Nionavyo Udhaifu wa Operesheni Sangara

Monoko Mushi,

Umeulizia kuhusu ni vipi tunaweza kuwaambia wananchi kuwa viongozi walioko ndio tatizo.

Hatuna ushahidi wa Viongozi kuwa mafisadi, lakini tuna Ushahidi wa wao kuwa wazembe na matunda ya uzembe wao.

HIvyo ni rahisi kuwafikia Wananchi katika vita vya Ufisadi kwa kwanza kuonyesha Uzembe wa Viongozi hawa na kisha wakishaondolewa na kuaibishwa, ndipo nguvu mpya iingie na kutumia sheria zilizopo au kuongeza sheria nyingine kubainisha Ufisadi wa Viongozi hawa.na kuwafunga.

Kwenda kuwahoji viongozi na wabunge wa CCM kuhusiana na walichofanya na kupima ufanisi waa na uwezo wa kiutendaji kuleta maendeleo na kupiga vita Ujnga, Umasikini na Maradhi ndio njia pekee ya kuwaangusha na kuwaondoa kwenye nafasi za kushikilia na kuiongoza Serikali yetu.

Ushahidi wa kuwaonyesha Watanzania kuwa shida na tabu katika maisha yao na kukwama kwao kupiga hatua kuondokana na umasikini upo tena mwingi sana.

Nenda kijijini Maswa umuulize Msukuma kwa nini bado anakwenda mtoni au bwawani kuteka maji na amekuwa akiahidiwa maji safi kwa miaka 30 iliyopita? Ukimuonyesha Msukuma huyu udhaifu wa kiuongozi na kukosekana mwamko wa kiongozi huyu kumletea Msukuma maendeleo na ukamuonyesha ni jinsi gani wewe utayaleta maendeleo haya, basi ni wazi kwa kiasi fulani Msukuma atakuelewa maana umeoanisha hali yake halisi na kumwonyesha ni jinsi gani Mbunge wake amekuwa akitoa ahadi hewa.

Naomba usichukulie kuwa natangazia umma kuwa hakuna haja ya kupiga vita ufisadi. La hasha, bali ni ukweli dhahiri kuwa Vita vya Ufisadi havitafanikiwa kama hakutakuwa na mabadiliko ya Uongozi na kuanza kutumika kwa Sheria au kuboresha sheria dhaifu. Aidha wananchi wengi hawaelewi chochote kuhusu EPA au Richmond kwa kuwa hata bila hujuma hizo mbili, wao bado wamekuwa wakitaabika.

Sasa ukitaka wafikia Wananchi, basi waonyeshe kile ambacho wanakiona kwa macho yao kila siku.

Ni kweli fedha za EPA zingesaidia kuleta maendeleo fulani, lakini je tatizo ni fedha?

Leo ukiwaambia Wananchi kuwa bajeti na fungu la bajeti iliyopaswa kuleta Hospitali au kujenga barabara, Uongozi wa Wilaya umezitumia visivyo, ni rahisi kwa wao kuelewa kuliko kuanza kuwaelezea kuhusu EPA.

Kwanza tukianza kuwaambia Wananchi kuhusu EPA na kusema pesa zimeibiwa, ni rahisi wao kutupuuzia maana kila siku kauli wanazozisikia kutoka kwa Viongozi ni kuwa Tanzania haina pesa na wameshawishika vizuri kuamini kuwa hakuna fedha.

Ndio maana unakuta wanashangilia pale mtu anapokuja na kudai ati ana Wafadhili au marafiki ulaya ambao watatuletea misaada. Hii ni kutokana na wao kuamini Tanzania haina uwezo na Serikali yao bado inajaribu kujikwamua tangu tamko la Mwalimu Nyerere baada ya vita vya kagera aliposema tujifunge mkanda!
 
Monoko Mushi,

Mfumo bora ni mfumo shirikishi, mfumo huru wenye kutoa usawa na haki na zaidi kuwajenga wananchi kuwa huru na kuishi katika Demokrasi ya kweli.

Kilichofanyika Zanzibar 1992 ni mazingaombwe ambayo yaliishia kujaza maduka bidhaa za kuagiza na kuanzishwa kwa mfumo butu wa kisiasa.

Katiba haikubadilishwa, Sheri ahazikubadilishwa na bado CCM inaendelea kuongoza eti katika mfumo wa Vyama vingi lakini Katiba, Sheria na mengine mengi ni ya mfumo wa zamani uliokuwa ni wa Ki-TANU na CCM.

Ndio maana leo hii TISS wanahangaika kwa vitu vidogo visivyo na maana, lakini vile vya msingi hawavioni, tatizo ni mfumo tulionao.

Leo hii walioko CCM wanajifanyia wanachotaka, hakuna wa kuwashikisha adabu. Wakivunja sheria, wanaogopewa kwa kuwa Polisi na Mahakama bado zinatawaliwa na kuongozwa kutoka mfumo wa awali na katiba inayovifunga vyombo hivi.

Hata Bunge, linapaswa kuwa lenye nguvu huru, lakini kwa kuwa CCM haijiamini na wana wasiwasi kila siku, basi kudhibiti hata mapinduzi ndani ya Chama kutoka kwa Wabunge wake, wameendeleza mfumu butu ambao wabunge ni kama galasa kwenye karata!

Tukibadilisha mfumo tutapata nafasi mpya na kuvua zile nguvu za mabavu za CCM na wateule wake wanaojiona wako juu ya sheria.
 

Mkuu mwanawasu,

Wataalamu wanaiita ni technical mistake ,kutaka kujaribu uongozi, ni makosa ambayo hayatakiwi kutokea na yakitokea mara nyingi ni kupromoka kwa taifa.

Mambo kama haya yanahitaji analysis ya kutosha na kupata kujiridhisha kwa asilimia kubwa. Mambo haya sio biashara za ukwaju.

Ni kosa kubwa mno kuwachukuwa wanajeshi na kuwapeleka vitani bila kutambuwa uwezo wao eti wakishindwa watauwawa na nitapeleka wengine. Na ni kosa kubwa mno kwenda kupigana vita yumkini ukitambua vita hiyo kwa vyovyote hutoshinda.
 
tatizo la umaskini wa Tanzania ni nini? jibu lako ni Nyerere.

Umetowa swali na ukalijibu mwenyewe, mimi sijajibu bado.

Kuna matatizo mengi yanayochangia. Kifupi

1.Mentality ya watanzania tuliyonayo. Ukiona kampuni ya mzungu iko kwetu wafanyakazi wanaikimbilia na kusema huko hakuna longolongo si kwamba wanakuwa wamekurupuka siku moja tu. Ama ukiona taasisi zina mwamini mzungu na kuacha mzawa jamii haikurupuki siku moja ku-conclude vile.

2.Nyerere sera yake wenda ilikuwa nzuri sana, lakini alikurupuka kuimplenti bila kufanya analysis ya kutosha ktk mazingira sahihi na ndiyo matokeo yake haikuwaingia wananchi na kuivalia ngozi ya kondoo alipokuwa kiongozi na alipotoka wakaibwaga.Hii nayo ina effect kubwa mno tena mno.Kwa kuthibitisha hilo wafanyakazi karibu wote wa serikali na wachama wamefanya kazi na Nyerere, sasa kwanini ndivyo sivyo.

Nyerere mwenye alikili kwamba sera yake haikuwaingia wananchi, naamini sera hiyo ilikuwa nzuri sasa kwanini wananchi haikuwaingia.? napo hapo unaweza pata chazo cha umasikini wetu.

Binafsi mambo haya yanamlolongo mrefuuuuu ambao unahitaji kuutafuta huko na kutibu.
Nimeona tofauti hata ya waganga wa hasa europe na wa kwetu, wakwetu ukienda unamwambia unaumwa kichwa anakutwanga klorokwini na asprini, lakini ha wa europe hakupi klorokwini mpaka ajue sababu ya kichwa kuuma.
 
Kuna haja ya kuweka mikutano kwenye YOUTUBE ili watu wasikie au sisi kama wadau wa JF tunaweza kufanya hivyo maana leo mambo mengi sana Chadema walisema na CCM walifanya hivyo na pia kuna sera nyingi sana ambazo CCM walikuwa wanaiga toka CHADEMA

Hii kuiga iga ndiyo itaifanya CCM itawale milele!


Watanzania tunapenda majibu rahisi na ya mkato sana.

.

Umejua lini hilo mkuu? ulichosema ni dhahiri, KUMBKENI nchi hii ufisadi uko kila kona, itakuwa kazi sana kuamini chama chochote cha upinzani au tawala. Kuzuia hilo vyma vyote viunde serikali na sio kudanganyana hapa miaka nenda rudi, na kufanya upinzani another way ya watu kupata ajira!



. Umasikini wetu unatokana na uongozi na uongozi mbovu ni zao la ufisadi na chama kinachotoa viongozi hao ni cha kifisadi pia, alamsiki.

What is your solution Mzee Mag3, kuiondoa CCM? na je tukiwapa chadema una hakika gani baada ya miaka miwili hatutaanza kujaza article tena humu za kulaumu yale yale.

Ufisadi pia kama ulivyosema una definition nyingi, je huoni kama Chadema wana fisadi mawazo ya watu kwa kuwapa matumaini yasiyo kuwepo! Yaani nini matumaini au tegemeo la vyama vya upinzani nchi hii kama tuasipokaa chini na kujenga nchi kwanza?

Huwa ninajiuliza iwe vipi tukubaliane kuwa tatizo ni uongozi halafu solutions za tatizo hilo ziwe tofauti na uongozi?Kuna mwenye kujuwa ni kwanini?

.

Mimi najua Mushi ni kwanini!!, yaani kuondoa uongozi m'bovu Tanzania siyo solution, solution ni kuandaa mazingira ya kuzuia viongozi wabovu!

Kama unakubali hapo basi swala la kwanza kabisa ni vyama, wanayharakati , wananchi n.k kuwaza mabadiliko ya katiba.

JMushi, watanzania hawa wameanza kuiba tangu enzi hizo, za maduka ya ushirika mkuu!

OS na harakati zingine zinafanyika kama kila kitu kiko shwari, hakuna ushwari, hakuna msingi ya taifa hili, hakuna kinachoeleweka , why one earth people are doing things as if we are OK?

Hivi leo kuna ubaya gani kusema wapinzani anzeni kwanza mabadiliko ya katiba? ili kuzuia chama kimoja kuongoza nchi hii,

hawa wapinzani ni akina nani leo hii watasema ni wasafi wakaaminika?
 

Japo umenikoti kila mahala, mie nitajitahidi kujibu kifupi.

serikali ni pamoja na wananchi, hivyo vita dhidi ya ufisadi ni jukumu la kila mwananchi. Huwezi linda mali yako kwako wakati unategemea hao unaowazuia wasikuchukulie mali zako uwategemee .

Wakati wa Nyerere ni % ilikuwa inaingia shule? ama kwa vile walikuwa wanaingia walikuwa wanasoma bure?? siamini hilo kama mlisoma sana wakati na kama mlisoma sana mgenkuwa tayari mmeshachukuwa njia sahihi kuliokoa taifa hili.

Labda enzi hizo UFISADI lilikuwa moja ya somo, maana watanzania mafisadi wote wamesoma wakati huo.
 
tatizo la umaskini wa Tanzania ni nini? jibu lako ni Nyerere.

MKJJ, Nyerere tunampenda lakini kama tukianza kulaumu waliotufikisha hapa tulipo Nyerere hakwepi na wengine wanaofuata.

Criticaly hata kama tunamtetea swala lake la kuleta chama kimoja nchi iliyokuwa na vyama vingi halitaweza kusahaulika kamwe.

Hali kadhalika tukisema viko vya kumsifia Nyerere pia havitakosekana viko vingi mno! Japo kwa kila utakachomsifia hutakosa criticism na kila utakachomlaumu huwa hakina utetezi concrete!

Leo hii japo tuna wazee wengi wanaolilia Nyerere wengi mentality zao si za ki-demokrasia ni kuwaza CCM.

So JKN tukisema tuanze kuanika yote negative tutajaza threads, na tukisema mazuri tutajaza pia.

Nyerere asiwe anatajwa jamani , mnaomtetea mtakosa raha kabisa na mnaomchukia mtakosa raha

Lets discuss now OS, na nchi yetu!
 

Ni kweli tupu.
1.kama sijakosea mashirika ya umma waliyafilisi nafikiri mwishoni mwa enzi za Nyerere na kati ya Mwinyi. Hapa nataka kusema huu ujanjanja wa watanzania ndio tatizo sugu.Watanzania ni wajanja wajanja fulani.

2.Angalia matukio, yanayotokea mfano limwanaume kubaka katoto, ama mijibaba kumfukuzia mkono wa albino ama mijamaa kumkatakata mapanga bibi eti kwa vile ana macho mekundu, sasa bibi atakosa je macho makundi wakati anatumia magunzi ya mahindi kama kuni??

Ukichukulia matukio ya na namna hiyo, unaona kabisa kuna tatizo kubwa sana si tu la kioungozi linaenda mbali sana.
 
Kwanza CHADEMA hongereni kwa Operation Sangara.................nimeshuhudia mwenyewe kuwa hii inawanyima majambazi CCM usingizi

Pili, nakupongeza Mh Dr. Slaa kw ajuhudi zako za kuelimisha umma wa Watanzania kuhusu mustakabali wa Taifa letu

Tatu nampongeza Rev na wachangiaji wa hii mada............

Matatizo ya nchi yetu yanajulikana
1. Uongozi
2. Katiba
3. Elimu ya uraia

Katika kushughulikia hayo matatizo hapo juu kuna mambo ya msingi inabidi yafanyike.........mojawapo ni kampeni kama OS ili kuwaelimisha wananchi kuhusu haki zao za kimsingi na kwenye uchaguzi...............mambo kuchagua picha/jina ni upuuzi ambao bado wananchi wanauendekeza..................
 

Hayo matatizo hayatatuliwi na chadema peke yake, watanzania bila kujali nani wanahitajika kutatua, CCM ndio wa kwanza kuyajua matatizo na kuyatatua!

Ogah, kama ulivyosema bila mabadiliko ya katiba hakuna tutakachofanikiwa, we can talk and talk and talk....

1. Kumbuka kuwa wabunge wengi hupata hizo nafasi kwa nguvu tu ya wananchi wa mahali hapo, hata huyo mbunge akiwa fisadi huku DSM kwao wakimkubali huwezi kumtoa! this is hard to swallow, ila watanzania hawa wanafanya hayo! nadhani unajua waliobebwa na wananchi kwa kutuhumiwa mafisadi. Mtu akipendwa jimboni ndiyo bai ameshashinda

2. Kumbuka mpaka leo hii, CCM hawajatumia RUNGU la kuiba kura! hakuna uthibitisho wa CCM kuiba kura kwenye majimbo, CCM wanashinda kihalali! na ndiyo maana vyama havina mpango wa kudai tume ya uchaguzi ibadilishwe.

Operation SANGARA ikiwezeshwa na kila mtanzania akawa tayari kuipigia kura chadema ishinde, then nguvu ya tume ndiyo itaonekana dhahiri that time tume ya uchaguzi ndiyo wataamua matokeo ya ajabu ili CCM wawe kwenye madaraka!


Kuna kila sababu ya kuamini kuwa vyama havina dira, havina malengo , wanasubiri bahati au mchezo wa sandakarawe amina!

Ni ufisadi na ku-miss use intelectual power kama leo tusipojadili ujenzi wa taifa, taifa la Tanzania halipo bado kama wananchi wote hawatakuwa katika serikali yao kutokana na itikdai zao. Leo tuna CCM tu!

Tutafika miaka 50 ijayo still watu watakuwa na imani na vyama? CCM haitaondoka madarakani piga ua! ufisadi halisi ni kutofanya zuri unalotakiwa kufanya. Vyama hivi vinaudanganya ulimwengu kuwa vitaiondoa CCM from no where! WAASISI wa upinzani walikosea kutotaka mabadiliko ya katiba na kudai serikali ya mseto, leo miaka baada ya 20 tunabaki kama living proof! tuna ushahidi wa kuwa walikosea. Watu badala ya kukaa chini na kugundua tumekosea wapi wanazika ukweli na kuendesha operation Sangara. Operation Sangara ni nzuri tena sana, ila sio muda wake huu!

Narudia najua inauma NCHI HII SIYO YA CCM wala haitakuwa ya chama chochote kile, we need government ambayo vyama vyote vitaingia kulingana na asilimia ya kura zao, hapa kwa namna moja tutapunguza sana ufisadi na kuleta efficiency serikalini. Thinking ya leaders itaongezeka, uzalendo utaongezeka, ukweli utaiongezeka, professional zitakua! KIKUBWA hatutatoka jasho na operation sangara na baada ya uchaguzi tunaumwa makoo!

Kuwaza leo CCM iondoke ije chadema, chadema wakikosea waje, NCCR then sijuia nani tutashangaa next century Tanzania bado inabaki ile ile ya watanzania, Tanzania halisi inakuwa ya wageni tu! tutatawaliwa na nguvu za globalisation, WB, IMF na simply kwa sababu ya viongozi dhaifu, kasi ya dunia kamwe haitatusubiri watanzania..

OS ni ufisadi tea mkubwa kabisa, siwezi nikawaza kuindia CCM A na kuleta CCM B! nitawaza kundoa negative issue za vyama vyote na kujenaga taifa imara. Ukweli huu SLAA anaujua, kama hawafanyi sawa na ukweli huu kinachoendelea ni nini?? siyo kuwadanganya watanzania, it is not fair kwa chadema yenyewe kutoa jasho wasilokula!

We need your brainy in the government! mkifika huko propose education system ibadilike, propose mitaal ibadilike n.k ,MASWALI HAYO YA REV. YANAJIBIKA VIZURI KWA MTU YEYTOE MWENYE COMMON SENSE, which I think we have it 'somewhere'!

Narudia OS ni ufisadi wa fikra! ni kubemendana TANZANIA halisi haijazaliwa. WE need President Chadema, PM CUF, Waziri a Ulinzi CCM n.k , what are waiting for why wasting time doing things that will not lead us anyhwere???

kusema tumesema sana, tumesema miaka hii minne kuliko kipindi chochote cha historia yetu, YET..GUESS WHAT?? CCM will still be in the power even more!
 

Waberoya unachosema ni kweli,na pia niko aware kuwa walianza kuiba toka zama za vyama vya ushirika,hata hivyo bado sheria zilikuwa zikiwabana lakini tatizo ni hatua za kisheria kutokuchukuliwa dhidi yao,na hapo basi tunarudi pale pale kwenye uongozi mbovu usiofuata sheria na hata katiba iliyopo,kwasababu ni uongozi mbovu umehalalisha wizi,yani kugeuza sheria za kuwabana kuiba na sasa wanaiba kiwazi wazi......Hivyo haijalishi,kama una uongozi mbovu wa mafisadi wataibadilisha hiyo katiba yako in wink of an eye!

Kuhusiana na issue ya mabadiliko ya katiba hilo ni vyema lakini ni tofauti na pointi yangu,mabadiliko ya katiba yataimarisha demokrasia na hivyo tutaweza kupata mwanya wa kuwabadilisha kwa urahisi wakionyesha kuwa na nia mbaya,huwezi kujua nia ya kiongozi kabla hujaona matendo yake au matokeo ya uongozi wake,na haitajalisha kama katiba hiyo imetoka mbinguni,uongozi makini ni first,uongozi mbaya utabadilisha sheria nzuri na kuziweka zile mbaya,hayo yako wazi mkuu!Sheria nzuri na hata katiba hubadilishwa na viongozi wabaya,ni lazima kwanza tujuwe wapi haswa tumekwama if we're to move forward.

Kusema bluntly kwamba ku uondoa uongozi mbovu siyo solution,hapo napingana kabisa na wewe,kama nilivyomwambia Rev Kishoka hapo nyuma,tunaweza ku compromise na kukubaliana kuwa tunahitaji vyote kwa pamoja,yani mabadiliko ya katiba na kuwaondoa viongozi mafisadi,binafsi naamini base on the situation we're in together with other factors,ninaweza kuchagua tuanze kuwaondoa kwanza viongozi mafisadi ndipo tujadili katiba yetu mpya sasa kuwa which direction we should take!
 
Watanzania,

Msisahau kuwa Ufisadi ni mfumo ulioshamiri katika jamii nzima Tanzania na si watu wawili au watatu!

Tofoauti ni viwango vya Ufisadi.

Kama hatuwezi kulitambua hili, na kuanza kulifanyia masahihisho ni vigumu kuondoa Ufisadi Tanzania.

Leo ukikamatwa na Trafiki, unamwachia kidogodogo, huo ni Ufisadi uliofanywa na wote nyie wawili. Ukienda Ardhi unatoa kidogodogo upewe hati, kutoa kwako rushwa na yule anayepokea rushwa ni Ufisadi.

Ukianza kwenda vijijini na kuanza kutumia umashuhuri na kukusanya zawadi, huo ni Ufisadi, hata kama utaita ni takrima au Ukarimu wa Kitanzania, lengo na nia ya kupewa kale kambuzi si nzuri bali ni Ufisadi.

Unapotoa pampu za maji, magari ya wagonjwa au kukimbilia wafadhili kuleta misaada na wewe kuringia wanajimbo kuwa ni wewe pekee unastahili kutokana na misada uliyoleta na kisha wananchi hao wakakupa kura kwa ajili ya misaada hiyo wewe na wananchi wote ni mafisadi.

Ufisadi una eneo na maan akubwa sana zaidi ya kuhujumu BOT au Richmond.

Jibu la kuondoa Ufisadi linaanza na Uongozi, kuwa na uongozi imara na bora, utakaosimamia haki na sheria, utakao tii haki na sheria na utakaoleta mstuko kwa Raia na raia wakajirusi na kuacha kufanya na kutukuza vitendo vya KIFISADI!
 
 
 
Rev. Kishoka.

Kufanya mabadiliko kule chini sio kazi rahisi kama ambavyo mtu unaweza kuona ukipita.

Operation Sangara ni hatua ya kwenda huko chini na kweli si kazi rahisi . Mafanikio ya CCM ni matunda ya kazi iliyoanza 1954 miaka 55 leo wameweza kuwa na kiongozi katika kila nyumba 10 nchini kote. Chadema ilianza kuimarika ktk maeneo machache tangu awamu ya uongozi wa kwanza hadi huu watatu yapo mabadiliko makubwa chama kimefika tkriban majimbo yote ya uchaguzi Tanzania bara na visiwani kwa hiyo tunapaswa kuwapongeza chadema na si kuwakatisha tamaa tuwakosoe ,tuwashauri na kuwapa msaada kadri itakavyowezekana kujenga chama mbadala.

Kuandika na kusema ni jambo moja kutenda ni jambo lingine wangapi kati yenu wapo tayari sasa kurudi na kufanya kazi za chama kijijini ili kuleta mabadiliko maandiko yenu hayasaidii na waosoma wachache najua hamuwezi kutoka laptop na viyoyozi vimewafanya kusahau shida na taabu za baba zenu.

Rev. usiwakatishe tamaa hao wachache wanaotoka kwenda vijijini na kunywa maji ambayo hujui ni tope au maziwa. Operation Sangara ni sahihi chadema iwe tayari kujisahihisha kwa matokeo bora zaidi
 

Hapa jukwaani hakuna njia yoyote utakayotumia kuwapa ushauri, kukosoa n.k na kutotafsirika vibaya. Kila nji itaonekana una ajenda ya siri, mamluki, mwana CCM fisadi n.k

Swala la kuangalia je ni namna gani viongozi mbalimbalia wa vyama huwa wanapokea haya maushauri na kusema wayafanyie kazi?

Leo hii Tz kuna historia nyingi nzuri na mbaya, haya yasiposemwa sasa wengine watasema na kuandika kwenye historia, 'failure ya oppositio parties in Tanzania' Historia zatayasema mazuri yote na nia njema ya Chadema kuendesha hii OS, lakini wenye nia nzuri wangapi nchi hii wamefeli? kutokana na kutokutumia njia sahihi za lazima?

Umesema vyema CCM wamezana kujiimarisha tangu 1954, kweli hivi vyama vinaweza ku-compete nacho.

Ili waingie ulingoni na kuwa sawa, cha kwaza ni kupunguza nguvu ya hiki chama, si kwa maneno, kwa sababu unasema kina mizizi ni dhaihiri maneno hayasaidii! kukivunja nguvu huku ni kupigania katiba na kuwa vyama vyote viwe na usawa serikalini. Hapo ndiyo unaweza kuwaweka mabondia wenye uzito sawa katika same ring!
 

1. Mushi nina mwasali mawili, unasema sheria kipindi hico za kuwabana zilikuwepo, leo hakuna sheria ya kuwabana wezi? na je kuna mtu anaeza akanipa rekodi viongozi wala rushwa kipindi cha JKN wangapi walienda jela? wangapi walirudisha mali? na waliofilishi mashirika walichukuliw hatua gani zaidi ya kuhamishiwa kwingineko?

2. Kama umekubali kuwa tunatakiwa kuanza na Katiba, yet hawaifanyii kazi huoni kuwa una-confirm kuwa hawa viongozi unaotaka wachukue nafasi za CCM ndiyo wao wabovu ? they dont know which is the right thing to do?

Au unafikiri kwa hali hii ya OS na ni kwa namna gani, lini, tunaweza kusema tunaiondoa CCM serikalini? Ikiwa hatuna vision ya kuwa na techniques ya kuiondoa CCM kwa mipango na malengo bila kujali bahati huoni hao ndio viongozi wanaotakiwa?

Je unaweza kuniaminisha vipi kuwa Chadema au NCCR etc wakiingia madarakani hatawakula rushwa? na je wakila rushwa our solution at that time itakuwa nini, KUJARIBISHA CUF? Hw3a akina Slaa wenyewe wameshaprove failure ndani ya chama chao, japo hili huwa hamtaki kusikia, kama kuna mtu mmoja anawa challenge ndani ya chama, leo hii mkishika taifa si hatari! we need systems ya kuweza kuangaliana wakati watu wanafanya kazi na maamuzi na system hiyo ni serikali ya mseto! sisi ni wezi kuanzia ngazi ya masecretary na mamesenja-tusijifanye hatujui haya mambo, ufusadi nchi hii hauanziaa CCM! WE ARE LIVING in a criminalised society, na mafisadi walioko ngazi za juu ndiyo wanaowalea wa ngazi za chini, yet tunataka tuwahubirie OS wale wa ngazi ya chini na kati!!??? wa ngazi ya kati wengi hawana mpango hata na siasa wana kula na kunywa! wenyeviti wa vijiji wengi nchi hii wanaingia na nyumba za nyasi kwenye mauongozi yao na kutoka na nyumba za mabati na matofali makali!

Leo hii kupiga kelele RA atoke, wakati kuna raia 10,000 ambao wanategemea kula na kunywa kupitia uwepo wa Rostam are we not fooling ourselves?

WHY dont we motivate or encourage these parties first to make sure our katiba is accomodating all! tukimaliza hapo tuanze hizi OS? au OS unaona kabisa ni kazi ya chadema? Hivi hatujajifunza hii miaka minne?

Watanzania hawa wanahitaji actions, siyo maneno! I joked with someone kuwa leo hii katka mapambano ya ya kudai katiba, ikatokea Slaa analala Segerea , then same Tanzania mnaowaona wajinga, hawajui mambo, mbumbumbu, wasioju akinachoendelea watageuka na kuwa upande wa Slaa, regardless ni CCM (siri kubwa hii).

watanzania hawa sio kama JK nasema wanafuata mkumbo, nataka kusema hakuna jamii inayomsifia mtu hapo hapo kwa kazi nzuri na kuwaponda kimya kimya kwa kazi mbaya! watanzania hawa wanahitaji spark of fire,(Initiator) ka-kitu kadogo tu kuwasha moto wa revolution, na hii ni lazima strong leader awepo wa kuitekeleza ndoto hii, maneno hayana nafasi!

Nikirudi kwenye joke yangu, Slaa akilala segerea siku 2(mfano) huna haja ya OS, huna haja ya kukodi helkopta, huna haja ya kumaliza hela nyingi kwenye kampeni, AUTOMATICALLY JAMII YA TANZANIA inakuwa tuned kwa slaa! These are Tanzanians!!!

Sasa kama tunafanya mambo hali tukijua siyo sahihi kwa wakati huu, ila siku ziende na wananchi wajue tupo, tunamdanganya nani?

Do you want a real uchaguzi? ni ule ambao haujui rais atakuwa nani? any one can be a president, tukifika hapo ndiyo tutakuwa tuko kwenye uchaguzi halisi, na hili tufike watu waivae serikali kutaka serikali ya mseto , hatujachelewa !
 
Sisi wote ni mashahidi wazuri juu ya operation Sangara na pia imefanya vizuri sana katika mambo mengi hata kuwaweka watu wote katika hisia na hatua nzuri kila na baada ya uchaguzi
 
Tena Chadema wakayaulize mapema, kabla akina REDET na wengine hawajaenda kuyauliza, kutoa na kuwalisha watanzania majibu yaliyopinda.
 
Wakuu zangu, mada hii ni nzito sana naomba kuchangia kidogo kukumbushana yaliyo mema yaani yanayoweza kuijenga nchi yetu na sii kutoa hoja za kufikirika.

Wengi hapa wanafikiria kwamba kuondoka kwa CCM ni sawa na kuruka mkojo ukakanyaga mavi lakini tunasahau kwamba kitu kinachoweza kubadilisha nchi sii vichwa vya watu bali mawazo mbadala ambayo yatatunga sheria kali dhidi ya Uharamia wa aina yoyote ile.

Sasa tunapozungumzia Ufisadi, ni nchi zote zina Ufisadi.. kifupi binadamu wote tumeumbwa na tamaa ya Ufisadi isipokuwa sheria na utekelezaji wa sheria hiyo ndio pekee unaweza kuwabadilisha watu wake. Hata manabii wa Mungu waliweza kuboresha na pengine kuleta ustaarabu ktk matendo yetu tofauti na hali iliyokuwepo hapo awali. Na kama hawa mitume wangefikiria ukubwa wa udhalimu ulokuwepo kulinganisha na nguvu ya mahubiri yao basi sidhani kati yetu angekuwepo mtu mwenye matumaini ktk mafanikio yao.

Nadhani ni bora sana tuwe wepesi wa kuwa na HOPE badala ya kusingizia kila kitu kwamba hakiwezekani pasipo CCM..Ukweli ni kwamba INAWEZEKANA!...

Binafsi baada ya kumsoma Rev. Kishoka nadhani ujumbe wake umesimama zaidi kitaalam badala ya kisiasa. Na binafsi naamini kabisa kwamba Kisiasa hutakiwi kuwauliza wananchi walichokipata.. kwa sababu mabadiliko yapo mengi tu hasa ukizingatia tulikotoka. Rev. anajua nini maendeleo nini tofauti ya maendeleo toka hatua moja kuingia nyingine jambo ambalo Watanzania wengi hasa wa vijijini hawafahamu kabisa. Kuwepo kwa magorofa na mali nyingi toka nje ni maendeleo makubwa sana kwao acha mbali utajiri wa wananchi wachache wanaomiliki mabillioni. Ukiwauliza wananchi watakwambia hatukuwa na hali hii hapo zamani hivyo hatua ya maendeleo ya mnyonge ni kwa mapana ya kutoa tonge mkononi kuingia kinywani, tofauti na orodha kubwa aloiweka Rev. Kishoka ambayo kwao wananchi ni kikwazo kikubwa kuelewa tu ilitakiwa kuwa vipi kuweza kuisifia CCM.Maanake wao wanayaona maendeleo kwa mtazamo finyu usiokuwa na exposure.

Ni katika mtazamo huu huu utawakuta wengi wakisifia utawala wa Mwinyi au Mkapa kwa kulinganisha hali ya Mwalimu ndani ya Ujamaa kuingia Ubepari wasijue kwamba ni mfumo wa Kibepari ulioboresha mazingira ya biashara na sii mfumo wa Utawala..Na ndio maana tunaziona tofauti kubwa baina ya Mwinyi, Mkapa na hata JK ndani ya Ubepari kuwepo hali kuna mapengo mengi ya Kiutawala baina ya wahusika hao hao..Moja kubwa ukiwa ni UFISADI.

Hivyo kwa mjumuiko wa maelezo yangu ni kwamba Ufisadi nchini ndiye ADUI mkubwa wa maendeleo ya nchi yetu na kwa bahati mbaya umefikia kiwango ambacho hakiwezi kuondoka kirahisi. Kila mtu ni fisadi kwa njia moja ama nyingine kutokana na Ubinafsi wa kibepari tusiokuwa na elimu nao...na ndio maana utaona nchi nzima inanadiwa, kila kiongozi na wananchi ni madalali wa nchi na rasilimali zake..JK akinadi nchi ugenini, mawaziri wakitafuta wawekezaji, wananchi wakitafuta wanunuzi hadi wa ndani yaani pato kubwa la nchi na wananchi wake linategemea zaidi Udalali kupata hicho kidogo cha ruzuku. Sisi sii wazalishaji wala wanunuzi isipokuwa madalali (middlemen) kwa mali yetu wenyewe.

Binafsi, siamini kama Chadema ama chama chochote kinaweza kutuondoa ktk hali hii pasipo Udikteta...Tanzania inahitaji mtu kama Chavez.. Na kwa vile matatizo yetu yanatoka ndani nchini zaidi na sii nje ya nchi basi Chavez wetu azidi kuhubiri biblia ya kumwondoa CCM (Shetani) kwa kuelezea madhara ya shetani huyu ili wananchi waongoke kwanza kisha utakapo kuja shika madaraka itakuwa rahisi sana kuiwezesha sheria kali kwa wahalifu wote...Ndivyo alivyofanya Chavez kabla hajapata ushindi na anafanya kile alichowaahidi wananchi wake.. Kakomesha Ufisadi mkubwa wa nchi za magharibi na wananchi wapo nyuma yake.. Sisi pia inawezekana kuuondoa Ufisadi wa ndani ya nchi yetu..

Mambo mengi ambayo CCM imeshindwa kuwawakilishia wananchi imetokana na ukweli kwamba Ufisadi umefikia kufur.. hivyo ikiwa viongozi wa chama (dini) wanafanya kufur unategemea nini wafuasi wake watafanya?...

Leo hii Ufisadi umeota mizizi kwa sababu viongozi wetu ni Mafisadi hivyo tusitegemee jema toka kwa raia wanaofanya ibada za kifisadi...Tuendelee kuukemea Ufisadi na hakika tegemeo kubwa la wananchi kuondokana na Ufisadi lilikuwa Kikwete mwenyewe.. Haku deliver na ndio maana analaumiwa. Hivyo INAWEZEKANA kabisa mtu mwingine iwe toka Chadema au CUF kufuta kabisa Ufisadi hata kama umeota mizizi kiasi gani..kiongozi yeyote Dikteta anaweza kufuta Ufisadi na itakuwa rahisi kwake kudeliver yote tunayoyahitaji chini ya Utawala bora...Pasipo AZIMIO hatuwezi kujenga hoja..na vigumu kuwawezesha wananchi. Nani baina yetu alitegema Obama anaweza kuleta mabadiliko ya Afya Marekani?.. walishindwa wangapi, leo huyu kaweza kutimiza Azma ya chama ambayo iliwashinda vigogo wengi wenye nguvu zaidi yake...

Vita ya Ufisadi sii vita ya Chadema pekee ni yetu sote hata ukiwa ndani ya CCM.. kupinga hoja kama hii inatokana na kutofikiria athari za Ufisadi kwani matokeo yote ya uchumi wetu, kuharibika kwa mariasili zetu kunatokana na Ufisadi hivyo mgawanyo wa kiuchumi hauwezi kuwa sambamba na maendeleo ya nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…