Nionavyo mimi: Miaka kumi ya Rais Magufuli umasikini utaongezeka sana

Nionavyo mimi: Miaka kumi ya Rais Magufuli umasikini utaongezeka sana

Watu tuliishi kwenye maisha yasiyokuwa na uhalisia. Mkwere aliwalambisha asali sahv haipo mnalialia tu. Hebu fikiria watu walivyokuwa wanajichotea pesa za serekali na kufanya maisha yaonekane mepesi kwa watu sahivi mirija ya kijinga imebanwa mnalialia mtandaoni. Ht viwanja ilifikia hatua kwasababu watu wanajiokotea pesa kiholela wananunua hata viwanja mia moja kwa bei kubwa Sasa hapo mnyonge angewezaje hayo maisha. Sasa hv ht heka moja unaipata kwa milioni tatu ndani ya manispaa
Mnyonge gani aliyepata nafuu mwenye hio milioni 3
 
Dah! Sijasoma uchumu lakini ningeambiwa nizungumzie uchumi wa Tanzania ningelizungumza vizuri zaidi yako.
Ni kweli uchumi uko vzr sana mpk wastaafu sasa hivi kila wakiona matangazo ya mifuko ya hifadhi ya jamii kwny TV wanawaombea kwa Mungu sana
Huyo siyo fisadi ni mgombea uraisi mwaka 2015 kwa tiketi ya CHADEMA! Aliyeshindwa kwa sababu kura zake ziliibiwa! Siyo fisadi, maana CHADEMA walimsafisha.
Safi sana kumbe Chadema inamiliki taasisi za uchunguzi wa mambo ya Rushwa/Ufisadi kiasi kwamba ikisema huyu ni fisadi anakua na ikisema huyu ni msafi inakua hivyo.

Asante sana mkuu,umeniongezea jambo kichwani leo.
 
Ni mtz gani unayemzungumzia hapa??-- ni wewe na mimi??!!, very hillarious .

Wewe unamjua kondoo??-- Wtz ni kondoo. Raisi yeyote akishindwa kuitawala Tz, kamwe hawezi kutawala hata serikali ya kijiji katika nchi jirani. Wtz wanaojitambua ni wachache mno.
Ukiweza chunga ng'ombe huwezi shindwa chunga watz
 
Watu tuliishi kwenye maisha yasiyokuwa na uhalisia. Mkwere aliwalambisha asali sahv haipo mnalialia tu. Hebu fikiria watu walivyokuwa wanajichotea pesa za serekali na kufanya maisha yaonekane mepesi kwa watu sahivi mirija ya kijinga imebanwa mnalialia mtandaoni. Ht viwanja ilifikia hatua kwasababu watu wanajiokotea pesa kiholela wananunua hata viwanja mia moja kwa bei kubwa Sasa hapo mnyonge angewezaje hayo maisha. Sasa hv ht heka moja unaipata kwa milioni tatu ndani ya manispaa

Hiyo million tatu unaipata wapi? Au unadhani vitu kuwa bei ya chini ndio kuwa na uwezo wa kuvinunua? Ukiona mtu anajisifia vitu kuwa vya bei ya chini basi ujue huyo mtu ana mitazamo ya kimasikini, na ataishia kuwaweka kwenye umasikini. Mfano halisi ni Nyerere, aliona sifa kutulea kwenye siasa za kutukuza umasikini, akatugeuza masikini zaidi. Matokeo yake Wakenya tuliowaona wanafuata siasa mbaya, wakawa na hali nzuri na kuishia kutucheka. Mchezo huohuo ndio anauleta Magufuli, tena kwa kuwafunika watu na blanketi la wanyonge.
 
Hivi hizi mada zenu mnazokuwa mnaandika , mnafanyaga uchunguzi kabla ya kuandika.
Mimi ni external Auditor haswa kwenye taasisi za kibank.
Ulichokiandika sio kweli kabisa.
Last microfinance niliyo-audit imepata faida ya bilioni 1.3 baada ya kodi ipo maeneo ya Mwenge tu hapo.
Serikali inazilea sana hizi bank maana nyingi hazija-meet requirements za BOT .
Nb:
Mkuu kama unataka kutoka kibiashara hakuna biashara inayolipa fasta kama microfinance. Trust me tena kipindi hiki hìki
cha Magu.
Nimeshindwa kukuambia in-deep kwenye ma-bank , lakini ukiona mpaka bank imefilisika ujue serikali imeisaidia sana ila imeshindikana.
Bank kama _CB ingekuwa nchi serious haitakiwi kuwepo

Sent using Jamii Forums mobile app
Labda umeifanyia hio moja ambao inabebwa na mishahara ya wafanyakazi.
 
U
Hiyo million tatu unaipata wapi? Au unadhani vitu kuwa bei ya chini ndio kuwa na uwezo wa kuvinunua? Ukiona mtu anajisifia vitu kuwa vya bei ya chini basi ujue huyo mtu ana mitazamo ya kimasikini, na ataishia kuwaweka kwenye umasikini. Mfano halisi ni Nyerere, aliona sifa kutulea kwenye siasa za kutukuza umasikini, akatugeuza masikini zaidi. Matokeo yake Wakenya tuliowaona wanafuata siasa mbaya, wakawa na hali nzuri na kuishia kutucheka. Mchezo huohuo ndio anauleta Magufuli, tena kwa kuwafunika watu na blanketi la wanyonge.
Ujamaa ni sumu ya maendeleo
 
Watu tuliishi kwenye maisha yasiyokuwa na uhalisia. Mkwere aliwalambisha asali sahv haipo mnalialia tu. Hebu fikiria watu walivyokuwa wanajichotea pesa za serekali na kufanya maisha yaonekane mepesi kwa watu sahivi mirija ya kijinga imebanwa mnalialia mtandaoni. Ht viwanja ilifikia hatua kwasababu watu wanajiokotea pesa kiholela wananunua hata viwanja mia moja kwa bei kubwa Sasa hapo mnyonge angewezaje hayo maisha. Sasa hv ht heka moja unaipata kwa milioni tatu ndani ya manispaa
Mkuu wewe na mleta mada TumainiEl wote mna hoja za msingi.
Habari ya watu kuishi maisha yasiyo na uhalisia wakati wa JK ni kweli kabisa.
Hoja ya mifuko ya hifadhi ya jamii na usumbufu na mateso wanayo pata wastaafu au watu waliositishiwa ajira ina ukweli kabisa, wastaafu wapo katika mateso makubwa na wengine wanakufa huku wakiwa hawajalipwa na wamedai haki zao kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Tukitaka tuende mbele bila kuumiza sana watu wengi inabidi Mh Raisi Magufuli na washauri wake tuwakumbushe au kuwaonesha mahali gani hawako sahihi au wamejisahau.
Unajua ukiwa kivulini si rahisi kujuwa aliyepo juani anaumia kiasi gani. Watumishi wengi wa umma huko ngazi za juu hawayajui machungu au magumu wanayopitia wastaafu na wahanga wa mambo mengine ya huku chini kabisa mitaani.
Ndiyo maana ni rahisi sana kiongozi au mtu aliyepo kwenye ajira kuongea kauli kama watu waende wakajiajiri kwenye kilimo au wafanye biashara au wakafanye vibarua.
Wenyewe wakitoka kwenye hizo nafasi au wakifilisika wengi wanachanganyikiwa kabisa au wanapata magonjwa ya moyo na kufa haraka.

Kujiajiri bila mtaji siyo kazi rahisi, mtaji wa kuuza maandazi hauwezi kulipia bima ya afya ya angalau mtu mmoja tu kwenye familia, wala mtaji huo hautoshi kwenda kukodi shamba, kununua mbegu, mbolea, na madawa ya kuulia wadudu shambani. Kilimo cha sasa bila madawa (viwatilifu) huwezi kuvuna kitu unapoteza nguvu na muda wako.
 
Yes, wanaonewa kwasababu wanakaa jela zaidi ya miaka mitatu bila kesi kutolewa hukumu, kila siku ushahidi haujakamilika, hii kitu haipo hapa duniani only in Tz, halafu hata hamuoni aibu wala kumuogopa Mungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mungu asaidie kwa kweli akirudi tena kipindi cha pili sikitiko kwa walio mahabusu wataendelea kusota again 5 yrs wakisubiria ushahidi
 
Nimekaa nakutafakari sana pamoja na kuchambuwa sera na mikakati ya serikali y awamu ya tano ninachokiona huko mbeleni hali ya watanzani kwenye kipato itakuwa mbaya sana jambo pia litasababisha ukosekanaji wa ajira.

Mkuu wa Taifa aka buludoza la mafisadi ataenda pia kuubuludoza uchumi kwakuwa sera zake haziangalii taifa lina hazina kiasi gani na maamuz yake yame elemea zaid kwenye ujenzi wa mager projects jambo ambalo ktk uchumi lina faida za muda mrefu wakati nyuma ukiwaacha watu na umasikini mkubwa na kukosa kaz ktk sector nyingine.

Unapojenga miundo mbinu mikubwa unatengeneza ajira zaid kwa kada fulan kwa wananchi wa sehem fulan. Huwez jenga daraja mwanza ukawafaidisha wana shinyanga lazima ajira zitaenda mwanza zaid kwa mafundi na Eng while wachumi na dk wakiwa hawana ajira au wamechukuliwakidogo.

Sera ya awamo ya Tano itayasinyaisha mabank nakupunguza watu ktk sector hii na sote ni mashahidi vile bank zimefungwa na kuunganishwa while watu wakiachishwakazi ktk kipindi cha kuanzia 2015-2020. Huitaji tochi au mwanga wa juwa kuona Kule tunaelekea na kile kinaenda tokea. Mbaya nikuwa data imekuwa kitu hadim na hili linakuwa msumari wa moto kwenye kidonda.

Wazabun wa serikali wengi wanalipwa mwaka huu tangu mwaka 2015 watu wamedai mpaka wengine umauti umewakuta, hakuna asie juwa ukifanya biashara na serikal unapata faida na pia in create job ila makampuni mengi kwa sasa yameondolew na hayajalipwa pesa zao biashara zimekufa kama uwamini nenda Brela uwauliz Rtn za makampuni mengi kama kwa miaka mitano wameziona? Wengi wamedai mpaka nakampuni wamezifunga.

Biashara ka clearance agency ndio kama imekufa maana serikali imeanzisha chombo , jiulize hizi agency zinaenda wapi? Maelfu Maelfu ajira zimepotea hii sio Afya ni umasikini ktk taifa.

Mifuko ya hifadhi nikweli ilikuwa hoi ila siomifuko yote mfuko kama ppf kabla yakuwa pssf ilikuwa vizuri sana lakini leo unaambiwa wastaafu wanahaha. Kupata mafao yao hivi mtu anafuwatilia mafao yake 2yrs kweli huu niumasikini naukikuwaji wa sheria za kazi. Jambo lakushangaza wanasiasa watalipwa mafao yao haraka wakati mnyonge akihangaikia mafao mpaka anakufa kwa presha.

Ukienda kariakoo utashangaa kuwa Zile biashara tulikuwa kwenye process kuzi rasimisha tupatekodi wengi wamebadilisha mbinu mtu anaona bora aweke mzigo barabarani alipe kitambulisho cha machinga kuliko awe na mlango hili limesababisha kariakoo kuwa soko la wa chuuzi Wala sio soko la kimataifa hii inamanisha nn kwa wachumi? Hii sio ishara nzuri kwa uchumi inamanisha Dalili mbaya kuwa una watu wengi wasiofanya biashara maeneo rasmi. Jambo ni hatari pata picha ya kariakoo 2014 na picha ya 2020.

Idadi ya walio malizachuo na waliopo mtaani inatisha Sina huwakika ikiwa hata theluthi yao wameajiriwa na ukweli ni kwamba hamna ajira tunajenga miundo mbinu hivyo tuna idadi kubwa vijana wasio ajiriwa jambo ni hatari Kule tuendapo.

Mfumo wa Tra ktk sheria ya kodi Tax administration act 2015 from sec 67 and sec68 ni msumari wa moto na kaburi la wafanyabiashara wengi ambao wamejikuta wakiamka masikini. Taifa litakuwa masikini na wananchi watazidi kuwa masikin zaidi kiasi watu watashindwa kununua chupi hasa vijiji, sio kukosa chup ila pia nguo ita kuwa shida why mmebana sana mkasahau pia magendo hupung ukali wa maisha yes taifa hili bado ni changa na yale tunayafanya ktk sera hizi za utawala wa awamo ya Tano kama hatuto angalia vizuri basi hili taifa linarudi pale alipo tuacha Hayati baba wa Taifa.
Stupid idea...jomba wewwe una elimu gani mzee...labda tuanzie hapo...au wewwe ni wale wazee wa elimu ya hapa na pale..unatoa hoja hujui hata reserve ya serikali ni kiasi gani, GDP ikoje, inflation iliyopo na forecast yake, productivity ikoje, market environment ikoje import na export na variable nyingine tele..embu tuambie una elimu gani
 
Nyie chadema mnaongozwa na viongozi vilaza sana ndio tatzo. Mahakama ya mafisadi ya nn wakati mafisadi mlishawasafisha jukwaani. Haiwezekani mumtaje mtu ni fisadi kwa zaidi ya miaka kumi alafu kakatwa kwenye chama cha ccm eti nyie mnamuokota na kumsafisha tena na kumpa nafasi ya kugombea uongozi[emoji23][emoji23][emoji23]bure kabisa nyie. Inamaana hamna hata mikakati ya kuandaa viongozi wenu
Kwa hiyo fisadi ni EL peke yake tuu? Maana ndiye "aliyesafishwa" na Chadema!!
Mahakama imeanzishwa baada ya EL "kusafishwa" na Chadema. Kwa nini ikianzishwa ilhali fisadi kasafishwa!? Je,hayo si matumizi mabaya ya fedha,muda,madaraka na akili?
 
Zamani Wakoloni walipotaka kufanya uwekezaji mkubwa walikuwa wanatumia watumwa.
Sasa hivi sera za kuwafanyisha kazi watu kama watumwa hakuna.
Sisi kizazi hiki lazima tuwe kondoo wa kafara kwa ajili ya maisha mazuri ya kizazi kijacho.
Pesa nyingi za Serikali zinaenda kwenye miradi mikubwa kwa ajili ya manufaa ya kizazi kijacho.
Kwa wale wanataaluma ya Financial Management wanakubaliana namni kuwa katika Balance sheet kuna vitu vifuatavyo.
1. Current Assets
2. Current Liabilities
3. Fixed Assets
4. Long term liabilities
5. Owners Equity.
Kitaaluma vipengere hivi ni sawa na kujenga nyumba. Ni lazima viwe na Ratio zake kati ya moja na kingine zinazokubalika kitaaluma. Kimoja kikizidi sana kitaathiri mwingine na balance sheet inaweze ikafa au kushindwa kufanya kazi.
Kwa sasa Kitaifa, pesa nyingi zimehamia kwenye Fixed Assets na long Term loans na kwa hiyo kufanya vitu viwili muhimu katika balance sheet yaani Currrent Assets na Current liabilities (tofauti kati ya vitu hivi viwili huitwa working capital) kusinyaa. Hivi vitu viwili ndiyo vinapima pesa iliyoko kwenye mzunguko.
Wanataaluma husema " Money works". Kama working capital imesinyaa inamaana kazi haziwezi kufanyika.
Kama hakuna pesa kwenye mzunguko fundi ujenzi, mtengeneza magari, mkulima mkubwa, mwenye Hoteli, mwenye hard ware nk hawawezi kufanya kazi.
Ni vyema wataalamu waangalie katika sera za Inchi za fedha ratio hizi zinatakiwa zikaeje.
Imefika wakati she ria za kuweka ratio za Balance sheet ya Taifa ziwekwe kwenye katiba ili kila Raisi ajaye azifuate na si kila moja akiingia madarakani anakuwa na za kwake mfukoni.
Balance sheet ya Taifa ni uhai wa Mwanainchi kwa hiyo hazitakiwi kuchezewa kwa kuweka ratio ambazo zitamwathiri.
 
Stupid idea...jomba wewwe una elimu gani mzee...labda tuanzie hapo...au wewwe ni wale wazee wa elimu ya hapa na pale..unatoa hoja hujui hata reserve ya serikali ni kiasi gani, GDP ikoje, inflation iliyopo na forecast yake, productivity ikoje, market environment ikoje import na export na variable nyingine tele..embu tuambie una elimu gani
Hivyo vyote ulivyovitaja wasomi wa awamu hii vyote wanavijua na vimewasaidia sana kuweza kulipa mafao ya wastaafu kwa haraka sana,hongereni sana wastaafu wanawapenda sana.
 
Kwa hiyo fisadi ni EL peke yake tuu? Maana ndiye "aliyesafishwa" na Chadema!!
Mahakama imeanzishwa baada ya EL "kusafishwa" na Chadema. Kwa nini ikianzishwa ilhali fisadi kasafishwa!? Je,hayo si matumizi mabaya ya fedha,muda,madaraka na akili?
Mafisadi siwalikiri wakarudisha pesa au nyie mlitakaje
 
Back
Top Bottom