Nioneshe ofisi yenye weledi wa kimataifa nami nikuoneshe kuku mwenye mwanya

Nioneshe ofisi yenye weledi wa kimataifa nami nikuoneshe kuku mwenye mwanya

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Kwa kipindi chote nilichofanya kazi na ofisi za serikali au kupata huduma ofisi za umma, nimejiridhisha pasipo na shaka kwamba hakuna ofisi hata moja inayokidhi vigezo vya kimataifa katika utoaji wa huduma.

Ofisi zote Bongo ni ujanja ujanja tu. Watu wameacha elimu darasani na kwenye madaftari huko kazini kila mtu anajiendea anavyojaaliwa.

Hali ni mbaya zaidi hasa kwenye ofisi za Halmashauri. Wamejaa wavivu, ni kama wananchi wanahudumiwa na watu wasio na shule kabisa. Longo longo kibao ili akuhudumie lazima untengenezee mazingira ya kumpa hela au kujuana.

Zipo ofisi kadhaa kama TRO na NHIF huwa naona zikuwa certified na ISO. Lakini uhalisia ni tofauti kabisa, nadhani waliwapa cerification bila kujua huku field kukoje waliangalia makaratasi tu. Wote ni wale wale tu waliokunywa uji wa mgonjwa. Ndiyo maana hapa Bongo mtu akiwa na kauwezo kidogo anaonekana kichwa kishenzi.

Ninakupa hii sio mambo ya kusimuliwa. Kama unabisha nitajie ofisi moja ili tubishane. Kwa hiyo, hatua zaidi tunatakiwa kuchukua kama nchi. Bahati mbaya zaidi hata viongozi wa juu nao ni walewale tu.
 
Taasisi nyingi sio za kiserikali ata binafsi ukija kwenye swal la utendaji wengi wanafanya kazi kwa kujuana au kwa mazoea zoea.
 
Ukitoa mashirika ya kimataifa ambao kimsingi wao hawataki ubabaishaji, KFC restaurant wana weledi kimataifa kwa utoaji wa huduma kuliko ofisi zetu za umma ikiwamo mashirika na taasisi mbalimbali za umma yaani wamezidiwa weledi na wahudumu wa bar ya kitambaa cheupe ya tabata na Sinza.
 
Mtoa maada uko sahihi angalia kwanza jinsi wanavotimiza majukumu yao hao watumishi ndio utajua kwa nini kama nchi hatusongi mbele, na unakuta eti faili wiki mbili halijasainiwa.

Unaenda ofisi nyingine eti mkurugenzi kasafiri hivo baadhi ya majukumu hayafanyiki hadi arudi kutoka safari halafu anakaa wiki huko, hua mambo yanafanyika kwenye maofisi unaona hawa watumishi ni malimbukeni na washamba, lakini kwenye kupanga kuiba mali ya umma wanakua na umakini na sio utendaji.
 
Ukitoa mashirika ya kimataifa ambao kimsingi wao hawataki ubabaishaji, KFC restaurant wana weledi kimataifa kwa utoaji wa huduma kuliko ofisi zetu za umma ikiwamo mashirika na taasisi mbalimbali za umma yaani wamezidiwa weledi na wahudumu wa bar ya kitambaa cheupe ya tabata na sinza,
Hahaha!jomba hatari na nusu.

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
NSSF
Naona wako kawaida
Labda muda wa mafao ndio wawe wazinguzi

HESLB wanaringa kuna muda, kuna muda wanakutreat poa.

AIR Tanzania - Arusha wako poa

Precision Arusha wako poa sana

UTT hawako serious na kazi

Kwa Mkuu wa Mkoa niliendaga nilipata huduma poa kuanzia getini, mpk nilikoelekea.
 
Africa is dark continent,
Ndio maana Magu hakuwa na muda na watumishi wa Umma,

Binafsi tangu mwezi 6 mwaka jana nahangaika na Loan board HESLB)
Wanipe loan statement bila mafanikio.
Mhhh
Hiyo kitu si ya dk 20 tu unapewa?
 
Africa is dark continent,
Ndio maana Magu hakuwa na muda na watumishi wa Umma,

Binafsi tangu mwezi 6 mwaka jana nahangaika na Loan board HESLB)
Wanipe loan statement bila mafanikio.
Tena hao ni wajinga kabisa. Watu wanamaliza mikopo wanaendelea kukatwa. Wengine wanakatwa hawakuchukua mkopo.

Mimi walinikata zaidi,wakaniambia nidai watarejesha huu mwaka wa tatu.
 
Huu ni ukweli aisee tuseme ile hali..

Kazi nyingi hazifanyiki coz sisi wabongo ni washamba sana kuridhika mapema.

Ipo hivi watu wanatengeneza mazingira ya kuleta story na mambo ya mtaani ofisi while ni mda wa kufanya kazi ..wanawake ni wanaboa sana wao utani na mambo ya nyumbani kazini.

Mwaka Jana palikuwa na staff mmoja wa kike alikuwa anataka kuolewa basi ile week moja kabla pale ofisi imekuwa ndo sehemu ya maandalizi yaani wanawake wanaboa mara waje na nguo za sare pale kuonyeshana ,mavigelegele kibao,kupenda makundi dk mbili mtu katoka section yake kaja kwa mwingine ni stori tu na Kuna wanaume pia.

Kingine unakuta wanawake hao waliokuwa na mimba au walijifungua basi wanatoka mda kabla ya muda husika ili kwenda nyonyesha ni very boring katika utendaji kazi kwa kweli waliangalie hili wanawake sio wa kuwategemea ..Mwaka Jana tulipata usumbufu coz wanawake wawili walijifungua nafasi zao itabidi sisi tureplace wakati tuna kazi zetu kazi ngumu kwa kweli .

Africa wengi ni washamba wanashindwa kutofautisha sehemu ya kazi na nyumbani pia wanaamini kweny uchawa yaani sio utendaji kazi kwamba yeye kupata safari nyingi ni kumshobokra bosi sio kufanya kazi kwa juhudi..Mtu anaweza kwenda safari ya kikazi ila kuja kuandaa ripoti ya hiyo kazi ni balaa.

Ukweli ni kwamba watu wapige kazi sio porojo na kukalia majungu .
 
Mhhh
Hiyo kitu si ya dk 20 tu unapewa?
Ndio hivyo Makuu,
Nilichoambiw ni kwamb Kwenye mfumo wao,

Kuna miezi nimekatwa lakini haionekani, na deni halipungui, hivyo taarifa zangu pia hawajaziwek sawa,

Hivyo wanashughulikia tangu mwezi wa 6 mwaka jana.

NIMEFATILIA Ofisini kwao mwanza, pale hawana ushirikiano, nikaenda dar,

Nilipewa ahadi tu,
Leo hii nikiangalia kwenye mfumo hamna progress yoyote,

Simu hawapokei, message hawajibu licha ya kufika ofisini kwao wote na wananikumbuk vzr.
 
Back
Top Bottom