Mtoto wa Shule
JF-Expert Member
- Nov 16, 2014
- 21,572
- 15,610
Dah! Sijasoma uchumu lakini ningeambiwa nizungumzie uchumi wa Tanzania ningelizungumza vizuri zaidi yako.Nimekaa nakutafakari sana pamoja na kuchambuwa sera na mikakati ya serikali y awamu ya tano ninachokiona huko mbeleni hali ya watanzani kwenye kipato itakuwa mbaya sana jambo pia litasababisha ukosekanaji wa ajira.
Mkuu wa Taifa aka buludoza la mafisadi ataenda pia kuubuludoza uchumi kwakuwa sera zake haziangalii taifa lina hazina kiasi gani na maamuz yake yame elemea zaid kwenye ujenzi wa mager projects jambo ambalo ktk uchumi lina faida za muda mrefu wakati nyuma ukiwaacha watu na umasikini mkubwa na kukosa kaz ktk sector nyingine.
Unapojenga miundo mbinu mikubwa unatengeneza ajira zaid kwa kada fulan kwa wananchi wa sehem fulan. Huwez jenga daraja mwanza ukawafaidisha wana shinyanga lazima ajira zitaenda mwanza zaid kwa mafundi na Eng while wachumi na dk wakiwa hawana ajira au wamechukuliwakidogo.
Sera ya awamo ya Tano itayasinyaisha mabank nakupunguza watu ktk sector hii na sote ni mashahidi vile bank zimefungwa na kuunganishwa while watu wakiachishwakazi ktk kipindi cha kuanzia 2015-2020. Huitaji tochi au mwanga wa juwa kuona Kule tunaelekea na kile kinaenda tokea. Mbaya nikuwa data imekuwa kitu hadim na hili linakuwa msumari wa moto kwenye kidonda.
Ukienda kariakoo utashangaa kuwa Zile biashara tulikuwa kwenye process kuzi rasimisha tupatekodi wengi wamebadilisha mbinu mtu anaona bora aweke mzigo barabarani alipe kitambulisho cha machinga kuliko awe na mlango hili limesababisha kariakoo kuwa soko la wa chuuzi Wala sio soko la kimataifa hii inamanisha nn kwa wachumi? Hii sio ishara nzuri kwa uchumi inamanisha Dalili mbaya kuwa una watu wengi wasiofanya biashara maeneo rasmi. Jambo ni hatari pata picha ya kariakoo 2014 na picha ya 2020.
Idadi ya walio malizachuo na waliopo mtaani inatisha Sina huwakika ikiwa hata theluthi yao wameajiriwa na ukweli ni kwamba hamna ajira tunajenga miundo mbinu hivyo tuna idadi kubwa vijana wasio ajiriwa jambo ni hatari Kule tuendapo.
Mfumo wa Tra ktk sheria ya kodi Tax administration act 2015 from sec 67 and sec68 ni msumari wa moto na kaburi la wafanyabiashara wengi ambao wamejikuta wakiamka masikini. Taifa litakuwa masikin kama sera hizi hazito angaliwa upya