Melki Wamatukio
JF-Expert Member
- May 3, 2022
- 6,156
- 10,974
Kuna mwanamke fulani hapa jirani, japo si jirani kivile nilitokewa kuvutiwa naye, na mpaka sasa navutiwa naye. Kwa mara ya kwanza kumuona nilijikuta namshangaa hasahasa macho yangu yalipokutana na mtrako uliotawanyika huku ukipepesuka huku na huko, mnara ulisoma 6G nikajikuta naunga naye njia moja hadi pale nilipopamia sinia la kashata. Huyo mwanamke alinikodolea macho kupita maelezo, na mimi nikajikuta namtupia tabasamu zito muda huo nikila makonde ya mgongo kutoka kwa wafanyabiashara wenye hasira kali
Kwa kuwa karibu na nilipopanga ni njia ya yule mwanamke nikaona wacha nimlie rada. Cha ajabu kila wakati alipopita alinikuta nikiwa na nzi, hivyo ikaniwia ugumu kujichoresha japokuwa kwa muda wote huo mama wa watu alikuwa akinitazama sana kila aliponiona
Huyu mwanamke amenizidi vingi sana, cha kwanza ni umri, kuna gape la miaka 9, cha pili familia, yeye ni Mama X wa mume Y ila mimi ni team Nay wa Mitego aka Bado nipo nipo kwanza almaarufu kama mwanachama wa kataa Ndoa, pia huyo mama ana kazi yake nzuri tu inayotambulika kiserikali, ila mimi kazi zangu ni njunga njunga, unaweza kunikuta kwenye kioski cha matunda kumbe nauza mundende kisirisiri. Lengo langu sio pesa zake, kikubwa nahitaji utamu wake hata kama akiwa ananigeia walau dozi ya mara moja kwa mwezi
Nimekuwa nikiwasiliana naye kwa macho kila nilipomuona. Kuna siku alikatiza tukatazamana, nikamwambia kuwa ananivutia sana, natamani walau kumkumbatia. Nikamwambia pia tutafanya siri, tena siri ya watu wawili, japo sikumtamkia maneno waziwazi ila nilimwambia kimoyomoyo kupitia mtazamano tuliokuwa nao
Siku ya leo nikaamua kujikaza, nikajitoa kimasomaso na kuanza kumuimbisha. Wakati wa mtongozo mzima alikuwa akinitazama tu, nilipohitimisha na kituo amecheka sana, kisha kuniambia "kuwa na adabu", akarusha nywele yake moja ikaning'inia mbele ya uso kuziba jicho moja, kisha akaondoka zake
Walahi tena hata ile kunitizama tu kwa umakini nilijikuta niko hoi taabani, ile ameondoka mbele yangu, nikajikuta niko kwa Mangi nanunua malaika
Nifanyeje kumkoleza, maake naona dalili za kupoteza mbususu