RD07
Member
- May 5, 2024
- 52
- 90
Muhali gani wana JF,
Ebana nahisi na naamini hii tabia sio mimi pekee ambaye ninayo, Naomba wenye tabia kama hii tukutane hapa na tushauriane mnaweza vipi kuji control?, au wataalamu wa Saikolojia watusaidie.
Ni kuhusu tabia ya MOYO WA MSHUMAA (Unaungua na kuteketea ili kuwamulikia wengine).
*
Kiukweli nashindwa kuiweka vizuri ila tuu ni ile hali ya kupenda sana kusaidia wengine, kuwa tayari hata kujinyima ili kusaidia wengine, na pindi naposhindwa kusaidia huwa naumia na kusononeka sana moyoni.
*
Ila changamoto inakuja kwamba, mara nyingi huwa sipokei ile thamani ninayostahili kulingana na juhudi nilofanya kujitolea, na hata pale mimi napohitaji msaada kwao au wengine inakuwa changamoto kuupata ama nisiupate kabisa hadi najiuliza mbona mimi naguswa sana na shida zao ila wao hawaguswi na zangu?
Mf. Namkopesha mtu pesa na nisilipwe pesa hizo, au kumkopa niliyewahi kumkopesha na asiguswe na shida yangu n.k.
<> Kuna wengine wananiambia nijifunze kuwa na roho mbaya ndo ntaweza kuendana na Walimwengu, Namimi wakati huo nikiwa na hasira na masononeko najiapiza kuwa sitosaidia mtu tena, kwamba sitokubali kuwa mjinga tena ila najikuta baadae nafanya yaleyale tena nilosema sitofanya (kusaidia).
*
Madeni mengi sana nishayasamehe kwa watu, nakosa ujasiri wa kumpigiapigia simu mtu ili kumkumbusha anilipe najiona kama nakuwa ombaomba kwake, so naonaga bora nipotezee tuu maisha yaendelee, nyingine za kudhulumiwa ndo usiseme.
*
Tunaambiwa kutoa ni Baraka, na anayetoa anaongezewa ila kwa upande wangu hata sio kama nina utofauti wowote kiuchumi, badala yake bado nipo chini tuu...
Badala yake nawaona wale wenye roho mbaya ndio wanaopiga hatua kimaendeleo.
Naomba kuwasilisha.