Sikuwahi kutarajia hii hali. Nina mshikaji wangu ambaye tulikutana kwenye kituo cha kazi mkoa x kipindi hicho mimi ndo nimetoka kumaliza chuo. Hatuzidiani sana umri sema mimi ndo namzidi jamaa kama mwaka mmoja. Ila yeye alitangulia kuoa, so nikawa nampa heshima zake. Mwaka huo huo mimi nikaoa, na yeye akajitwisha jukumu la kuwa msimamizi wa harusi yangu. kuanzia hapo urafiki wetu ni zaidi ya urafiki, na zaidi ya undugu. Yeye ni mtu wa connections sana so amenivusha kwenye mitihani mingi ya maisha.
Kuna wakati nilikuja kugundua jamaa ni mtu wa michepuko sana ila ni mjanja sana hadi kuja kugundua inahitaji akili ya ziada. Pia anamiliki mguu wa kuku ni aina ya wale watu muda wowote anasepa home na haijulikani anarudi lini, na namba nyingiiiiii za simu. Sitaki kufungua codes zaidi ya hapo najua mtakuwa mmeshaelewa huyu mtu ni wa aina gani. Kilichofanya nijue kama ni mtu wa michepuko kuna wakati tunabadilishana magari, anaweza kuniachia gari lake nikae nalo hata wiki, au yeye akachukua langu mimi nikabaki na lake. Sasa kuna vitu alikuwa anavisahau kwenye gari (i hope you understand). Ila siwezi kupata details za mwanamke yeyote anayetoka naye. Kwenye hii fani nampa heshima zake.
Mambo mengi yametokea kadiri miaka ilivyosogea. Inaonekana kuna baadhi ya codes zake mke wake kashazifungua na hawako in good terms any more. Mojawapo ni nyumba aliyoijenga hadi akamaliza bila wife kujua na akaja kujua baadaye. Kuna kipindi shem alinipigia akaniuliza baadhi ya mambo kwa kweli nikamwambia sijui chochote (na kweli sina details zozote), hata anazonisimulia shem sizijui. Sasa kadiri miaka inavyosonga mambo yanazidi kwenda mrama. Kuna siku shem akanipigia na kuniambia mume wake ana wanawake wengi siyo chini ya 15, na kuwa amechoka na hajui la kufanya. Leo hii amenipigia akiwa anatembea barabarani, nilivyopokea simu akawa anaongea kama mtu aliye msibani, anaongea huku analia. Amelemewa na mawazo kiasi kwamba ananitafuta tuonge mimi na yeye. Sasa i smell something fishy. Yeye na mke wangu ndo mabest wanapigiana simu wanajuliana hali. ila sasa hataki kuongea na mke wangu anataka kuongea na mimi tukiwa peke yetu, anasema atatafuta sehemu peke yetu.
Huyu jamaa siyo kwamba tuna ukaribu kivileee. yaani aliniwekea boundary kubwa sana kiasi kwamba hakuna yale mazoea ya kutaniana au ile hali ya kumchana mshikaji. Kuna wakati inaweza kupita miezi hata mitatu hatujawasiliana na tukiwasiliana ni very brief. so hakuna muda wa kujua details za mwenzako. siri zangu ni zangu na siri zake ni zake. Huwa tunawasiliana pale ambapo kuna issue muhimu baada ya hapo mawasiliano yanakata. Sasa, nimewaza sana. huyu shem anataka tuongee nini na nimshauri nini? Je, what if anataka kulipiza kisasi kwa kudate na mimi kama namna ya kujiliwaza? Na jamaa akijua nawasiliana na mke wake (hata kama hatufanyi lolote) nini kitafuata. Sasa nimemblock shemeji aache kuchat whatsaap wala sms. Nimemwambia kama kuna issue tafuta muda nipigie kawaida tuu, maana whatsaap na sms mtu anaweza kuhack.
Roho inaniuma maumivu ya huyu mwanamke mtoto mzuri asiyechuja sura angavu. Lakini siwezi kumshauri lolote maana atakachoniambia mimi sina namna ya kuprove kama ni kweli au uongo. Na hata kama najua siwezi sema lolote kwa sababu madhara yake ni makubwa kuliko faida. Nifanyeje katika hali hii wakuu? Ninavyozidi kumkaushia shem ndo anaona mimi najua issues za jama na ninamkingia kifua jamaa. Lakini nikiruhusu kuwa na ukaribu na shem siku jamaa akijua bastola itanihusu. Hii ndo inaitwa njiapanda/dilemma.