Nionavyo mimi ni uzushi wa Marekani kudai China ina bidhaa feki

Nionavyo mimi ni uzushi wa Marekani kudai China ina bidhaa feki

MTV MBONGO

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2016
Posts
1,288
Reaction score
1,262
Karibu kila Bidhaa mbovu utasikia imetoka China, 'cha Mchina hicho'. Mbona kwao huko China na Ulaya bidhaa za Kichina ni bora kuliko Maelezo?

Ukifuatilia bifu nyingi za kibiashara baina ya mataifa haya mawili utagundua kuwa MADAI YA BIDHAA FEKI TOKA UCHINA, ni UZUSHI wa Marekani na washirika wao wa Kimagharibi.

Tusiache kujiongeza tunapofanya maamuzi ktk manunuzi ya bidhaa
 
😂😂😂😂😂 hawakurupuki Mkuu ni ukweli MTUPU. Nguo, viatu, handbags za akina mama za makampuni ya Kimarekani jamaa wanaiga na kuziuza katika nchi mbali mbali duniani ikiwemo USA lakini quality ya hivyo vitu ni ndogo ukilinganisha na original hivyo ni lazima waanikwe hadharani japo kuna soko kwani huwa ni bei chini mno ukilinganisha na original.
 
China hawatengenezi bidhaa feki bali wnatengeneza bidhaa kulingana na bei ya mhitaji
 
TBS za wenzetu huwezi ukaingiza hata sindano feki.

Wenzetu wana-mantain standard. Wao ni matajiri.

Kwa hiyo kanuni yao ni: " You buy it or leave it"

Mchina anakutengenezea kitu kulingana na hela yako (hata barabara), Mmarekani hana hiyo tabia

Tairi moja la katapila la Mmarekani ni IST 10
 
(made in china) siamini chochote kabisa hapo mchina ni fekifekifekiiiiiii hadi watu ni feki kifupi tu mchina anaingiza hela kiujanjaujanja!
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hawakurupuki Mkuu ni ukweli MTUPU. Nguo, viatu, handbags za akina mama za makampuni ya Kimarekani jamaa wanaiga na kuziuza katika nchi mbali mbali duniani ikiwemo USA lakini quality ya hivyo vitu ni ndogo ukilinganisha na original hivyo ni lazima waanikwe hadharani japo kuna soko kwani huwa ni bei chini mno ukilinganisha na original.

Muulize tu kuwa mara ngapi hapa Bongo Wachina wamedakwa na viwanda bubu vya kutengeneza vitu mbali mbali mpaka vinywaji

ASingie you tube akutane na kesi za wachina kufungua viwanda bubu vya vyumban kwenye nchi za Afrika wanazohamia.

Wachina wako proactive kwenye kutafuta pesa sema hawajali usalama wa mlaji wala mfanyakaz so kwao ubora sio issue swala ni kuweza kuipata hata ile sumni ya maskini wa mwisho

Ila wanauweza wa kutengeneza bidhaa bora maradufu, ndo maana Ulaya zinaenda bidhaa bora tu ila huku wanaharibu brand kwa kutuletea fake.
 
Zipo bidhaa feki nyingi sana kutoka uchina huo ndio ukweli tuache kuwatetea, kiukweli kabisa hawa jamaa wanaiharibu sana dunia kwa kutengeneza bidhaa nyingi za hovyo na copy feki ya bidhaa nyingi original from europe.
 
Kama tungeendelea kutumia/kuhitaji original made from Europe kwa 90% tungeendelea mpaka sasa kutumia mitumba mpaka machupi na masidiria. Ashukuriwe Mchina japo ndo hvyo tena nyingi hazidumu
 
Mpaka leo wengi Flat TV tungezisikia kwenye bomba,tungeendelea na maTV chogo yetu maana TV 32inch tu inafika mpaka million KWA brand za kutoka europe
 
Back
Top Bottom