Kiti Chema
JF-Expert Member
- Oct 18, 2017
- 1,793
- 1,961
Habari wana Jf. Bila kupoteza mda niende moja kwa moja kwenye lengo, mimi tangu mwaka jana niliajiriwa kwenye kampuni ya mtu binafisi,
Kipindi ninaajiriwa msimamizi mkuu walikuwa ni wahindi baada ya kama miezi 4 wale wahindi wakaondoka kwao wakafanya kumkabidhi MTANZANIA ili aimiliki hiyo kampuni baada ya hapo ndipo maisha ya kufurahiya kazi yalitoweka nikaanza kuteswa kwa kupewa kazi nyingi ambazo zilinilazimu kutoka usiku wakati nimeingia muda wa kazi asubuhi saa 2:00, na tena kutumia computer mpaka macho yanauma kutokana na kazi nyingi.
Baada ya hapo yule Boss wangu mpya akanipunguzia mshahara pia na pesa ya chakula na chai ikapunguzwa. Me nilivumilia lakini jambo lililonifanya kuandika uzi huu yaani tangu mwezi wa kwanza mwaka huu mpaka mwezi wa tano sikulipwa hata mia katika mshahara wangu maana kila nilipokuwa nikidai yeye anasema nivumilie kampuni imeshuka katika kiwango cha mapato.
Uamuzi niliouchukua niliamua kuacha kazi na kila nikimdai anasema kuwa deni halifungi hata nikienda kushitaki haita saidia lolote.
NAOMBENI USHAURI JE NIENDE KUDAI HAKI YANGU KWENYE VYOMBO VYA SHERIA AU MUNGU NDIYE ATAFANYA KISASI MWENYEWE
Na sheria ya kazi inasemaje maana ninachohofia mimi sikupewa mkataba au karatasi ya kusaini wakati naingia ktk kazi hiyo