteza ajira kwa sababu ya janga la Corona, na serikali kushindwa kutoa stimulus package.

- Pesa nyingi za walipa kodi kupotea bila kutolewa maelezo yoyote ya maana mfano. 1.5 trillion. Hizi kama zingetumika vizuri zingesaidia kukuza uchumi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Samahani mkuu 'denooJ', imenibidi niku'quote' kumwonyesha huyo mwenye mipasho hapo juu ukali wa bangi wanazovuta siku hizi.
 
Hio iko kwny maandishi tu,ikija kwny utekelezaji ni UPS&DOWN

Hukuwahi kusikia kale ka msemo ka yaani nikuteue mimi,nikupe mshahara,nikulipe posho ya gari na bado umtanganze mpinzani ameshinda hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.
Malizia na kale kakichecho,,

Khee he,, mhhhh,,, Bhaghosha,,[emoji1787]

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu wewe na mleta mada TumainiEl wote mna hoja za msingi.
Habari ya watu kuishi maisha yasiyo na uhalisia wakati wa JK ni kweli kabisa.
Hoja ya mifuko ya hifadhi ya jamii na usumbufu na mateso wanayo pata wastaafu au watu waliositishiwa ajira ina ukweli kabisa, wastaafu wapo katika mateso makubwa na wengine wanakufa huku wakiwa hawajalipwa na wamedai haki zao kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Tukitaka tuende mbele bila kuumiza sana watu wengi inabidi Mh Raisi Magufuli na washauri wake tuwakumbushe au kuwaonesha mahali gani hawako sahihi au wamejisahau.
Unajua ukiwa kivulini si rahisi kujuwa aliyepo juani anaumia kiasi gani. Watumishi wengi wa umma huko ngazi za juu hawayajui machungu au magumu wanayopitia wastaafu na wahanga wa mambo mengine ya huku chini kabisa mitaani.
Ndiyo maana ni rahisi sana kiongozi au mtu aliyepo kwenye ajira kuongea kauli kama watu waende wakajiajiri kwenye kilimo au wafanye biashara au wakafanye vibarua.
Wenyewe wakitoka kwenye hizo nafasi au wakifilisika wengi wanachanganyikiwa kabisa au wanapata magonjwa ya moyo na kufa haraka.

Kujiajiri bila mtaji siyo kazi rahisi, mtaji wa kuuza maandazi hauwezi kulipia bima ya afya ya angalau mtu mmoja tu kwenye familia, wala mtaji huo hautoshi kwenda kukodi shamba, kununua mbegu, mbolea, na madawa ya kuulia wadudu shambani. Kilimo cha sasa bila madawa (viwatilifu) huwezi kuvuna kitu unapoteza nguvu na muda wako.
Umeshusha nondo fupi ila umegusa kila kona. Ndugu yangu kuna shida.
 
Uongezeke mara ngapi wakati ushaongezeka tayari! Tena maradufu.

Mmesahau! 1.5 trillion zilitafunwa na majizi CCM
 
Kutufanya sisi wa kizazi hiki tuumie kwa manufaa ya kizazi kijacho ni upuuzi 1ST CLASS,kinachotakiwa ni SUSTAINABLE DEVELOPMENTS na sio story za kutesana.

Watoto wao hao viongozi wakimaliza vyuo ni kupewa kazi za vitengo vinono kwa vimemo tu lkn watoto wa maskini wao ndio utaambiwa wavumlie na blah blah blah kibao,wao na ndg zao msoto wa kufuatilia mafao hawaujui lkn wananchi wa kawaida wakicheleweshewa mafao yao wanaambiwa wavumilie tu ndio uzalendo huo,wao wako ndani ya ma v8 na wana vitega uchumi kibao lkn bado wanazuga eti nao ni wanyonge yaani ni usanii wa hali ya juu.
Wewe umeelewa mada ila sasa kunaitajika will kutoka tulipo.
 
Nimekaa nakutafakari sana pamoja na kuchambuwa sera na mikakati ya serikali y awamu ya tano ninachokiona huko mbeleni hali ya watanzani kwenye kipato itakuwa mbaya sana jambo pia litasababisha ukosekanaji wa ajira.

Mkuu wa Taifa aka buludoza la mafisadi ataenda pia kuubuludoza uchumi kwakuwa sera zake haziangalii taifa lina hazina kiasi gani na maamuz yake yame elemea zaid kwenye ujenzi wa mager projects jambo ambalo ktk uchumi lina faida za muda mrefu wakati nyuma ukiwaacha watu na umasikini mkubwa na kukosa kaz ktk sector nyingine.

Unapojenga miundo mbinu mikubwa unatengeneza ajira zaid kwa kada fulan kwa wananchi wa sehem fulan. Huwez jenga daraja mwanza ukawafaidisha wana shinyanga lazima ajira zitaenda mwanza zaid kwa mafundi na Eng while wachumi na dk wakiwa hawana ajira au wamechukuliwakidogo.

Sera ya awamo ya Tano itayasinyaisha mabank nakupunguza watu ktk sector hii na sote ni mashahidi vile bank zimefungwa na kuunganishwa while watu wakiachishwakazi ktk kipindi cha kuanzia 2015-2020. Huitaji tochi au mwanga wa juwa kuona Kule tunaelekea na kile kinaenda tokea. Mbaya nikuwa data imekuwa kitu hadim na hili linakuwa msumari wa moto kwenye kidonda.

Wazabun wa serikali wengi wanalipwa mwaka huu tangu mwaka 2015 watu wamedai mpaka wengine umauti umewakuta, hakuna asie juwa ukifanya biashara na serikal unapata faida na pia in create job ila makampuni mengi kwa sasa yameondolew na hayajalipwa pesa zao biashara zimekufa kama uwamini nenda Brela uwauliz Rtn za makampuni mengi kama kwa miaka mitano wameziona? Wengi wamedai mpaka nakampuni wamezifunga.

Biashara ka clearance agency ndio kama imekufa maana serikali imeanzisha chombo , jiulize hizi agency zinaenda wapi? Maelfu Maelfu ajira zimepotea hii sio Afya ni umasikini ktk taifa.

Mifuko ya hifadhi nikweli ilikuwa hoi ila siomifuko yote mfuko kama ppf kabla yakuwa pssf ilikuwa vizuri sana lakini leo unaambiwa wastaafu wanahaha. Kupata mafao yao hivi mtu anafuwatilia mafao yake 2yrs kweli huu niumasikini naukikuwaji wa sheria za kazi. Jambo lakushangaza wanasiasa watalipwa mafao yao haraka wakati mnyonge akihangaikia mafao mpaka anakufa kwa presha.

Ukienda kariakoo utashangaa kuwa Zile biashara tulikuwa kwenye process kuzi rasimisha tupatekodi wengi wamebadilisha mbinu mtu anaona bora aweke mzigo barabarani alipe kitambulisho cha machinga kuliko awe na mlango hili limesababisha kariakoo kuwa soko la wa chuuzi Wala sio soko la kimataifa hii inamanisha nn kwa wachumi? Hii sio ishara nzuri kwa uchumi inamanisha Dalili mbaya kuwa una watu wengi wasiofanya biashara maeneo rasmi. Jambo ni hatari pata picha ya kariakoo 2014 na picha ya 2020.

Idadi ya walio malizachuo na waliopo mtaani inatisha Sina huwakika ikiwa hata theluthi yao wameajiriwa na ukweli ni kwamba hamna ajira tunajenga miundo mbinu hivyo tuna idadi kubwa vijana wasio ajiriwa jambo ni hatari Kule tuendapo.

Mfumo wa Tra ktk sheria ya kodi Tax administration act 2015 from sec 67 and sec68 ni msumari wa moto na kaburi la wafanyabiashara wengi ambao wamejikuta wakiamka masikini. Taifa litakuwa masikini na wananchi watazidi kuwa masikin zaidi kiasi watu watashindwa kununua chupi hasa vijiji, sio kukosa chup ila pia nguo ita kuwa shida why mmebana sana mkasahau pia magendo hupung ukali wa maisha yes taifa hili bado ni changa na yale tunayafanya ktk sera hizi za utawala wa awamo ya Tano kama hatuto angalia vizuri basi hili taifa linarudi pale alipo tuacha Hayati baba wa Taifa.
Vyuma vishalegea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Suluhisho ni nini kifanyike mkuu. Ki ukweli umenigusa Sana hasa ulipojiweka kwenye nafasi ya wafanyabiashara binafsi. Toa suluhisho sasa. Nini kifanyike?

Sent using Jamii Forums mobile app
Jambo kubwa linapaswa kufanyika ni kwanza kukubali serikali inaenda shimon
Pili kufuwata taratibu za kiuchumi wafute ushauri hawezi kufanya yot for ten years
 
Wewe utakuwa mcawi mtarajiwa kama si mchawi tayari! Ina maana kila mmoja alikuwa anaishi maisha ya kuigiza? Mhitimu wa 2016-2019,mstaafu,mkulima wa korosho,pamba,mwenye kiosk n.k wote wana kosa gani? Usikufuru kisa unanufaika na mfumo uliopo leo.Kuna kesho.
Hajuwi alisemalo Wala hajuwi sera za maendeleo huwezi juw msiba wa mwenzio mpaka yakukute.
 
Ungezungumzia vizuri zaidi kivipi wakati hujasomea???? Wewe ndiyo walewale akina Kabudi wanajifanya wanajua kila kitu lakini vitu vidogo tu vinamshinda. Huyu Magufuli ni disaster na ni wa hovyo katika historia ya nchi ya yetu.
Hayo ni maoni yangu kama yalivyo yangu. Lakini Watanzania walio wengi "site" wanamkubali. Anataka kingine kipi zaidi ya hicho?
 
Miaka mitano inamtosha ,nchi ameivuruga balaa ,makadilio ya ukuaji uchumi 2020 ni 2% nchi kaifanya Zimbabwe, mtu una msmlaka yote na una kila kitu halafu unashindwa kupeform ajabu kweli.
 
Ni kweli uchumi uko vzr sana mpk wastaafu sasa hivi kila wakiona matangazo ya mifuko ya hifadhi ya jamii kwny TV wanawaombea kwa Mungu sana

Safi sana kumbe Chadema inamiliki taasisi za uchunguzi wa mambo ya Rushwa/Ufisadi kiasi kwamba ikisema huyu ni fisadi anakua na ikisema huyu ni msafi inakua hivyo.

Asante sana mkuu,umeniongezea jambo kichwani leo.
Chadema kwisha habari yenu. Mtabaki mtandaoni tu.
 
Back
Top Bottom