SI KWELI PreGE2025 Nipashe wamechapisha taarifa inayosema Kibatala amtaka Lema kuacha kutumia kesi ya Lissu kujipatia fedha

SI KWELI PreGE2025 Nipashe wamechapisha taarifa inayosema Kibatala amtaka Lema kuacha kutumia kesi ya Lissu kujipatia fedha

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
SIKWELI_NIPASHE_6MEI25.jpg
 
Tunachokijua
Mnamo tarehe 09 Aprili, 2025 Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Tundu Lissu alikamatwa na jeshi la polisi mara baada ya mkutano wa hadhara alioufanya Jimbo la Mbinga mkoani Ruvuma na kusafirishwa hadi Dar es Salaam.

Aprili 24, 2025 Lissu alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashitaka matatu ikiwemo uhaini na kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao wa kijamii wa X ambapo kesi hiyo ilihairishwa hadi Mei 06, 2025.

Aidha tarehe 03 mwezi Mei Jopo la mawakili wanaomtetea Lissu walifanya mkutano na waandishi wa habari wakiongozwa na wakili Peter Kibatala ambapo alisema wameamua kuzungumza na waandishi wa habari ili kuwaeleza watanzania uhalisia wa masuala mbalimbali kuhusu kesi hiyo.


Madai

Kumekuwapo na Taarifa inayodaiwa kuchapishwa na Nipashe kuwa Wakili Kibatala 'amtaka Lema kuacha kutumia kesi ya Lissu kujipatia fedha'

Uhalisia

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia maneno muhimu ulibaini kuwa taarifa hiyo haikuchapishwa katika kurasa rasmi za Nipashe bali ni chapisho lililotengenezwa na wapotoshaji.

Hata hivyo madai hayo si ya kweli kwani katika mkutano na waandishi wa habari Kibatala hakutoa kauli yoyote iliyomhusisha Godbless Lema kuhusu kesi inayomkabili Tundu Lissu.

Aidha Kibatala alieleza kusikitishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Innocent Bashungwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Hamza Johari kwa kile alichodai kuwa ni kutoa kauli zinazoingilia uhuru wa mahakama na kuingilia kesi inayoendelea inayomhusu Lissu. Rejea hapa dakika 1:05:00 hadi 1:16:00

Pia aliongeza kuwa wataendelea kusisitiza haki ya wananchi kushiriki kwa uwazi ili wapate kujifunza kutokana na kesi hiyo.

“Tutaendelea kusisitiza haki ya wananchi kushiriki katika kesi yao kwa wazi ili wajifunze uhaini ukifanya unachakatwa hivi na adhabu yake ni.. Ili nao wasifanye uhaini, tutaendelea kusema mahakamani kinachofichwa ni nini?”​
Back
Top Bottom