Nionavyo mimi: Miaka kumi ya Rais Magufuli umasikini utaongezeka sana

Nionavyo mimi: Miaka kumi ya Rais Magufuli umasikini utaongezeka sana

Baada ya hiyo miaka kumi tutampa kura zetu Mbowe ili asahihishe makosa na kufanya uchumi upae hadi mbinguni.
 
Awamu hii ndio pesa imechotwa kuliko awamu zote, ndio maana wanatumia nguvu nyingi kufunika
Sio kwa yale ya mfanyakazi wa Serikali kuwa nyumba zaidi ya hamsini bila ya kuwa na hata biashara yoyote.
 
Utakapo kamilika mradi wa JNHPP ndio utakuja kuona mazuri ya JPM.
Litakapokamilika daraja la busisi to kigongo ndio utakuja kutambua unalalamikia upuuzi.
Pale reli ya Sgr itapoanza kusafirisha mizigo na abiria utakuja kuona aibu.
Maana Cement mwanza ni elfu ishirini lakini itashuka bei na kuwa elfu kumi na tatu.
Nadhani hujaelewa mada , umedandia tu.....Sasa ili uielewe haraka , ulizia bei ya hiyo cement huko mwanza kabla hajaingia huyu bwana , alafu linganisha na sasa....wakati huohuo ujue kipato cha mwananchi hakijaongezeka kwa kipindi chote hicho....ukipata jibu rudia tena kwenye bidhaa nyingine kama mchele, sukari,Unga , Maharage, Sabuni, Nondo, Bati, n.k......Paka hapo utakuwa umeelewa mada alafu uchangie sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wewe na mleta mada TumainiEl mna hoja za msingi.
Habari ya watu kuishi maisha yasiyo na uhalisia wakati wa JK ni kweli kabisa.
Hoja ya mifuko ya hifadhi ya jamii na usumbufu na mateso wanayo pata wastaafu au watu waliositishiwa ajira ina ukweli kabisa, wastaafu wapo katika mateso makubwa na wengine wanakufa huku wakiwa hawajalipwa na wamedai haki zao kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Tukitaka tuende mbele bila kuumiza sana watu wengi inabidi Mh Raisi Magufuli na washauri wake tuwakumbushe au kuwaonesha mahali gani hawako sahihi au wamejisahau.
Unajua ukiwa kivulini si rahisi kujuwa aliyepo juani anaumia kiasi gani. Watumishi wengi wa umma huko ngazi za juu hawayajui machungu au magumu wanayopitia wastaafu na wahanga wa mambo mengine ya huku chini kabisa mitaani.
Ndiyo maana ni rahisi sana kiongozi au mtu aliyepo kwenye ajira kuongea kauli kama watu waende wakajiajiri kwenye kilimo au wafanye biashara au wakafanye vibarua.
Wenyewe wakitoka kwenye hizo nafasi au wakifilisika wengi wanachanganyikiwa kabisa au wanapata magonjwa ya moyo na kufa haraka.

Kujiajiri bila mtaji siyo kazi rahisi, mtaji wa kuuza maandazi hauwezi kulipia bima ya afya ya angalau mtu mmoja tu kwenye familia, wala mtaji huo hautoshi kwenda kukodi shamba, kununua mbegu, mbolea, na madawa ya kuulia wadudu shambani. Kilimo cha sasa bila madawa (viwatilifu) huwezi kuvuna kitu unapoteza nguvu na muda wako.
Lakini maendeleo yoyote yanaambatana na maumivu kidogo. Lakini ni lazma ujue utofauti wa kikwete na magufuli. Alichokifanya kikwete enzi zake makusanyo hayakuwa makubwa sana ila aliweza kujikomba kwa wahisani na wahisani c unajua hawatoi bure ndo ukaona mikataba ya kijinga. Kujikomba kwa kikwete kuliweza kuleta misaada mingi ya kimitego ukiwa uangalii kwa makini utajihisi unapata kumbe unaliwa bila kujua. Magufuli yeye alijua ili nchi iepuke kulizwa rasilimali zake ni kuiogopa kidogo misaada ambayo ndio iliwapa viburi mjini kwa hali hiyo lazma maumivu kidogo
 
Zamani Wakoloni walipotaka kufanya uwekezaji mkubwa walikuwa wanatumia watumwa.
Sasa hivi sera za kuwafanyisha kazi watu kama watumwa hakuna.
Sisi kizazi hiki lazima tuwe kondoo wa kafara kwa ajili ya maisha mazuri ya kizazi kijacho.
Pesa nyingi za Serikali zinaenda kwenye miradi mikubwa kwa ajili ya manufaa ya kizazi kijacho.
Kwa wale wanataaluma ya Financial Management wanakubaliana namni kuwa katika Balance sheet kuna vitu vifuatavyo.
1. Current Assets
2. Current Liabilities
3. Fixed Assets
4. Long term liabilities
5. Owners Equity.
Kitaaluma vipengere hivi ni sawa na kujenga nyumba. Ni lazima viwe na Ratio zake kati ya moja na kingine zinazokubalika kitaaluma. Kimoja kikizidi sana kitaathiri mwingine na balance sheet inaweze ikafa au kushindwa kufanya kazi.
Kwa sasa Kitaifa, pesa nyingi zimehamia kwenye Fixed Assets na long Term loans na kwa hiyo kufanya vitu viwili muhimu katika balance sheet yaani Currrent Assets na Current liabilities (tofauti kati ya vitu hivi viwili huitwa working capital) kusinyaa. Hivi vitu viwili ndiyo vinapima pesa iliyoko kwenye mzunguko.
Wanataaluma husema " Money works". Kama working capital imesinyaa inamaana kazi haziwezi kufanyika.
Kama hakuna pesa kwenye mzunguko fundi ujenzi, mtengeneza magari, mkulima mkubwa, mwenye Hoteli, mwenye hard ware nk hawawezi kufanya kazi.
Ni vyema wataalamu waangalie katika sera za Inchi za fedha ratio hizi zinatakiwa zikaeje.
Imefika wakati she ria za kuweka ratio za Balance sheet ya Taifa ziwekwe kwenye katiba ili kila Raisi ajaye azifuate na si kila moja akiingia madarakani anakuwa na za kwake mfukoni.
Balance sheet ya Taifa ni uhai wa Mwanainchi kwa hiyo hazitakiwi kuchezewa kwa kuweka ratio ambazo zitamwathiri.
Kutufanya sisi wa kizazi hiki tuumie kwa manufaa ya kizazi kijacho ni upuuzi 1ST CLASS,kinachotakiwa ni SUSTAINABLE DEVELOPMENTS na sio story za kutesana.

Watoto wao hao viongozi wakimaliza vyuo ni kupewa kazi za vitengo vinono kwa vimemo tu lkn watoto wa maskini wao ndio utaambiwa wavumlie na blah blah blah kibao,wao na ndg zao msoto wa kufuatilia mafao hawaujui lkn wananchi wa kawaida wakicheleweshewa mafao yao wanaambiwa wavumilie tu ndio uzalendo huo,wao wako ndani ya ma v8 na wana vitega uchumi kibao lkn bado wanazuga eti nao ni wanyonge yaani ni usanii wa hali ya juu.
 
Nadhani hujaelewa mada , umedandia tu.....Sasa ili uielewe haraka , ulizia bei ya hiyo cement huko mwanza kabla hajaingia huyu bwana , alafu linganisha na sasa....wakati huohuo ujue kipato cha mwananchi hakijaongezeka kwa kipindi chote hicho....ukipata jibu rudia tena kwenye bidhaa nyingine kama mchele, sukari,Unga , Maharage, Sabuni, Nondo, Bati, n.k......Paka hapo utakuwa umeelewa mada alafu uchangie sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimekuelewa vizuri sana. Unalalamikia utekelezaji wa hizo unazoita megaprojects. Lakini ni projects ambazo zitaliletea manufaa taifa letu.
 
Nimekaa nakutafakari sana pamoja na kuchambuwa sera na mikakati ya serikali y awamu ya tano ninachokiona huko mbeleni hali ya watanzani kwenye kipato itakuwa mbaya sana jambo pia litasababisha ukosekanaji wa ajira.

Mkuu wa Taifa aka buludoza la mafisadi ataenda pia kuubuludoza uchumi kwakuwa sera zake haziangalii taifa lina hazina kiasi gani na maamuz yake yame elemea zaid kwenye ujenzi wa mager projects jambo ambalo ktk uchumi lina faida za muda mrefu wakati nyuma ukiwaacha watu na umasikini mkubwa na kukosa kaz ktk sector nyingine.

Unapojenga miundo mbinu mikubwa unatengeneza ajira zaid kwa kada fulan kwa wananchi wa sehem fulan. Huwez jenga daraja mwanza ukawafaidisha wana shinyanga lazima ajira zitaenda mwanza zaid kwa mafundi na Eng while wachumi na dk wakiwa hawana ajira au wamechukuliwakidogo.

Sera ya awamo ya Tano itayasinyaisha mabank nakupunguza watu ktk sector hii na sote ni mashahidi vile bank zimefungwa na kuunganishwa while watu wakiachishwakazi ktk kipindi cha kuanzia 2015-2020. Huitaji tochi au mwanga wa juwa kuona Kule tunaelekea na kile kinaenda tokea. Mbaya nikuwa data imekuwa kitu hadim na hili linakuwa msumari wa moto kwenye kidonda.

Wazabun wa serikali wengi wanalipwa mwaka huu tangu mwaka 2015 watu wamedai mpaka wengine umauti umewakuta, hakuna asie juwa ukifanya biashara na serikal unapata faida na pia in create job ila makampuni mengi kwa sasa yameondolew na hayajalipwa pesa zao biashara zimekufa kama uwamini nenda Brela uwauliz Rtn za makampuni mengi kama kwa miaka mitano wameziona? Wengi wamedai mpaka nakampuni wamezifunga.

Biashara ka clearance agency ndio kama imekufa maana serikali imeanzisha chombo , jiulize hizi agency zinaenda wapi? Maelfu Maelfu ajira zimepotea hii sio Afya ni umasikini ktk taifa.

Mifuko ya hifadhi nikweli ilikuwa hoi ila siomifuko yote mfuko kama ppf kabla yakuwa pssf ilikuwa vizuri sana lakini leo unaambiwa wastaafu wanahaha. Kupata mafao yao hivi mtu anafuwatilia mafao yake 2yrs kweli huu niumasikini naukikuwaji wa sheria za kazi. Jambo lakushangaza wanasiasa watalipwa mafao yao haraka wakati mnyonge akihangaikia mafao mpaka anakufa kwa presha.

Ukienda kariakoo utashangaa kuwa Zile biashara tulikuwa kwenye process kuzi rasimisha tupatekodi wengi wamebadilisha mbinu mtu anaona bora aweke mzigo barabarani alipe kitambulisho cha machinga kuliko awe na mlango hili limesababisha kariakoo kuwa soko la wa chuuzi Wala sio soko la kimataifa hii inamanisha nn kwa wachumi? Hii sio ishara nzuri kwa uchumi inamanisha Dalili mbaya kuwa una watu wengi wasiofanya biashara maeneo rasmi. Jambo ni hatari pata picha ya kariakoo 2014 na picha ya 2020.

Idadi ya walio malizachuo na waliopo mtaani inatisha Sina huwakika ikiwa hata theluthi yao wameajiriwa na ukweli ni kwamba hamna ajira tunajenga miundo mbinu hivyo tuna idadi kubwa vijana wasio ajiriwa jambo ni hatari Kule tuendapo.

Mfumo wa Tra ktk sheria ya kodi Tax administration act 2015 from sec 67 and sec68 ni msumari wa moto na kaburi la wafanyabiashara wengi ambao wamejikuta wakiamka masikini. Taifa litakuwa masikini na wananchi watazidi kuwa masikin zaidi kiasi watu watashindwa kununua chupi hasa vijiji, sio kukosa chup ila pia nguo ita kuwa shida why mmebana sana mkasahau pia magendo hupung ukali wa maisha yes taifa hili bado ni changa na yale tunayafanya ktk sera hizi za utawala wa awamo ya Tano kama hatuto angalia vizuri basi hili taifa linarudi pale alipo tuacha Hayati baba wa Taifa.
Nionavyo Mimi DJ atakuwa Raisi Bora sijui kwanini huko nyuma alikuwa anawaachia akina Slaa na Lowasa kugombea
 
Kama wanyonge walishindwa kuwa na maisha mazuri enzi mkwere za kujichotea pesa, tuambie wanawezaje kuwa na maisha mazuri enzi hizi za msukuma ambapo mtu hawezi kuchota pesa?
Kipi Bora sasa. Kipind cha kikwete wachache wanachota na mnyonge hafaidi au kipindi hiki ambacho kweli hali sio nzuri sn kwa maana ya pesa mifukoni mea watu lakini maendeleo ya vitu yanakuja
 
Nimekuelewa vizuri sana. Unalalamikia utekelezaji wa hizo unazoita megaprojects. Lakini ni projects ambazo zitaliletea manufaa taifa letu.
Hv mradi km wa umeme unavyoona hautaleta manufaa kweli? Ilkua ni lazma tutafute uzalishaji wa umeme wa uhakika la sivyo tungenyonywa vibaya sana na haya makampuni ya kitapeli km iptl coz mahitaji ya umeme kila siku yanaongezeka huwezi kubakia na vyanzo vilevile vya uzalishaji wa umeme
 
Hv mradi km wa umeme unavyoona hautaleta manufaa kweli? Ilkua ni lazma tutafute uzalishaji wa umeme wa uhakika la sivyo tungenyonywa vibaya sana na haya makampuni ya kitapeli km iptl coz mahitaji ya umeme kila siku yanaongezeka huwezi kubakia na vyanzo vilevile vya uzalishaji wa umeme
Nafikiri ungemuuliza huyo mleta mada. Yaani megawatts 2100+ hazina manufaa?
 
Uko sahihi kabisa mkuu, hii ni awamu ya ujenzi wa miundombinu mikubwa iwe kwa fedha za ndani au mikopo mikubwa hivyo sera zake zimejikita kwenye matumizi makubwa na walionufaika zaidi ni makampuni makubwa ya ujenzi ya nje ya nchi, hivyo raia watakamuliwa mno ili hii miradi ikamilike na mwishowe nchi itaachwa na madeni makubwa mno mwishoni wa huu utawala wa awamu ya 4.
Ndio sababu iliopunguza mzunguko wa fedha.Kama makandarasi wangekuwa wa ndani pesa ingezunguka ndani.
Ilitakiwa makandarasi yakigeni yalazimishwe kuachia local contractors kazi yenye mapato kwa asilia 50.
 
Kipi Bora sasa. Kipind cha kikwete wachache wanachota na mnyonge hafaidi au kipindi hiki ambacho kweli hali sio nzuri sn kwa maana ya pesa mifukoni mea watu lakini maendeleo ya vitu yanakuja
Kwamba sasa hivi hawa wachache wanaotafuna keki ya Taif
Ndio sababu iliopunguza mzunguko wa fedha.Kama makandarasi wangekuwa wa ndani pesa ingezunguka ndani.
Ilitakiwa makandarasi yakigeni yalazimishwe kuachia local contractors kazi yenye mapato kwa asilia 50.
ni mwendo wa Forced Accounts tu sasa hivi.

Utakubali mziki.
 
Back
Top Bottom