Nipeni ushauri: Je, nimpeleke kwenye vyombo vya sheria au nimuachie Mungu?

Hapo ukienda kwenye vyombo vya sheria kuna mawili.. Either boss wako akubali kwamba ulikuwa mfanyakazi wake afu kesi itakuwa kwake kwanini hakukupa mkataba wa kazi hapo lazima akulipe pia upande mwingine akikataa kwamba ww cio mfanyakazi wake kesi itakuja kwako kwanini ulikubali kazi bila mkataba kuna possibility ya kulipwa au husilipwe maana unaweza aambiwa utafute mashahidi ili waje kukutetea au kesi ikawa imeishia hapo na hela huwezi pata..
NB.. Kama unataka kwenda kwenye vyombo vya sheria tafuta wakili ambae yupo vzur
 
aisee pesa hizo zinanipa mawazo sana nitaziripwa kwa njia gani.
 
Kazi umeacha lini? Uko mkoa gani?
Nenda Tume ya usuluhishi na uamuzi (CMA) ya eneo ulilokuwa ukifanyia kazi ukafungue shauri dhidi ya kampuni uliyokuwa ukifanya kazi.

Hapo kuna constructive termination, mwajiri kafanya mazingira ya kazi kuwa magumu kwako...
Na ukashindwa kuendelea na kazi.
 
Wanasema huwezi shindana na bosi wako hata ukienda huko vyombo vya sheria unaweza udhulumiwe haki yako maana mkubwa ndie anaetazamwa zaidi so we kama ni mtu wa MUNGU mwachie yeye atakunyanyua tuu.
Kwa mfano huyo bosi unataka uniambie hajui kuwa unamdai? ni wewe peke yako unadai au kuna wenzio? after all haki itendeke haijalishi wangapi mnadai...
Mpe last warning asipokulipa nenda zako MUNGU hamtupi mja wake.
 
Kuwa na mkataba wa kazi au kutokuwa nao ni immaterial, kwanza ni kosa kwa mwajiri kutokutoa mkataba. Hivyo, vitu kama kiambulisho cha kazini, salary slip, attendance register inatosha kuonyesha kuwa ulikuwa na mkataba.

Siyo kweli kwamba deni halimfungi MTU, kuna wafungwa wa madai. Hivyo, hizo in porojo tuu za mtaani. Kama hakulipi na anamali, naiwapo umeshinda shauri, Mali hupigwa mnada ili ulipwe madai yako.

Hata hivyo, yawezekana umeshachelewa kufikisha malalamiko yako kwenye mamlaka husika, I.e CMA
 
hapana mkuu me nalinda usalama wangu kwanza. Nashukuru kwa mchango wako tu
Haijawahi kutokea mtu alie wahi kudai haki kwa uoga na akafanikiwa. Kwataarifa yako haki haijawahi kuombwa, bali hudaiwa. Na uoga wako ndio Umasikini wako.
Kwa mawazo yako ninavyo kuona, nibora ukamuachia tu Mungu, kama ulivyo tangulia kusema mapema
 
Deni halifungi ila utapata haki yako. nenda ukamshitaki huyo tapeli. kwanza ueme alikunyima mkataba ama ulipenda mwenyewe kutopewa huo mkataba.
 
sikupewa mkataba wowote. Kumbuka hii ni kampuni binafsi me niliitwa na kuwapa vyeti vyangu walipovithibitisha wakasema anza kazi ikawa asubuhi nikiingia nasain tu basi siku zinaendelea mwisho wa mwezi napewa changu
Kama huna mkataba lakini ulikua unasaini kitabu cha mahudhurio at least yanazungumzika. Nenda mbele fasta
 
mkuu lakini kuna jamaa tuliyekuwa tunafanya naye kazi na yeye aliondoka hivi nikimuita si anaweza kuwa kama shahidi wa kunitetea
Umefanyakazi kiswahili sana...kubali matokeo Mahakama itahitaji Document
 
Kuwa na mkataba wa kazi au kutokuwa nao ni immaterial, kwanza ni kosa kwa mwajiri kutokutoa mkataba. Hivyo, vitu kama kiambulisho cha kazini, salary slip, attendance register inatosha kuonyesha kuwa ulikuwa na mkataba.

Siyo kweli kwamba deni halimfungi MTU, kuna wafungwa wa madai. Hivyo, hizo in porojo tuu za mtaani. Kama hakulipi na anamali, naiwapo umeshinda shauri, Mali hupigwa mnada ili ulipwe madai yako.

Hata hivyo, yawezekana umeshachelewa kufikisha malalamiko yako kwenye mamlaka husika, I.e CMA
Very right, attendance peke yake inatosha! Kitambulisho, na mengine yatafuata tu.
 
Hiyo attendance anaimiliki yeye au Mwajiri wake
Hahahahah swali gani hili? Tangu lini mfanyakazi akamilliki attendance register? Najua unachotaka Kusema but hawezi kuitupa attendance register au kumfuta Kwa namna yoyote! Ile attendance lazima atatakiwa aipeleke CMA
 
Bado sheria iko upande wako, ukisoma vizuri sheria ya ajira na kazi ya mwaka 2004, kuna mkataba wa kuandikwa na mkataba wa kutamkwa,
Nenda kwa watu wa sheria watakusaidia, sema yote hata kama hukupewa likizo we sema yote
 
Wanasema huwezi shindana na bosi wako hata ukienda huko vyombo vya sheria unaweza udhulumiwe haki yako maana mkubwa ndie anaetazamwa zaidi so we kama ni mtu wa MUNGU mwachie yeye atakunyanyua tuu.
Kwa mfano huyo bosi unataka uniambie hajui kuwa unamdai? ni wewe peke yako unadai au kuna wenzio? after all haki itendeke haijalishi wangapi mnadai...
Mpe last warning asipokulipa nenda zako MUNGU hamtupi mja wake.
tupo wawili tu tunaodai badi anayedai pesa nyingi ni mimi tu jamaa yangu yeye anadai kama mshahara wa miezi 2.
 
Bado sheria iko upande wako, ukisoma vizuri sheria ya ajira na kazi ya mwaka 2004, kuna mkataba wa kuandikwa na mkataba wa kutamkwa,
Nenda kwa watu wa sheria watakusaidia, sema yote hata kama hukupewa likizo we sema yote
asante kwa ushauri ndugu yangu
 
sikupewa mkataba wowote. Kumbuka hii ni kampuni binafsi me niliitwa na kuwapa vyeti vyangu walipovithibitisha wakasema anza kazi ikawa asubuhi nikiingia nasain tu basi siku zinaendelea mwisho wa mwezi napewa changu
Hapo hauna chako mkuu
 
Ulitakiwa kuliiba daftari la kusain
 
Back
Top Bottom