Nionavyo Udhaifu wa Operesheni Sangara

Nionavyo Udhaifu wa Operesheni Sangara

Monoko Mushi,

Bila kuunda mfumo unaokubalika hata kujenga katiba mpya, kubadilisha uongozi kwanza ni kazi bure!

CCM ndio viongozi sasa hivi na wamesema mara kadhaa kuwa wao hawaoni tatizo lolote jinsi Katiba ilivyo, mfumo wa kiutawala ulivyo au hata sheria zilivyo, zinakidhi matakwa na maslahi yao.

Tunahitaji kujenga msingi mpya ambao kila mtu atanufaika na msingi huu na si mtu mmoja.. Leo hii CHADEMA, CUF, TLP au NCCR wakishika madaraka, nao wataona manufaa ya mfumo ulioinawiisha CCM, na wao watasema hakuna haja ya kubadilisha Katiba au mfumo.

Kama leo hii ndani ya CHADEMA kuna mgongano wa kifikra kati ya makundi mawili, kama vile kulivyo na mvutano ndani ya CCM< je ikifika zamu yao, ni nani atakuwa na nguvu kusema ni lazima tubadilishe mfumo na katiba?

Tulichojifunza kutoka CCM ni hiki. Leo kundi la Wapiganaji linataka mfumo mpya, katiba mpya, lakini wamezidiwa kura ndani ya CCM kwa wale wanaoneemeka na kunufaika na Katiba jinsi ilivyo.

Panapokuwa na mvutano na msuguano namna hii, njia pekee ni kushinikiza kuweka misingi mipya ambayo itahakikisha hakuna atakayeingia na kuwa na dhamana ya kuongoza nchi atajifanyia mambo anavyotaka.

Reverand:
1)Tumekubaliana(ku compromise) kwamba mabadiliko hayo ni vyema yakienda sambamba(hand to hand)
2)Tumekualiana katiba ni tatizo?
3)Tumekubaliana viongozi ni tatizo

Sln:
Sasa solution hapa ni nini?naweza ku conclude na kusema so and so should be or is a solution,lakini obvious maswali ya ziada yatafuatia!

Nikupe mfano;Tume conclude,kwamba tunahitaji vyote sambamba hilo tunakubaliana,lakini utekelezaji wake unaweza usiwe possible,yani kupata ama ku achieve both at the same time,kwa mantiki hiyo tunabaki na swali la msingi,given all the facts,kipi kianze?Uongozi makini then katiba ama katiba then oungozi makini? and please give the reasonable reasons why!

Umeshaweka sababu kadhaa ni kwanini unadhani katiba kwanza,na mimi nimeweka zangu kwanini uongozi kwanza....So lets go from there,njoo na convincing points hapa sasa kwamba tukibadilisha katiba kwanza ni vyema zaidi ya kubadilisha uongozi kwanza...Ya kwamba ni bure kama tusipoanza na mfumo kwanza,swali ni kwamba,ebu jaribu kufikiri zaidi,what makes the other? Hivi unadhani ni viongozi makes a good katiba ama ni a good katiba makes viongozi makini?
 
Katiba haisababishi uongozi bora na uongozi wenyewe hausababishi katiba bora. Wananchi ndio huchagua uongozi na wakichagua uongozi mbaya matokeo yake yako wazi; wakichagua uongozi mzuri basi uongozi huo utaweza kusimamia kuandikwa kwa Katiba bora ambayo wao viongozi bora watakuwa tayari kuilinda na kuwa chini yake.

Hivyo, wananchi bora huleta viongozi bora na ambao huongoza kuandika Katiba bota itakayowafaa wote; na ikishaandikwa, wote wanakuwa chini ya Katiba hiyo bora.

Ndio maana Katiba yetu inasema "wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali
itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii;".. kumbe msingi wa mamlaka yote siyo viongozi, katiba n.k bali ni wananchi! So.. kama wananchi wakiwa wazembe mamlaka zitakuwa zembe..
 
Hayo mambo ya serikali ya mseto ni nje ya pointi hayana uhusiano na weaknesses za OS!
Mkuu kwenye highlights kweli umelikoroga,hakuna shida kuhusu muda ninao kwa takriban wiki hivi....Ila ebu jaribu kupitia hiyo posting yako kwa makini na uweke msisitizo kwenye highlights,mzee umelikoroga kweli kweli,mara unakubali mara unakataa,mara unanipachika uchadema halafu unajenga hoja ya uchadema vs u ccm na huku ukijitoa kwamba uko neutral na wakati ni mkororgo mtupu huku ukisema hakuna nayefaa nk,bado unataka tutegemee mafisadi wattupatie katiba suistanable!?

Samahani,turudi kwenye hoja za msingi,ama labda hatujaelewana,tafakari tena na narudia,pitia postings zote na yako ikiwemo.

Kaka asante kumbe wewe kujadili mambo ni lazima ujadili sawa na title hauwezi ukajadili kupanua wigo asante kwa kunipa hilo angalizo!!, sasa kama mtu ameona udhaifu asitoe solution? Na hiyo solution lazima iwe ndani ya OS?

Back to the OS, naomba kujua unafikiri kwa mawazo yako ni kwa vipi OS itasaidia kuindoa CCM, fanya analysis kulingana na historia ya watanzania, na Unafikiri ni lini upinzani au tuseme chadema wanaweza kuishinda CCM.

Naomba analysis ya OS isiwe ya kufikirika, toa kwa mifano ni operation gani ya kuhubiriwa ilifanikiwa nchi, hii, chukua tabia za watanzania na -draw conclusion kuwa OS is viable solution. Ukiweza hivyo utakuwa umenisaidia sana.

Mkuu jmushi1........nakubaliana sana na hoja yako kuwa inabidi tupat viongozi wapya.......na hao viongozi wenyewe inabidi wawe wenye vision na madikteta kama Hugo Chavez (nai-support hii idea ya Bob Mkandara).............

.

Ogah Mkuu tuacheni siasa, niambie kwa mazingira ya Tanzania tutapataje viongozi bora?. Nipe indicators ya kupata viongozi bora ambayo unajua imeshafanikiwa.

Niambie OS itawezaje au ina kitu gani special ambacho kitawezesha kuindoa CCM!

Hints: rudia historia ya vyama vingi tangu 1992. angalia tuhuma za ufisadi kutokea mwembe yanga, angalia bungeni

Tufanye evaluation tangu tumeanza kusema ufisadi tumefanikiwa kwa kiasi gani na wananchi wa tanzania wamerespond kwa kiasi gani.

Angalia matokeo ya chaguzi serikali za mitaa yaliyofanyika juzi tu, sio siku nyingi

Then nieleze namna ya kupata viongozi bora au kuiondoa CCM.YOu may propose any!

hiyo poposal yako weka vision namna itakavyo-draw attention ya kila raia na kusababisha stimulation ya uchaguzi nchi hii.
 
Katiba haisababishi uongozi bora na uongozi wenyewe hausababishi katiba bora. Wananchi ndio huchagua uongozi na wakichagua uongozi mbaya matokeo yake yako wazi; wakichagua uongozi mzuri basi uongozi huo utaweza kusimamia kuandikwa kwa Katiba bora ambayo wao viongozi bora watakuwa tayari kuilinda na kuwa chini yake.

Hivyo, wananchi bora huleta viongozi bora na ambao huongoza kuandika Katiba bota itakayowafaa wote; na ikishaandikwa, wote wanakuwa chini ya Katiba hiyo bora.

Ndio maana Katiba yetu inasema "wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali
itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii;".. kumbe msingi wa mamlaka yote siyo viongozi, katiba n.k bali ni wananchi! So.. kama wananchi wakiwa wazembe mamlaka zitakuwa zembe..
MM heshima natanguliza. Nakubaliana nawe wananchi ndiyo chanzo cha mamlaka yote. Lakini binadamu anaweza kuwa kigeugeu. Wananchi wanaweza kumchagua kiongozi mzuri baadaye akageuka. Katika hali kama hii unahitaji katiba bora ili kuwadhibiti viongozi wasiwe vigeugeu. Kwa mantiki hii katiba bora itafanya viongozi wawe bora. Pia kiongozi bora anaweza kufanya katika iwe bora, kwa kuwa anashiriki katika kuitengeneza katiba. Mfano, juzijuzi Dr. Slaa ambaye ni kiongozi bora ameona madudu kwenye sheria ya gharama za uchaguzi, ameshapiga kelele tayari. Bunge litakapofanya mabadiliko yeye kiongozi bora amesaidia kuleta sheria bora. Na katiba ni hivyohivyo.
 
Watanzania.. kwa kadiri ya kwamba wananchi wanaelewa jukumu lao la kuchagua viongozi bora haijalishi kiongozi atafanya nini mbeleni kwa sababu atajua wananchi watamuondoa. Demokrasia siyo haki ya kuchagua viongozi wazuri tu bali pia kuchagua viongozi wabovu na haki ya kuwaondoa tukigundua hivyo.

Hivyo, hatuwezi kuepuka kuwa na viongozi wabovu, lakini ni muhimu kutambua kuwa tuna uwezo wa kuwaondoa na hili ndio lengo kuu la uchaguzi.
 
I wish Wananchi wangelikuwa wanatambua hilo..........kelele zetu hapa JF zingekuwa chache..........otherwise huo hapo juu ndio ukweli wenyewe.............
 
....................Ogah Mkuu tuacheni siasa, niambie kwa mazingira ya Tanzania tutapataje viongozi bora?. Nipe indicators ya kupata viongozi bora ambayo unajua imeshafanikiwa..............Niambie OS itawezaje au ina kitu gani special ambacho kitawezesha kuindoa CCM!

Unajua nimecheka sana majadiliano yako na jmushi1.............mkanikumbusha ile hadithi ya "egg & chicken"..............

well, Mkuu Webby tuko ukurasa mmoja........OS ina shortfalls zake hivyo tuwasiadie kimawazo CHADEMA ili waimarishe mapambano ya kifikra..........operation kama hizi zina impact................results zake zaweza zisiwe immediate............lakini in the long run tunajua wananchi wanapata elimu ya uraia which is most important............kama Mbunge wa CCM alipata kura 1000 last time trust me baada ya OS check the figures again hata kama atashinda..............inawezekana isi-work sehemu zote kwani si wabunge wote wa CCM hawawajibiki kwa wananchi wao..................pia ukumbuke CCM they watch this OS...............na watakuwa makini kupitisha wabunge wao kwenye kura za maoni............wasiouzika "yawezekana" wakaula wa chuya............. kw ahiyo OS ina impact....................

..............Hints: rudia historia ya vyama vingi tangu 1992. angalia tuhuma za ufisadi kutokea mwembe yanga, angalia bungeni

Tufanye evaluation tangu tumeanza kusema ufisadi tumefanikiwa kwa kiasi gani na wananchi wa tanzania wamerespond kwa kiasi gani.

Angalia matokeo ya chaguzi serikali za mitaa yaliyofanyika juzi tu, sio siku nyingi

Then nieleze namna ya kupata viongozi bora au kuiondoa CCM.YOu may propose any!

hiyo poposal yako weka vision namna itakavyo-draw attention ya kila raia na kusababisha stimulation ya uchaguzi nchi hii.

Ndio maana tunatafuta njia za kupata viongozi wanaofaa sasa hivi.................CCM tumewapigia keleleee weeee kuhus katiba.......gues what.........wakaja na counter argument.................."tuelezeni ni wapi katiba ina mapungufu...........mapungufu hayo yatachambuliwa na ikibidi katiba itakuwa amended................."

sasa ukiangalia majority kwenye Bunge ndio hao CCM (mashetani/majambazi/walevi).......unategemea fisadi/mbinafsi/mlarushwa atabadilika ili abadilishe katiba ili ije imbane yeye mwenyewe?..............no way!

Unajua CCM wala hawana wasiwasi......wanajua wananchi ni "mali" yao ambayo itawaidhinisha kwenye power regardless...........so they don't care about mabadiliko ya Katiba...............

machache tunavyoweza kufanya na tuyafanye kwa juhudi zote............ikiwemo kampeni kama OS

Mkuu Webby...........tufanyeje ili tupate viongozi wanaofaa............watakaokubali kushirikiana na wananchi kutengeneza Katiba Mpya?
 
Unajua nimecheka sana majadiliano yako na jmushi1.............mkanikumbusha ile hadithi ya "egg & chicken"..............

well, Mkuu Webby tuko ukurasa mmoja........OS ina shortfalls zake hivyo tuwasiadie kimawazo CHADEMA ili waimarishe mapambano ya kifikra..........operation kama hizi zina impact................results zake zaweza zisiwe immediate............lakini in the long run tunajua wananchi wanapata elimu ya uraia which is most important............kama Mbunge wa CCM alipata kura 1000 last time trust me baada ya OS check the figures again hata kama atashinda..............inawezekana isi-work sehemu zote kwani si wabunge wote wa CCM hawawajibiki kwa wananchi wao..................pia ukumbuke CCM they watch this OS...............na watakuwa makini kupitisha wabunge wao kwenye kura za maoni............wasiouzika "yawezekana" wakaula wa chuya............. kw ahiyo OS ina impact....................

Ndio maana tunatafuta njia za kupata viongozi wanaofaa sasa hivi.................CCM tumewapigia keleleee weeee kuhus katiba.......gues what.........wakaja na counter argument.................."tuelezeni ni wapi katiba ina mapungufu...........mapungufu hayo yatachambuliwa na ikibidi katiba itakuwa amended................."

sasa ukiangalia majority kwenye Bunge ndio hao CCM (mashetani/majambazi/walevi).......unategemea fisadi/mbinafsi/mlarushwa atabadilika ili abadilishe katiba ili ije imbane yeye mwenyewe?..............no way!

Unajua CCM wala hawana wasiwasi......wanajua wananchi ni "mali" yao ambayo itawaidhinisha kwenye power regardless...........so they don't care about mabadiliko ya Katiba...............

machache tunavyoweza kufanya na tuyafanye kwa juhudi zote............ikiwemo kampeni kama OS

Mkuu Webby...........tufanyeje ili tupate viongozi wanaofaa............watakaokubali kushirikiana na wananchi kutengeneza Katiba Mpya?

I do believe our discussion here iwe kufikia ultimate workable solution

-Ogah tumenza uchaguzi wa vyama vingi 1995, kuna chaguzi tatu tumezipita
-Katika kila chaguzi zinazofuata CCM ndiyo wanaongeza kupata kura! mpaka wa 2005 ushindi wa kishindo,

Leo tunazungumza 2010 almost 20yrs after system hii inaze , LEO hii tuna hakika mimi na wewe kuwa next president ni Jakaya Mrisho Kikwete kutoka CCM chama ambacho tunakiita cha majambazi

Hatuishii hapo nature ya OS na mahubiri kama hayo ni ephemeral, ukipita upepo wa vyama vingine wananchi wanageuka, siyo permanent!

PIGA PICHA HII, lets assume

Rudi 1992, Katiba ingebadilika, na mwaka 1995 wakati wapinzani wamepata asilimia 40% tungepata nfasi kulingana na hiyo asilimia 40, lets say katika wizara 20, tano wanachukua chadema au NCCR at that time.

Leo hii assume tungekuwa wapi?, I strongly believe katika uchaguzi wa mwaka 2010 tungekuwa hatujui rais anatoka chama gani. Ikifikia hatua ya ''yoyote anaweza kuwa rais'' NDIYO muda huo sasa!! msimimko wa uchaguzi utagusa kila nafsi ya mtanzania, kama vile mnaangalia mechi ya mpira!

Hakuna hata siku moja chini ya jua hili serikali itasema mabadiliko haya chukueni,

Weakness moja kuliko zote ni kuwa ukiwauliza wapinzani wanasema CCM wamesema hawataki serikali ya mseto!! my God is this country belong to CCM au kwa watanzania?

Najua tuna uchungu na tumeichoka CCM, Zanzibar wamewezaje? na ninachosema ni kufikia lengo hilo, hii ya sasa hivi ni sandakarawe! mkuu historia inaonyesha hivyo. kikubwa ni kuwa mabadiliko au kutaka serikali ya mseto maana nyingine ni wote kuwa sawa na kuanza mbio ka pamoja, hivi sasa CCM wako mbele sana ndiyo maana hizi kelele haziwatishi wao achilia mbali wananchi.

Turn up ya kupiga kura inakuwa kubwa kama chaguzi zina msisimko, mwaka huu wakat majority wanajua CCM itashinda then turn upe itakuwa ndogo.

Ok, ili tusilaumiwe na vizazi vijavyo, ijulikane haya na hizi operation zitakumbukwa sana tu. Serikali ya mseto is self-minitoring systems, wakija NCCR leo na wakaanza kama CCM then tusubiri baada ya miaka mitano waondoke! what if ikitokea ya Kenya.

Ogah tungekuwa na serikali ya mseto leo hii thread hizi zisingekuwa hivi, leo hii vyama vya siasa visingelala kutegemea ruzuku tu, unavyoona chadema wanapiga kelele na kujitoa si sawa na vyama vingine! vingine vimelala na je chadema kazi hii wataiweza? when should we excpect positive results? tumejifunza nini na kelele za ufisadi toka mwaka 2005 mpaka leo, the very same government bado itashinda, ndiyo maana nauliza, is it wrong to change tactics? if yes why we are not telling them?

Hivi kuna ubaya gani mtu akasema Slaa na style zenu haifai lets move this way, tukimwonea aibu Slaa how are we defining Tanzanian na hizi harakati zetu?

we are on the same agenda, same page, same goal we may only differ in how to reach same traget. Yours techniques has been proven wrong for 20yrs should we continue to use this?

Tusubiri kuibiwa kwanza ndio tubadili chama au tuwe na system tuzuie wizi usiwepo??

Serikali ya Mseto ingekuwepo wizi wa EPA, RICHMOND, vingetokea wapi? akina mama wangapi wanakufa kwa kukosa dawa na kulala sakafuni, yes tumesema sana nini kilichotokea? fedha zimerudishwa? kama zimrudishwa whi is hero mbele ya wananchi CCM au upinzani? si ndio watu wanampa sifa JK! eti kisam Mramba na Yona wameenda mahakamani! should we learn to prevent uwizi au tusubiri watu waibe kama akina Mkapa ndiyo tupige kelele? kitu gani kitabaki kwa kizazi kijacho?
 
Naona mjadala umejikita katika mambo makuu mawili, nayo ni Uongozi na na Katiba, sasa ni Bora tukajielekeza katika Kujibu maswali yafuatayo

1: Uongozi Bora: Nini kifanyike ili Wananchi wachague Viongozi Bora na makini
2: Katiba: Nini kifanyike ili tuwe na katiba Mpya na Nzuri
 
I do believe our discussion here iwe kufikia ultmate workable solution

Webby,
Zanzibar its a unique case..........pale kuna Upemba na Uunguja............Seif amepata nguvu sababu ya huo mgawanyiko nathing else..............kitu hiyo bara haipo kabisa...........

Serikali ya Mseto ni very good...........The question comes.........how do we get there.......i.e. Serikali ya Mseto?...........

JKN aliwashauri CCM kuhusu hilo waruhusu kule Zanzibar.........jamaa mpaka leo wanaweweseka (how many years past)............vipi huku Bara?......i'm afraid it may take us half a century................

Ninacho sisitiza ni kuwa kuna vitu vidogo lakini vina impact.........twaweza kuvifanya na vikatupeleka tunako kuhitaji...........
 
Naona mjadala umejikita katika mambo makuu mawili, nayo ni Uongozi na na Katiba, sasa ni Bora tukajielekeza katika Kujibu maswali yafuatayo

1: Uongozi Bora: Nini kifanyike ili Wananchi wachague Viongozi Bora na makini
2: Katiba: Nini kifanyike ili tuwe na katiba Mpya na Nzuri

Maswali yako mzuri nitajibu kwa kifupi

Uongozi bora

Kuchagua uongozi bora ni tabia aidha ya asili ya ya kufundishwa. Sio kitu cha kufanyaika kil baada ya miaka mitano. Wala watu hawatabadilika kwa kusikia kwa muda fulani tu. Tabia ya kuchaguzi viongozi bota inaanzia nyumbani, kwenye ngazi za mitaa, kata, tarafa , wilaya, maofisini, mavyuoni, mashuleni. Ndege ya Uchumi umeshachagua viranja wewe! kuna Dr. mmoja alisema society zetu zinaenda kuchagua viongozi kishikaji, wapole na mchezo huu ndio unaendelea mpaka ngazi ya taifa, kuchaguz kiranja mnoko ! NO!

Hii tabia ya kuchagua viongozi inaendana na sana na historia ya taifa au watu wa mahali hapo, kwa mfano Marekani pamoja na kuwa na uchumi mzuri they are excited na ma-uchaguzi, wakati sisi pamoja na kuwa an shida sana still hatuoni umuhumi wa kuchagua viongozi bora tuna ile ya ''huyo huyo anafaa' why? Tumezoea shida, shida kwetu sisi sio shida, ndiyo maisha, wakati JF wengi wameona na kufunguka macho, na kusema mwananchi wa karagwe anaishi maisha ya shida, wao HAWAJIONI HIVYO! kwao bongo tambarare!

Hii ni issue ya kuanzia mashuleni, msikitini, makanisani n.k kwa ujumla ia a big problem! Unless taifa lilipitia hali ngumu sana kama vita, majanga, shida za kiuchumi hapo ndio watu watachagua kiongozi mzuri.

Mabadiliko ya katiba

Ili katiba mpya na nzuri ifanyike , mazungumzo yanatakiwa, harakati na kila aina ya style, kwangu mimi mabadiliko ya katiba itakayoweza kuzalisha serikali ya mseto Tanzania ndio ukombozi wenyewe! then from there Taifa jipya litazaliwa taifa lenye nuru ya matumaini yote, at that time tukisema our mision is to do this we know for sure we will not waste out time and money

CUF zanzibar ni mfano mzuri wa kuwa inawezekana, kwa sasa as I said vyama vyote vitaendela kuisaidia CCM na CCM watachukua Idea zao na they will rule forever! Nimesema kwa mazingira yetu ya hapa.

Usitishike hata mwaka huu inawezekana!
 
I wish Wananchi wangelikuwa wanatambua hilo..........kelele zetu hapa JF zingekuwa chache..........otherwise huo hapo juu ndio ukweli wenyewe.............

Tungekosa kazi na chemsha Bongo kuitafakari Tanzania
 
Webby,
Zanzibar its a unique case..........pale kuna Upemba na Uunguja............Seif amepata nguvu sababu ya huo mgawanyiko nathing else..............kitu hiyo bara haipo kabisa...........

Serikali ya Mseto ni very good...........The question comes.........how do we get there.......i.e. Serikali ya Mseto?...........

JKN aliwashauri CCM kuhusu hilo waruhusu kule Zanzibar.........jamaa mpaka leo wanaweweseka (how many years past)............vipi huku Bara?......i'm afraid it may take us half a century................

Ninacho sisitiza ni kuwa kuna vitu vidogo lakini vina impact.........twaweza kuvifanya na vikatupeleka tunako kuhitaji...........

Is that not our weakness? , if that will take us half a century what about these operations? How can ypu account that it will take us a half century are not confirming Mkamp's argument kuwa tunapenda njia za mkato?

We may discuss this thread again baada ya uchaguzi, may be from there we can open our eys and see what should be done now.

That Mseto is necessary to our nation not an option failure do that CCM will rule forever thay know that and they will discourage any movements toward new constitution!
 
Wakuu zangu,
Kulingana na hali halisi ya nchi yetu nadhani la kwanza kabisa tunahitaji kurekebisha ni KATIBA, hasa ktk kifungu tata cha chaguzi za Vingozi na nguvu zao kiutawala. Hapa nikiwa na maana hatuwezi kuwa na viongozi bora ndani ya mfumo unaopingana na malengo ya kuwapata viongozi bora..Hii haiwezekani tutakuwa tunacheza mduara tu.

Kwa maelezo yangu haya machache nitautoa mfano wangu binafsi ktk mtazamo wangu. Kwanza kabisa inatakiwa kila mbunge atakayegombea ubunge awe mkazi wa jimbo hili..mkazi na sii kutafuta jimbo lisilo kuwa na upizani kama ilivyo sasa hivi. Hii itasaidia zaidi ufanisi wa hawa Wabunge wenyewe kuwa viongozi bora.. hakuna mtu kati yetu anayependa kuishi ktk mazingira magumu, hivyo kumlazimisha mbunge kugombea ktk jimbo analoishi ni hatua ya kwanza kabisa ya kuleta maendeleo ktk majimbo hayo. Huyu mbunge atalazimika kuyaleta maendeleo kwake kutokana na yeye mwenyewe na familia yake kuishi ktk mazingira hayo..Hivyo basi, hatuwezi kulazimisha sheria hii pasipo katiba kurekebishwa ama kubadilishwa...

Pili, maadam nchi yetu ina mihimili mitatu nadhani itakuwa bora sana kama kila mhimili utajitegemea kwa Uongozi nikiwa na maana Mbunge yeyote haruhusiwi kuwa Waziri ama kushika madaraka ndani ya ofisi ya Rais..Vile vile kwa makundi mengineyo kutoingia upande wa pili ama tatu, ili kuondoa Ukiritimba wa viongozi kuwa Wabunge, Mawaziri na wengine Ikulu kuwa waamuzi ya ngazi zote za kiutawala.. Hivyo sheria itamzuia rais wetu kuteua kiongozi yeyote ndani ya serikali ama Ikulu kutokea bungeni.

Tatu, tanzania haihitaji ngazi ya RC na DC hawa wote ni mzigo mkubwa kwa wananchi na ndio sababu kubwa ya Ufisadi ngazi ya mizizi kunyonya nguvu za wananchi..Na kama ni muhimu sana kuwa na RC ama DC kwa sababu ambazo mimi binafsi sizijui basi watu hawa wachaguliwe na wananchi wenyewe na sio uteuzi wa rais ili kuzipa nguvu manispaa na tawala za mikoa kupitia wananchi wenyewe...Na mwisho, kuwapa wananchi nguvu ya kisheria kumfikisha mahakamani kiongozi yeyote pasipo kulindwa nasheria hasa ktk maswala mazito ya Ufisadi (Uharibifu wa aina yeyote ile).

Haya maswala hayawezi kupatikana pasipo kuwa na sheria kikatiba, hivyo nadhani katiba ni muhimu zaidi kufanyiwa marekebisho kwa malengo ya kupata viongozi bora..Na sidhani kama tunaweza pata viongozi bora kuitengeneza katiba ktk mfumo ambao unachagua kwanza viongozi wabovu.. nani ataiweka ama kupitisha sheria inayowakandamiza!... Mfano mdogo tu ni sakata na EPA, Richmond, Rada na kadhalika yote haya yametokana na kutokuwa na viongozi bora waliotokana na mfumo mbaya wa sheria.
 
Nashukuru kwa mjadala huu, hili limekuwa somo zuri sana kwangu.Week ijayo nitakuwa Kyela napeleka ujumbe huu kijijini kwangu.Ahsanteni sana!
 
Mkandara,
Hili la MaRC na DC kuchaguliwa kwa kura alilisema Freeman Mbowe mwaka 2005 wakamwita mkabila. CCM walimwita mkabila kwa kauli hiyo.
 
aha ha! ulitaka CCM wasemeje?
 
aha ha! ulitaka CCM wasemeje?

The point is.....usitegemee majambazi CCM walio majority bungeni wakabadilisha katiba huku wakijua mabadiliko hayo yatawapa challenge wao wenyewe...........
 
Hivi jamani wakina kalebu tupo wachache kiasi hiki jamani, watu tunaoiyona kanani hata kama imezungukwa na majitu? Nyie endeleeni kujiona mapanzi ooh katiba oooh sijui nini, mnaweza kupata vyote hivyo na mambo yakawa yale yale.

Tatizo letu ni kwamba watu wanajiona kama mapanzi ni wengi kuliko wakina kalebu hata hivyo kanani tutaiona tu na good news ni kwamba wote wanajiona ni mapanzi hawata fika huko
 
The point is.....usitegemee majambazi CCM walio majority bungeni wakabadilisha katiba huku wakijua mabadiliko hayo yatawapa challenge wao wenyewe...........

Kumbe mkuu ulidhani nataka CCM wabadili katiba? kwani Zanzibar Katiba wamebadioli CCM? mabadiliko ya katiba yanaletwa na nia, nguvu na mshikamano wa wananchi, hata siku moja CCM hawawezi kukubali hilo. Vyama vaya siasa should dedicate their resources in mabadiliko ya katiba. Ogaha tusitegemee zur5i lolote kutoka CCM! mabadiliko yanaletwa na wananchi kupitia vyama, bila mabadiliko CCM watatawala milele study zimeonyesha hivyo.

Sio rahisi ni nguvu na kujitoa vinatakiwa hapo ikiwa na kuwa tayari kudhalilishwa na kulazwa polisi, na hili hatulitaki! na hao wanaosema wapinzani hawataki hili!
 
Back
Top Bottom