Hayo masaa 10 unaweza ukayapunguza kuwa 7?
Jamaa kasema ana ford, tupige mahesabu!!
Akitoka Mwanza hadi Shy town ni mwendo wa 100km/hr, average kwasababu barabara hiyo sio nzuri sana!!
Ukitoka Shy town hadi Tinde hakuna kona kali sana na tuta kali hapo ni moja tu liko eneo linaitwa Nyeregeni, unaingia, Samuye Usanda, Tinde hapo average speed ni 150km/hr...road iko vizuri...
Ukitoka Tinde hadi Nzega pia road iko vizuri, hakuna kona kali wala matuta mazito speed unapunguza kidogo kwenye matuta ya mto Manonga.
So Tinde To Nzega hapo average speed ni 140km/hr at kuna vimji vidogo huwezi pita kwa kasi hasa pale Nata...
Ukitoka Nzega to Igunga kama uko vizuri barabarani na Ford unayotumia iko vizuri average speed ni 160km/hr.
Igunga to Shelui kuna eneo moja tu korofi pale kwenye mpaka wa mkoa wa Tabora na Singida so hapo average inaweza kuwa tena zaidi ya 160km/hr.
Shelui hadi kufika mteremko wa Senkenke kupandishia Misigiri ni almost 80km/hr.
Upite kwenye berrier ya Misigiri.
Baada ya Hapo ni Goti hadi Singida town, barabara ni myoko sana, isipokuwa kwenye ile kona ya barabara inayoelekea Kiomboi... Makadirio ya Misigiri to Singida town average speed ni 150km/hr...
Singida to Manyoni pana mnyooko poa sana, achilia vimatuta vichache vichache kama vile pale Puma na visehemu sehemu... Average speed hapa nampa tena 150km/hr.
Changamoto kidogo ni Manyoni to Bahi hiyo Saranda ndogo ukishuka kiboya inaweza kula kwako... Average speed 100km/hr.
Bahi to Dodoma town pazuriii hapo hata unatembea kwa wastani wa 150km/hr.
Dodoma hadi Gairo 130km/hr.
Gairo to Moro 120km/hr...
Moro to Chalinze 130 hadi 140km/hr...
Chalinze to Dar almost average speed ni 110 hadi 120km/hr...
Wastani wa jumla hapo ni karibia 135km/hr kwa muda wote...
Umbali wa Mwanza to Dar ni Karibia Km 1100 hivi...
So ukiwa na gari nzuri na mzoefu wa Barabara Mwanza to Dar kwa masaa 8 unatoboa kabisa...