Nipeni ushauri biashara ya dobi

Nipeni ushauri biashara ya dobi

October man

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2017
Posts
3,635
Reaction score
5,012
Salaaam wakuu,

Nina wazo moja la kufanya biashara ya dobi. Ndugu yangu mmoja alishawahi kuwa dobi alikuwa anafua nguo na kupiga pasi kwa siku alikuwa analaza around 10,000/= mpaka 15,000/= alikuwa anafanyia uswahilini tu.

Mimi ninataka nifanyie sehemu wanapoishi watumishi wengi kama maeneo yenye apartments za wafanyakazi, national house nk. ila sijui nianzie wapi na sijui sehemu nzuri ni wapi. Changamoto nyingine, kweli nitapata wateja maana nyumba nyingi zinaongoza kuwa na wafanyakazi wa ndani wanaofua nguo na kunyosha pasi nguo za maboss wao hata wasiokuwa hivyo wanapasi zao za umeme.

Vipi nitaliendea hili jambo? Nitapata wateja? Nitapata sehemu?
 
Umejiandaa vipi upande wa Jua na Mvua. Maana balaa la mvua unalijua! (kuna mashine za kukausha usiwaze)
We fungua wateja tupo! Suala la eti karibia kila nyumba kuwa na mfanyakazi usiwaze.

Ukute huyo mfanyakazi atakuwa anapewa hela ya sabuni afue nguo, yeye anakuletea wewe mnagawana umasikini, si unaona maisha yalivyo simple.
 
Utapata mkuu..hakuna biashara isiyo na wateja kikubwa location
 
Wazo zuri sana...kwa kuanza nakushauri nenda kwenye hostel za wanachuo huko wateja utawapata wengi hasa hostel za boys hata girls pia

Wakati huo ukijipanga kutafuta sehem rasmi ya kufanyia shughuli yako
 
Back
Top Bottom