Nipe sababu tatu unapenda kuishi ukanda gani mwa Tanzania?

Nipe sababu tatu unapenda kuishi ukanda gani mwa Tanzania?

Kijiji gani!
Achana na wale wa mjini mgeni akienda hasa wavuvi unakuta umeandaliwa mwanamke tayari ule ni uhuni..
Nitajie kijiji chenye mabaki ya waarabu halafu wanamaadili sahihi.
Wewe jamaa ni muongo sana
 
Kanda ya ziwa Napenda sana esp Mwannza Musoma hiyo masato yale ...furu..ningu wooii samaki watamu wale jamani ..usafiri ndege moja tu upo dar..Beach...japo gharama za maisha zipo juu bei za vyakula ss hazishkiki ndizi zinalimwa tarime hapo jirani lkn beinkali ndizi 1 00 while huiu ruvuma 2500 unapata mkungu mzima,viazi tele..maharage kibaao mahindi bwelele maparachichi mengi kila nyumba inamparachichi na mgomba cha ajabu wenyeji si wapenzi kiviiile lkn si sababu I love Lake zone japo nipo Ruvuma..
 
Kanda ya ziwa Napenda sana esp Mwannza Musoma hiyo masato yale ...furu..ningu wooii samaki watamu wale jamani ..usafiri ndege moja tu upo dar..Beach...japo gharama za maisha zipo juu bei za vyakula ss hazishkiki ndizi zinalimwa tarime hapo jirani lkn beinkali ndizi 1 00 while huiu ruvuma 2500 unapata mkungu mzima,viazi tele..maharage kibaao mahindi bwelele maparachichi mengi kila nyumba inamparachichi na mgomba cha ajabu wenyeji si wapenzi kiviiile lkn si sababu I love Lake zone japo nipo Ruvuma..
Kama unataka kuendelea Baki huko huko Ruvuma ila kama unataka umaskini na kansa Rudi kwenu Kanda ya Ziwa
 
Nimezaliwa na kukulia ukanda wa Pwani nimesoma Dodoma, Iringa na Mtwara yaani O Level, Chuo na Advance, kwa Mtwara shule ni hapo Ndanda ulipopasema. Vijiji vya Mwena, Mkalapa n.k Vibe la Dar tangu nikiwa mtoto. Nimeishi nikifanya kazi Mwanza mjini. Nimefika Geita, Musoma, Mara mpaka Sirari, Kahama, Simiyu hasa Bariadi bila kusahau kisiwani Nansio, Ukerewe kupitia Bunda.
Nimefika Singida, Tabora, Mbeya, Nachingwea, Masasi, Kilwa zote, Lindi, Nanyumbu, Newala, Tandahimba na kijiji kimoja kinaitwa Kitaya Mtwara Vijijini.
Dar es Salaam yote nimeivuruga. Professionally nimekuwa sales manager hapa Dar so najua chocho nyingi hadi nje ya mji kama Zingiziwa huko. Nishafika hadi Pemba Mnazi Kigamboni. Kiufupi hakuna sehemu siijui hapa DSM.......kuna barabara 1 tu sijawahi kupita. Kutoka Madale kupitia Mbopo kwenda Mabwepande.

Nimefika Tanga, Kilimanjaro, Arusha hadi Babati na Kondoa, Mbulu hadi Karatu.
Sehemu ambazo sijawahi kufika kabisa ni mkoa wote wa Songwe, Rukwa na Katavi, Kigoma na Kagera, Pemba na Songea mjini. Tunduru nilifika.

Tofauti na huku ukanda wa Pwani, nipeleke tu Mwanza kaniache, kanda ya ziwa Yaani Geita, Kahama, Mwanza comes first of all.
Reasons:
1. The people......The Sukuma are friendly, above all the city has a mixture of people of diff tribes making it a small Dar. The Haya, the Ha, Chagga, Kurya and the local Sukuma make the most business people in the city without forgetting Hindus and Arabs.

2. The economy......Mwanza is more or less like Dar in almost everything.
3. The weather....moderate temps just like Dar

I love Mwanza.
Pamoja na sifa zote mnazoipaga Mwanza ila watu Wana make pesa Dar,Arusha na Dom huko kwingine ni second hand choice
 
Mzee baba umechambua vizuri sana,,sema pale ndanda ni kama ujerumani mwanangu yaani kule water source ni kama ardhi iliyomegwa kutoka ujerumani na kuwekwa pale 😂😂😂
Ndio mana ndanda inaitwa kipande cha ulaya
 
Nimezaliwa na kukulia kanda ya kati ila Shule nimesoma sana kanda ya pwani ya mashariki dar na maisha ya kikazi nikatupwa kanda ya kusini na bahati nzuri field zangu nimebahatika kufika wilaya zote za mtwara lindi na ruvuma nimezizungikia zaidi ya mara kumi.sababu tatu kwanini ukanda wa kusini umeninogea sana ni AMANI,UOTO WA ASILI NA VIBE.

1.Aman;Watu wa huku ni wastaarabu sana sio rahisi kukuta wakigombana hakuna migogoro wala kesi kubwakubwa ukitoa tukio la jamaa wa madini kuuwawa sijawahi kusikia lingine matusi wanatukanana ila yanaisha juu kwa juu ni kama sehemu yao ya utani .huku hata ukiwa na tabia za seleman kushika wake za watu kwenye pombe hupigwi unaangaliwa tu hakuna wivu wa kimapenzi maana kuachana ni suala la dakika tu.

2.UOTO WA ASILI;kuanzia kipande cha kilwa kivinje ,mpara na masoko hali ya hewa ni nzuri pale kisiwani waarabu walishakula bata long time ago njoo mpaka mchinga na kijiweni kuna beach nzuri na mabaki ya watoto wa kiarabu njoo mpaka kwenye mashamba makubwa sana ya minazi ng’apa ni kuzuri lindi yenyewe iko shimoni sawa na 0 usawa wa bahari pamoja na mabonde ya Rutamba Milola na rondo plateu miliman kama uko ulata elevation ni 500 m toka USawa wa bahari.milima ya rondo inamwaga maji kuja nyangao mto lukuledi pamoja na Makonde plateau huko newala ubaridi kama ulaya chini kidogo utakutana na ndanda ukienda Tunduru Mbinga songea ndo pazuri ajabu mto ruvuma unafanya pawe na ubichi huku wamatengo na wangoni wakichapa kazi kwa ukarimu.sijakupitisha selous na kwenye corridor za tembo kwa kweli kusini haijaharibiwa mazingira yake.

3.VIBE;mangoma unayoyasikia anayapiga mr miso misondo huku nimeanza kuyaenjoy miaka mitatu nyuma huku mtwara na lindi kuna unyago shughuli ambazo zinaanza na kigodoro kinakesha kisha kesho yake unyago unachezwa watu wanaonyesha utaira kama wazee wa makoti .kunakuwa na chama kinakuja kukushika mkono. Aisee wakilewa fujo lake balaa mixer kujimwagia mavumbi ila uzuri hakuna ugomvi hata kidogo ndo maana lile vibe la mr misondo sisi huku tunaona kawaida sana hata hizo ngoma anazopiga ndo zinazorudiwa huku zilezile.

Changamoto kubwa ni upatikanaji wa vyakula jamii ya nyama za kuchoma tushazoea minadani nyama zinachomwa huku hakuna na pia maokoto sio sana maana viwanda vichache atleast vingejengwa kama vya dangote hata vitano aisee huku pangekuwa best place kuishi .
karibu tarime
1.Hali ya hewa nzuri sana
2.hawapendi mambo ya kijinga, hata mbowe akizingua tunamtoa nduki, wale wa kijani wanaatujua vizuri
3.usafiri wa uhakika, tuna enjoy mahitaji kutoka nchi jirani
 
Back
Top Bottom