Gazeti la Nipashe toleo la leo limeripoti kuwa mchakato wa kuifanya wilaya ya Chato kuwa mkoa mpya wa CHATO umekamilika rasmi na sasa anasubiriwa rais Samia kuitangaza kuwa mkoa tarehe 14/10/2021 hivyo kutimiza ndoto na maono ya hayati Dr Magufuli aliyekuwa rais wa 5 wa nKikao maalumu cha ushauri cha Mkoa wa Geita, kimeridhia kuanzishwa kwa mkoa mpya wa Chato na kupendekeza mkoa huo mpya kuwa na wilaya tano, huku mkoa mama wa Geita ukibaki na wilaya tatu.
Gazeti la Nipashe toleo la leo limeripoti kuwa mchakato wa kuifanya wilaya ya Chato kuwa mkoa mpya wa CHATO umekamilika rasmi na sasa anasubiriwa rais Samia kuitangaza kuwa mkoa tarehe 14/10/2021 hivyo kutimiza ndoto na maono ya hayati Dr Magufuli aliyekuwa rais wa 5 wa nchi yetu.
View attachment 1958050
Kikao maalumu cha ushauri cha Mkoa wa Geita, kimeridhia kuanzishwa kwa mkoa mpya wa Chato na kupendekeza mkoa huo mpya kuwa na wilaya tano, huku mkoa mama wa Geita ukibaki na wilaya tatu. Alisema kama vigezo vimekidhi suala hilo litakamilishwa, na kama havijakidhi watashauri namna ya kufanya ili vikidhi.
Kulingana na maelezo ya kikao hicho, Mkoa wa Geita utakuwa na tarafa 16, kata 108, vijiji 379 katika eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 23,697.55 lenye wakazi 2,668,173.
Aidha, mkoa mpya wa Chato utakuwa na tarafa 18, kata 87, vijiji 360 huku ukiwa na ukubwa wa eneo la kilomita za mraba 30,215.85, lenye watu 1,557,139.
Vigezo vya uanzishwaji mkoa
Kwa mujibu wa mwongozo wa Tamisemi wa mwaka 2014, vigezo vya kuzingatia katika kuanzisha mkoa ni pamoja na kuwa na ukubwa wa eneo lenye kilomita za mraba usiopungua 20,000. Pia kuwa na wilaya nne, idadi ya watu isiyopungua asilimia tatu ya idadi ya kitaifa, tarafa zisizopungua 15, idadi ya kata zisizopungua 45 na idadi ya vijiji visivyopungua 150.